Ligi kuu Tanzania Bara imepiga hatua katika raundi yanne mambo yanazidi kuwa moto siku zote tumekuwa tukiangalia takwimu leo tuna badilisha kidogo kisha chini tutafanya kama tulivyozoea.
Leo tutaangalia ukuta upi umefanya kazi sana kati ya timu hizi tatu Yanga, Simba na Azam FC ambazo zinaonekana kugombania ubingwa zikiwa na wachezaji wenye ubora wa hali ya juu.
Safu ya ulinzi ya Azam FC iko imara zaidi ya Yanga na Simba kwani Wanarambaramba hawajaruhusu nyavu yao kutikiswa kwa michezo yote minne.
Goli kipa namba moja wa Azam David Kisu ndiye anaye ongoza kwa ‘Clean Sheets’ akikusanya nne akifuatiwa na Metacha Mnata wa Yanga aliye nazo 3.
Yanga
Mabingwa mara 27 ligi kuu Tanzania Bara timu ya Yanga ‘Wananchi’ imechezea michezo minne ambapo imeruhusu goli moja katikaa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Tanzania Prisons, goli lilifungwa na Lambert Sabiyanka dakika ya 8 ya mchezo huo.
Yanga inaonekana kujiiamarisha zaidi upande wa ulinzi unaongozwa na Bakari Nondo Mwamnyeto, Lamine Moro, Kibwana Shomary pamoja na Mustapha Yassini.
Huku viungo wake wa ukabaji wanasaidia kutoruhusu washambuliaji wasipite kwa urahisi ni pamoja na Mukoko Tonombe, Feisal Salum na Zawadi Mauya.
Cha kushangaza zaidi timu hiyo imefunga magoli manne moja likifungwa upande wa washambuliaji, alikuwa Michael Sarpong dhidi ya Tanzania Prisons, lakini magoli matatu yamefungwa na idara ya ulinzi, Lamine Moro kafunga mawili, moja dhidi ya Mbeya City uwanja wa Mkapa na lingine amefunga dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Jamuhuri Morogoro.
Goli lingine lilifungwa na Mkongoman Mukoko Tunombe dhidi ya Kagera Sugar, magoli ya watu wa idara ya ulinzi yameipa Yanga alama 9 huku ile ya ushambuliaji wamepata alama moja.
TAKWIMU ZA YANGA
Katika magoli manne, moja limefungwa kipindi cha kwanza ambalo amefunga Michael Sarpong dakika ya 19 wakati yale matatu yamefungwa kipindi cha pili.
Kwa muonekano huo Yanga iko vizuri nyuma lakini katika safu ya ushambuliaji haijafikia malengo kwa michezo mine.
Huwezi kuilaumu sana kutokana na idara ya ushambuliaji haifikiwi na mipira bado kuna maswali mengi kwa kocha mkuu wa timu hiyo Zlatica Krmpotic.
Simba SC
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba nayo haikuwa nyuma katika kuvuka viunzi ili iutetee ubingwa wake kwani imeanza vizuri na haijapoteza mchezo wowote hadi sasa.
Mnyama Simba safu yake ya ulinzi imeruhusu magoli 2 ambayo wameyapata katika mechi ya Ihefu FC na Mtibwa Sugar.
Haina utofauti na wapinzani wake Yanga kwani nawao walianza kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ihefu FC magoli ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 10 na Mzamiru Yassin dakika ya 44 kipindi cha kwanza, lile la kusawazisha la Ihefu lilifungwa na Omary Mponda.
Mchezo wa pili mabeki wao wameruhusu dhidi ya Mtibwa Sugar goli la Simba alifunga Mzamiru Yassin kipindi cha kwanza lakini Mtibwa walijibu mapigo kipindi cha pili dakika za mwanzoni alifunga Bobani.
Hivyo michezo ya nje ya Dar es Salaam ambayo wameruhusu kufungwa magoli mawili.
Ile waliyocheza Dar es Salaam hwajaruhusu hata goli moja na wamepachika magoli 7.
Mchezo wa Biashara United wamefunga magoli 4 huku ule wa Gwambinanao wamepachika magoli matatu.
Simba inaonekana kuwa na safu bora ya ushambuliaji katika magoli 10 yaliyofunga ukitoa ya viungo Chama kafunga mawili na Mzamiru katia mbili manne hayo, lile moja kafunga Wawa matano wamefunga washambulijia, Bocco moja , Mugalu mawili na Kagere moja.
Azam FC
Azam FC haisemwi nayo imo, safu yake ni miongoni mwa safu bora katika raundi hii ya nne kwani haijaruhusu hata kuguswa nyavu zake.
Katika michezo mine imeshinda mchezo dhidi ya Polisi Tanzania goli 1-0 Obrey Chirwa, imeua dhidi ya Mbeya City 1-0 Allly Niyonzima, imeumiza dhidi ya Tanzania Prisons goli 1-0 Prince Dube na imeibutua coastal Union magoli 2-0 mfungaji akiwa Prince Dube yote kipindi cha pili.
Hivyo Azam FC imefunga magoli 5 katika michezo minne ikionekanaa kuwa mpinzani halisi wa Yanga na Simba.
MAGOLI YA VIPINDI
Azam FC imeshinda magoli 3 kipindi cha pili yote mfungaji akiwa Prince Dude wakati mawili yamefungwa kipindi cha kwanza wafungaji Obry Chirwa dhidi ya Tanzania Prisoni na Ally Niyonzima dakika ya 25 dhidi ya Mbeya City.
Yanga imepata magoli matatu kipindi cha pili, Lamine Moro kafunga mawili dhidi ya Mbeya City na Mtibwa wakati Mukoko amefunga dhidi ya Kagera Sugar lile moja limefunga na Sarpong dakika ya 19.
Simba imefunga magoli 6 kipindi cha kwanza na manne kipindi cha pili.
Wafungaji Mzamiru Yassin kafunga mawili kipindi cha kwanza huku Bocco na Chama nao wakichangia goli moja moja kiindi cha kwanza.
Mengine yamefungwa kipindi cha pili, Kagere, Chama, Mugalu katia kamba mbili na Wawa.
Kwa rekodi ya ujumla Yanga, Azam na Simba wamezalisha magoli 19, ikiwa 12 yamefungwa kipindi cha kwanza na magoli sita (6) yamepatikana kipindi cha pili hii kwa raundi zote nne.
TAKWIMU ZA RAUNDI YA NNE MECHI 8
Ikiwa tayari michezo nane imechezwa ligi kuu Tanzania bara ikisubiriwa mchezo mmoja ili uhitimishe raundi ya nne , nyavu zimeumizwa sana maana tayari magolki 53 yameingizwa.
Takwimu ya mwisho tulipata magoli 25 yalifungwa kipindi cha kwanza na 16 kipindi cha pili kwa mechi zote.
Lakini hii kwakuwa bado mechi moja kwa hizi nane zilizochezwa tunapata magoli 32 yaliyofungwa kipindi cha kwanza na 21 kipindi cha pili.
Rekodi inayongojwa ni ile ya magoli 14 ambapo raundi ya kwanza na ya tatu magoli yalishabihiana na ile ya pili yalipigwa matatu.
Kwa raundi ya nne mechi nane yamefunga magoli 12 tu ambayo matano kipindi cha kwanza na saba kipindi cha pili, je hiyo mechi moja iliyobaki ya tazidi au yataishia hapo?
Unaionaje ligi ya mwaka huu, je kombe linaenda kwa Injinia au litaenda kwa Mudi ama Bakharesa , yellow subai kombe litabaki hapa hapa wewe subiria.
Comments
Loading…