in , ,

Bado najiuliza kwanini KICHUYA kaamua kurudi SIMBA

Kichuya

Swali gumu sana kwenye akili yangu, akili yangu imeshindwa kung’anua jibu ambalo litakuwa jibu sahihi kwa sababu mpaka sasa hivi hapajaonekana usahihi wa Shiza Ramadhani Kichuya kurudi Simba.

Sehemu ambayo ilionekana kama sehemu ya yeye kupita kuelekea sehemu kubwa ya mafanikio kwenye mpira wake na mpira wa Taifa kwa ujumla. Sehemu ambayo ilionekana kama soko la yeye kumuuza huko ambako tunaamini ndiyo penye mpira.

Kutoka Simba kwenda nchini Misri tena kwenye ligi kuu ya Misri ulikuwa ushindi mkubwa sana kwenye miguu ya Shiza Ramadhani Kichuya. Ulikuwa ushindi ambao alitakiwa kuulinda kwa nguvu zote ili usipotee.

Ulikuwa ushindi ambao ulikuja na lugha moja tu kwake, aongeze bidii, aendelee kukimbia kwa kutazama mbele, shingo yake haikutakiwa kugeuka nyuma kwa sababu nyuma hakukuwa na faida tena kubwa kama mbele.

Mbele ndiko kulikuwa na mafanikio yake, mbele ndiyo kulikuwa na ukubwa wake kwenye mpira na mbele ndiko kulikuwa na tiketi yake ya yeye kwenda kucheza katika ligi barani ulaya.

Kufanikiwa kwake kucheza ligi kuu nchini Misri kulikuwa na nafasi kubwa sana kwake yeye kuuzika. Misri ndiyo sehemu ambayo mawakala ni wengi kuliko Tanzania.

Mawakala ambao kila uchwao hupishana kwenye viwanja vya ndege kutazama wachezaji ambao watakuwa bidhaa muhimu kwao wao kuziuza katika ligi ambazo ni bora kuzidi ligi ya Misri.

Misri ndiyo kulikuwa ni sehemu nzuri kwake yeye yenye mazingira bora na mazuri kwa kucheza kuliko hapa Tanzania. Kule kulikuwa na kila kitu ambacho mchezaji anatakiwa kuwa nacho ili kufikia hatua kubwa ya mafanikio.

Utake nini usipate kwenye ligi ya Misri? Viwanja bora vya mazoezi? GYM bora za kufanyia mazoezi? vifaa bora vya kufanyia mazoezi? makocha bora? wachezaji bora ambao watakupa wivu wa kupigana zaidi? Misri hata pesa ni nzuri kuliko hapa Tanzania.

Misri ni kanani ya mpira wa miguu ukilinganisha na hapa kwetu. Mazingira ya Misri yalikuwa mazingira sahihi kwake yeye kumfanya aone kuwa anatakiwa kukimbia mbele kuelekea kwenye mlima mafanikio.

Hakutakiwa tena kurudi Simba, tafasri ya yeye kurudi Simba ni yeye kuanza upya. Bahati mbaya anaenda kuanza upya sehemu ambayo kuna rundo la wachezaji ambao ni bora kuzidi yeye. Nafasi yake inakuwa finyu, mwisho wa siku tutaishia kumuona kwa mkopo Namungo FC.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Top 10 most-watched YouTube goals featuring Lionel Messi, David Beckham and other legends

Tanzania Sports

Ingenoga Morrison kucheza na Balinya na siyo Yikpe