in , , ,

Bayern klabu bingwa ya dunia

Bayern Munich wamejiongezea taji jingine baada ya kuwafunga Raja Casablanca ya Morocco 2-0 na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.

Katika mechi iliyopigwa jijini Marrakech kwenye falme ya Morocco, Wajerumani hao walijawa furaha kuongeza kombe hilo katika hazina yao ambayo tayari ina makombe ya ubingwa wa Ulaya,
Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Uefa Super Cup.

Raja walikuwa wanajaribu kuwa klabu ya kwanza ya Afrika kutwaa taji hilo, lakini waliparaziwa mbali na Bayern wanaofundishwa na Pep Guardiola kwa mabao ya Dante na Thiago Alcantara katika kipindi cha kwanza yalitosha kuwatangazia Bayern ufalme.
Hii ni rekodi kubwa kwa Guardiola, kwani katika kazi yake ya ukocha ametwaa kombe kama hili mara tatu, mara mbili za mwanzo akiwa na Barcelona 2009 na 2011.

Bayern walipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi japokuwa Raja walikuwa na uungwaji mkono wa washabiki wa Morocco. Hata hivyo, walichukuliwa kuwa timu dhaifu zaidi kwenye mashindano hayo lakini wakafanikiwa kuwafunga Auckland City, Monterrey na Atletico Mineiro ya Ronaldinho.

Bayern kwa upande wao waliwafunga mabingwa wa Asia, Guangzhou Evergrande kutoka China.
Mabingwa wengine wa kombe hilo kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka jana ni Corinthians, Sao Paulo na Internacional zote za Brazil.
Wengine ni AC Milan (Italia), Manchester United (England), Barcelona (Hispania), Inter Milan (Italia), Barcelona (Hispania) na Corinthians wa Brazil.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Simba wamestahili ushindi…

Everton watinga nne bora