in , , ,

Balotelli aenda Liverpool


*Rojo kamili Man United, sasa  wamfikiria Xabi Alonso
* Chelsea kumtoa Torres, Arsenal bado wapo sokoni

 
Jitihada za Liverpool kuziba pengo la Liverpool zimewapeleka Italia, ambapo tayari wamekubaliana na AC Milan kumchukua mshambuliaji wao, Mario Balotelli.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City anasajiliwa Anfield kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 16 na sasa Liverpool watazungumza naye juu ya maslahi yake binafsi.

 Balotelli (24) atakuwa kwenye kikosi cha bosi Brendan Rodgers kinachosaka heshima nyumbani na Ulaya. Alijiunga Milan kwa pauni milioni 19 na kufunga mabao 30 katika mechi 54.

Alikaribia kusajiliwa Arsenal kiangazi hiki kwa karibu pauni milioni 30 kabla ya dili kusambaratika kutokana na kutong’ara ipasavyo kwenye michuano ya Kombe la Dunia, lakini pia Arsenal wakafikiria hatari ya tabia zake ndani na nje ya uwanja.

Liverpool wanakwenda Etihad Jumatatu hii kucheza dhidi ya Man City, na habari kutoka Italia zinasema kwamba tayari Balotelli ameshaaga. AC Milan wametangaza kwamba Balotelli ameshaondoka kwenye Kituo cha Michezo cha Milanello mchana baada ya kuwaaga wachezaji wenzake.

Liverpool walimuuza Suarez Barcelona kwa pauni milioni 75, akiwa ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, na pia mchezaji bora wa ligi hiyo maarufu zaidi duniani.

Liverpool walijaribu kuwashawishi Milan wawape mchezaji huyo lakini kwenye mkataba kuwe na kifungu kuwa lazima awe na tabia njema, vinginevyo arudishwe Milan, lakini Wataliano wamekataa.

Kwa upande mwingine, Liverpool walikuwa wanafikiria kutoa pauni milioni 22 ili kumpata mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao (28) kwa mkopo. Anawaniwa pia na Manchester United na Juventus.
 
 
Manchester United wamemsajili Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon kwa pauni milioni 16 na kuwapa Nani, juu ya fedha hizo.

Nani ambaye ni raia wa nchi hiyo, anakwenda kwa mkopo lakini United wataendelea kulipa mshahara wake kwa msimu wote wa 2014/15 atakapokuwa huko, kiasi cha pauni milioni 4.8.

Manchester United  wanafikiria kumsajili kiungo wa zamani wa Liverpool anayekipiga Real Madrid,  Xabi Alonso (32), huku wakiendelea vyema na mazungumzo ya kumsajili mchezaji wmenzake, Angel Di Maria (26).

Man U wamesema si kweli kwamba wamekuwa wakitaka kuwasajili Wajerumani, Thomas Muller na Marco Reus kiangazi hiki. Muller amesema United walimpa ofa akakataa. Bayern Munich wamedai wanataka kumsajili Sami Khedira.

Mshambuliaji garasa wa Chelsea, Fernando Torres (30) anatarajiwa kuondoka Stamford Bridge baada ya klabu yake kufanya mazungumzo na Roma ili wamchukue na wao kuwapa mshambuliaji Mattia Destro (23).

Arsenal wanaendelea na jitihada za kumsajili mlinzi Costas Manolas kutoka Olympiakos, hasa kutokana na kuumia kwa Mikel Arteta, lakini pia Arsene Wenger amefufua mbio zake za kumnasa Sami Khedira wa Real Madrid au William Carvalho wa Sporting Clube de Portugal anayewaniwa pia na Chelsea.

Arsenal wamewaambia Galatasaray kwamba wanaweza kumuuza  Lukas Podolski (29) na si Joel Campbell (22) ambaye klabu hiyo ya Uturuki inamtaka.

Arsenal wanachuana na  Lokomotiv Moscow ya Urusi kumsajili kiungo mkabaji wa Newcastle, Cheick Tiote (28). Kadhalika wanaweza kuwafunika Everton wanaotaka kumsajili kiungo wa Paris St-Germain, Clement Chantome (26) kwani The Gunners wanakaribia kumsajili Adrien Rabiot (19) na klabu hiyo ya Ufaransa inasema hawatawauza wachezaji wote wawili.

Monaco wanafikiria kupeleka posa Chelsea ili kumchukua kipa wao Petr Cech (32) aliyeangukia papili wa Thibaut Courtois (22), jambo ambalo kipa huyo aliyekaa Chelsea kwa muongo na zaidi hapendi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barcelona waangukia pua

Hodgson: Waingereza kachezeni nje