in , , ,

Arsenal wabanwa na Everton

*Fulham waona mwezi kwa Villa

Kasi ya Arsenal imepunguzwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates, baada ya kwenda sare ya 1-1 na Everton.
Katika mchezo mkali, Arsenal walitangulia kupata bao dakika 10 kabla ya kumalizika mchezo kupitia kwa Mesut Ozil lakini likasawazishwa dakika nne tu baadaye na Gerard Deulofeu (19) aliyeingia kipindi cha pili.

Sare hiyo imewanyima Arsenal kutanua uongozi kwenye kiti cha ligi kwa pointi sana, hivyo kubakiza pengo la pointi tano mbele ya Liverpool na Chelsea wenye pointi 30 kila moja.

Kipa wa Everton, Tim Howard alifanya kazi ya ziada kuzuia mabao ya Aaron Ramsey na Olivier Giroud lakini pia Wojciech Szczesny aliwaokoa Arsenal dhidi ya zahama kutoka kwa Kevin Mirallas. Giroud pia aligonga mtambaa wa panya dakika za majeruhi.

Everton wanabaki wakiwa wamefungwa mechi moja tu, dhidi ya Manchester City msimu huu na wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 28 wakiwa timu iliyoonesha ugumu sana kufungwa.

Katika mechi nyingine, Fulham mbele ya kocha wao mpya Rene Meulensteen walifanikiwa kusitisha vipigo vya mechi saba mfululizo walivyopata kwa kuwanyuka Aston Villa 2-0.

Mabao ya Fulham yalifungwa na Steve Sidwell na mkongwe Dimitar Berbatov kwa penati baada ya Leandro Bacuna kumchezea rafu Alex Kacaniklic.

Kwa matokeo ya mechi hizo mbili za Jumapili na nyingine za Jumamosi, Arsenal wanaongoza kwa pointi 35 wakifuatiwa na Liverpool na Chelsea wenye pointi 30 na nyuma yao ni Man City wenye 29 na Everton 28.

Tottenham Hotspur wanashika nafasi ya sita wakifuatiwa na Newcastle, Southampton na Manchester United wametulizwa katika nafasi ya tisa kwa pointi zao 22.

Villa ni wa 10 kwa pointi 19, Swansea wana 18 wakifuatiwa na Stoke, Hull na Norwich kila moja wakiwa na pointi 17.
West Bromwich Albion wameangukia nafasi ya 15 kwa pointi sawa na nafasi yao wakati Cardiff wana 14, West Ham 13 sawa na Fulham na Crystal Palace na mkoani wapo Sunderland wenye point inane.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man United gonjwa?

Matatani kwa kupanga matokeo England