in , ,

Barcelona mbendembende San Siro

*Wacharazwa 2-0 na AC Milan

*Galatasaray sare na Schalke

Fukuto la mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) limeishuhudia AC Milan wakiwatandika Barcelona mabao 2-0.

Walikuwa vijana wawili wa Ghana, Kevin Prince-Boateng na Sulley Muntari walipata kuchezea Ligi Kuu ya Uingereza waliowaaibisha Barcelona, kwa mabao yao ya dakika ya 57 na 81.

Baada ya kutawala kipindi cha kwanza kwa mbwembwe, zile pasi zao za uhakika, ulinzi wa kuaminika na mashambulizi yasiyo na shaka yalififia.

Mbele ya maelfu ya washabiki wa Milan katika uwanja wao wa San Siro wilayani hapo, Barcelona walionekana kuelemewa kadiri mchezo ulivyoelekea kumalizika.

Nje ya dimba, mchezaji tata wa Kitaliano aliyekuwa anacheza Manchester City, Mario Balotelli alionekana akishabikia mafanikio ya timu yake mpya na vimwana wa Milan.

Balotelli hawezi kuchezea AC Milan katika mashindano haya kwa vile alichakipiga akiwa na City msimu huu. Amefunga mabao katika mechi zote alizochezea Milan tangu ajiuge nao Januari hii.

Mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi hakuwa chochote mbele ya viungo na mabeki wa Milan, huku wachezaji wenzake wakionekana kuchoka, kana kwamba walikuwa wachache zaidi uwanjani.

Kwa matokeo hayo, Barcelona wanahitaji kufunga mabao mawili katika mechi ya marudiano ili wawe sare na wapinzani wao; atakeyeongeza bao ndiye atavuka kuingia robo fainali.

Barcelona wamekuwa chini ya kocha msaidizi, Jordi Roura, kutokana na kocha wake, Tito Vilanova kuwa likizo ya ugonjwa. Alifanyiwa upasuaji na uchomaji mionzi kutokana na saratani ya koo.

AC Milan wametwaa taji hili mara saba – 1963, 1969, 1989, 1990, 1994, 2003 na 2007. Ni Real Madrid pekee waliotwaa taji hili zaidi, mara tisa.

Barcelona ambayo ni klabu bora zaidi duniani, katika mchezo huo walionekana wa kawaida, na wameshafanikiwa kutwaa kombe hilo mara nne – 1992, 2006, 2009 na 2011. Mwaka jana waling’olewa na Chelsea.

Katika mchezo mwingine nchini Uturuki, Galatasaray walishindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani, kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Schalke ya Ujerumani.

Wenyeji waliongoza kwa kupata bao katika dakika ya 12 tu ya mchezo, kupitia kwa Burak Yilmaz aliyesukuma mpira kimiani akiwa ndani ya eneo la hatari.

Hata hivyo, wageni walipata bao muhimu la ugenini katika dakika ya 45 kupitia kwa Jermaine Jones kwa shambulizi la kushitukiza.

Galatasaray iliwachezesha kwa mara ya kwanza pamoja Didier Drogba na Wesley Sneijder, kocha wao, Fatih Terim akijinasibu kwamba watailetea timu mafanikio.

Drogba alijiunga na klabu hiyo ya Uturuki baada ya kuondoka Shanghai Shenhua ya China alikokaa kwa muda mfupi baada ya muda wake mrefu Chelsea kumalizika kwa kutwaa UCL dhidi ya Bayern Munich mwaka jana.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal watota kwa Bayern

Drogba wingu jeusi Ulaya