*Mexico washinda na kuwatoa Croatia
*Uholanzi wasafi, Hispania wajiliwaza

Brazil wamefanikiwa kufikia hatua ya 16 bora baada ya kuwashikisha adabu Cameroon kwa mabao 4-1.
Neymar wa Barcelona alifunga mabao mawili na alikuwa mchezaji bora wa mechi ambayo Samba Boys walicheza vyema hasa katika ushambulizi.

Fred na Fernandinho walifunga mabao mengine mawili huku Cameroon waliomaliza mashindano wakiwa wa mwisho kwenye kundi lao wakifuta machozi kupitia kwa Joel Matip.

MEXICO WAWAPIGA CROATIA NA KUVUKA

Mexico wameungana na Brazil kuingia hatua za mtoano baada ya kuwafunga Croatia katika mechi ambayo mshindi yeyote angevuka.

Rafael Marquez aliwaongoza Mexico kwa bao la kwanza kabla ya Andres Guardado na Javier Hernandez kumalizia udhia na kutoka na ushindi wa 3-0.

Croatia walishindwa kabisa kuonesha cheche kwenye mechi hiyo muhimu licha ya kuwa na wachezaji kama Luka Modric ambaye hakufurukuta lakini Ivan Perisic alifunga bao la kufutia machozi.

UHOLANZI WAWAPIGA CHILE

Uholanzi wamemaliza hatua ya makundi kwa ushindi wa asilimia 100 baada ya kuwafunga Chile 2-0, lakini timu zote zimesonga mbele.
Mabao ya Wadachi hao yalifungwa na Leroy Fer na Memphis Depay.

HISPANIA WAJILIWAZA KWA USHINDI

Mabingwa watetezi waliovuliwa taji la dunia, Hispania wamemaliza mechi zao kwa kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya vibonde Australia.

Hispania waliotolewa kwa aibu baada ya kufungwa mechi mbili za mwanzo walipata mabao yao kupitia kwa David Villa, Fernando Torres na Juab Mata lakini hayakuwasaidia kitu zaidi ya heshima kidogo tu.

Kocha wa Hispania, Vicente Del Bosque amesema bado anatafakari iwapo ataachia ngazi au la wakati chama cha soka nchini mwake kinamtaka aendelee na kazi hiyo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Taifa Stars kuzivaa Botswana na Lesotho

Ivory Coast watolewa kiutata