in , , ,

Arsenal wabanwa lakini waongoza

*Spurs wagaragazwa na West Ham

Arsenal wameambulia pointi moja kwa West Bromwich Albion lakini imewasaidia kurejea kwenye uongozi wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ilikuwa mechi ngumu, ambapo Arsenal walitanglia kufungwa bao kupitia kwa Claudio Yacob aliyeunganisha majalo ya Morgan Amalfitano.
Arsenal wangeweza kuwa katika hali mbaya zaidi kama si kwa Mfaransa Nicolas Anelka kukosa nafasi mbili za wazi.

Hata hivyo, kiungo Mwingereza wa Arsenal, Jack Wilshere alifyatua kombora umbali wa yadi 20 na kuwapatia Arsenal bao.

Kocha wa West Brom, Steve Clarke alisema sare ni halali yao ambapo nusura Giroud apate bao la ushindi lakini kipa Boaz Myhill aliokoa hatari hiyo.

West Brom ndio walikuwa wametoka kuwafunga Manchester United katika mechi iliyopita. Wanakuwa pia timu ya kwanza kutwaa pointi moja kutoka kwa Arsenal, kwani Arsenal waliianza ligi kwa kufungwa na Aston Villa kabla ya kushinda mechi zote zilizofuata.

20131006-210701.jpg

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Tottenham Hotspur walikung’utwa mabao 3-0 na West Ham United kwa magoli yaliyofungwa na Winston Reid, Ricardo Vaz Ten a Ravez Morrison.

Yalikuwa mabao matatu yaliyowaacha Spurs wakiwa wamechoka bila kutarajia, ambapo wenzao wa London, Chelsea walifanikiwa katika dakika za mwisho kuwashinda Norwich kwa mabao 3-1.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Oscar, Eden Hazard na mchezaji mpya Willian wakati la kufutia machozi, japo lilifungwa kusawazisha lile la kwanza lilifungwa na Pilkington.

Southampton nao walizidi kuwazamisha Swansea kwa kuwafunga mabao 2-0.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wanashikilia usukani licha ya kufungana na Liverpool kwa pointi 16 walizo nazo, wakifuatiwa na Chelsea walio nyuma kwa pointi mbili sawa na Southampton.

Nafasi ya tano inashikwa na Manchester City na wanaofuata baada ya hapo ni Spurs, Everton, Hull, Manchester United, Aston Villa, Newcastle, West Brom, West Ham, Cardiff, Swansea, Stoke, Fulham, Norwich, Crystal Palace na Sunderland.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Liverpool wakoleza mapinduzi

Yanga waisogelea Simba