*Suluhu na Everton yawaacha njiapanda

Arsenal wamezuiwa kuchanja mbuga kujihakikishia kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimishwa suluhu na Everton.
Wakicheza nyumbani Emirates mbele ya washabiki 60,071, Washika Bunduki wa London walionesha udhaifu wa hapa na pale, lakini pia wakikosa nafasi murua baada ya kuwageuza uchochoro wapinzani wao.
Sare ya bila kufungana haiwasaidii sana wote wawili, kwani licha ya Arsenal kuwa nafasi ya tatu, wamecheza mechi nyingi zaidi ya wapinzani wao wakubwa Tottenham Hotspurs na Chelsea.
Ikiwa wapinzani wao hao watashinda mechi walizo nazo mkononi (Spurs moja na Chelsea mbili), basi Arsenal wataangukia nafasi ya tano.
Everton walianza vyema zaidi mechi ya Jumanne hii, lakini Steven Pienaar aliwakosesha bao, lakini mwenzake, kinda la miaka 19, Ross Barkley aling’ara vilivyo kwa Toffees.
Vijana hao wa David Moyes walikuwa na bahati ya kumaliza mechi wakiwa 11 uwanjani kutokana na walivyocheza rafu, ambapo Darron Gibson alicheza rafu mbili mbaya akimdhibiti Theo Walcott, ya kwanza akapata kadi ya njano, lakini ya pili mwamuzi Swabrick akala jiwe na kulalamikiwa na Arsenal.
Olivier Giroud alikosa nafasi kadhaa za kufunga, na kama kawaida yake alikuwa ama akijilaumu au akitazama eneo fulani kana kwamba ndilo limemkosesha.
Suluhu hii imehitimisha mfululizo wa ushindi wa vijana wa Arsene Wenger katika mechi tano, lakini ni mwendo wa kawaida kwa Everton.
Golikipa namba moja wa Arsenal, Wojsiech Szczesny alirejeshwa kundini na kucheza, na kwa ujumla alifanya vyema pamoja na mabeki wake.
Hata hivyo, nahodha Thomas Vermaelen alibaki benchi baada ya Per Metersacker kurejea kutoka kutumikia adhabu ya kukosa mechi moja kwa kadi nyekundu aliyopata walipocheza na West Bromwich Albion.
Mwelekeo zaidi wa nafasi nne za juu unajulikana Jumatano hii, Chelsea walio nafasi ya nne wanapokaribishwa kupepetana na Fulham na Jumapili Spurs watakapowakaribisha Manchester City wanaoshikilia nafasi ya pili.
Mechi nyingine Jumatano hii ni kati ya West Ham United wanaowakaribisha vinara wa ligi, Manchester United wakati Man City watakuwa wenyeji wa Wigan.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Di Canio akata ngebe

Manchester United wapepesuka