in , , ,

Bayern wawapa kipondo Barcelona


*Messi ndani, ashuhudia wakilambwa 4-0

Nyota ya Bayern imeng’aa mbele ya timu inayodhaniwa kuwa bora zaidi duniani Barcelona kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa Ulaya.
Wakicheza nyumbani kwao Munich, vijana wa kocha
Jupp Heynckes anayestaafu mwisho wa msimu huu, waliwachakaza Barca 4-0.
Mabao ya Bayern yalitiwa kimiani na Thomas Muller aliyefunga mawili, Mario Gomez na Arjen Robben na kuwaweka Bayern wakipewa nafasi ya kutwaa kombe hilo.
Heynckes alionya mapema kwamba hakuwa na wasiwasi na kurejea kwa mchezaji bora wa dunia Lionel Messi kwenye kikosi cha Barca kwa mechi hiyo.
Hata hivyo, Messi hakutamba, na mara kwa mara wachezaji wa Barca walionekana kumlalamikia mwamuzi, ikiwa ni pamoja na baada ya Robben kufunga bao, kwani beki wao aliangushwa katika eneo la hatari.
Barca, hata hivyo nao baadaye walicheza hovyo wakionekana kuwa na hasira, kama Jordi Alba aliyempiga Robben na mpira kwa kumrushia usoni wakati akiusubiri kwa ajili ya kurusha.
Messi aliyeumia katika mechi ya robo fainali ya kwanza dhidi ya Paris Saint-Germain , aliingia na kucheza dakika 30 za kipindi cha pili na kuiwezesha timu yake kuwashinda PSG.
Aliingia baada ya PSG kuelekea kuwazidi nguvu, licha ya kwamba hakuwa fiti vya kutosha. Barca walivuka kwa faida ya bao la ugenini.
Hata hivyo, Bayern waliwafunika Barca wakiwa imara kila idara, huku Messi akionekana kuzuiwa hata kufurukuta.
Bayern walifanikiwa kumiliki mpira, wakifungua vyema vyumba na kuwazuia wapinzani wao katika karibu kila fursa wanazopata.
Barca wapo chini ya kocha Tito Vilanova ambaye licha ya kuwapo uwanjani, anaendelea na matibabu ya saratani ya koo. Kocha wao wa awali, Pep Guardiola ndiye anayemrithi Heynckes, tayari kuanza msimu ujao wa soka kitaifa na kimataifa.
Barca watakuwa na kazi ya ziada kwenye mechi ya marudiano nyumbani, ambapo watatakiwa kufunga walao mabao 4-0 ili kuwa na matumaini ya kuvuka kwa ama muda wa nyongeza au mikwaju ya penati.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

TAIFA STARS KUCHEZA MICHUANO YA COSAFA

Real Madrid nao waadhibiwa