in , , , ,

Arsenal wawapopoa Liverpool


*Everton wavuka, kualikwa Emirates
*Man City na Wigan, Sunderland bado

Kocha Arsene Wenger amevuka moja ya vihunzi vigumu katika soka ya England, hasa baada ya kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kudai amebobea katika kushindwa.

Arsenal wamewafunga Liverpool 2-1 katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la FA, ikiwa ni siku chache baada ya Liverpool kuwabomoa The Gunners 5-1 katika Ligi Kuu ya England.

Ilikuwa furaha kwa maelfu ya washabiki wa Arsenal waliofurika Emirates jioni ya Jumapili wakiwa wameshikilia roho zao baada ya ushindi huo.

Alikuwa Alex Oxlade-Chamberlain aliyewaamsha vitini washabiki wa Arsenal dakika ya 16 kabla ya Oxlade-Chamberlain tena kumtengea Mjermani Lukas Podolski aliyewapa raha washabiki katika dakika ya 47 kwa bao zuri.

Hata hivyo, alikuwa Podolski ambaye hachezeshwi mara kwa mara na analalamikia hali hiyo, aliyesababisha penati dakika ya 58 kwa kumchezea rafu kwa nyuma nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, naye akafunga dhidi ya kipa namba mbili Lukasz Fabianski.

Kocha Arsene Wenger alichanganya wachezaji wa kikosi cha kwanza na wengine, akijua kwamba jumatano hii ana shughuli pevu dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja huo huo wa Emirates.

Zemanta Related Posts Thumbnail

Katika mechi nyingine, Everton waliwafunga Swansea 3-1 na kujihakikishia kuingia hatua ya robo fainali.

Huko, watakumbana na Arsenal katika dimba la Emirates na kocha wao Toffees, Roberto Martinez anasema hahofii safari hiyo.

Mabao ya Everton yalifungwa na Lacina Traore, Steven Naismith na Leighton Baines na kuwavusha katika hatua ya nane bora kwenye michuano hiyo.

Katika mechi nyingine Jumapili hii, Sheffield United waliwafunga Nottingham Forest kwa mabao 3-1.

Droo hiyo inaonesha kwamba kati ya Brighton na Hove Albion au Hull City watakabiliana na Sunderland wakati Sheffield United watacheza dhidi ya Sheffield Wednesday au Charlton Athletic na Manchester City watakuwa dhidi ya Wigan Athletic.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man City wawapiga Chelsea

  Vumbi Mabingwa 16 Ulaya