in , , ,

Arsenal tayari kwa mechi- Ngao ya Jamii

Kuna mechi kubwa ya soka Jumapili hii katika Uwanja wa Wembley, baina ya Mabingwa wa England, Manchester City na Mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal.

Wanawania Ngao ya Jamii, ambapo kwa kawaida mechi huchukuliwa kama ya kirafiki lakini yenye hadhi ya juu, kwani ndiyo inafungua pazia la msimu na baada ya hapo mechi za Ligi Kuu zinaanza.

Mitaani washabiki wa Arsenal wanasubiri kwa hamu kuona kikosi gani kitaanza mechi hii, ambayo inafanyika London ambako ni kwao tofauti na Manchester ambako ni mbali. Watakuwa na watu wengi wa kuwashangilia ndani na nje ya uwanja bila shaka.

Mechi hii si kiashirio sahihi cha jinsi vijana wa Arsene Wenger watakavyofanya msimu ujao, kwa sababu si wachezaji wote muhimu watakuwa uwanjani, na hilo ni kwa vikosi vyote viwili. Hata hivyo, wadau wa kila timu wangependa ya kwao ishinde.

Upo uwezekano wa kipa wa kawaida wa Arsenal, Wojciech Szczesny wakati kipa mpya kutoka Colombia,  David Ospina akizoea mazingira lakini pia anaelezwa kuwa na majeraha kidogo. Szczesny atafurahi kuwa golini na kuendeleza ‘utawala’ wake hapo.

Beki inadhaniwa kwamba itaongozwa na Laurent Koscielny pale kati na Kieran Gibbs kwa upande wa kushoto. Kwa kuwa Thomas Vermaelen anajiandaa kuondoka na beki mwingien wa kati, Per Mertesacker yupo mapumziko baada ya mechi za kuchosha za fainali za Kombe la Dunia, basi chipukizi Calum Chambers kutoka Southampton anaweza kuanza hapo kati.

Kwa beki ya kulia labda itakuwa fursa ya washabiki wa Arsenal kuona kifaa chao kipya kutoka Newcastle na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Mathieu Debuchy.

Kiungo huenda kikawa na Mikel Arteta ambaye ni nahodha msaidizi anayesemwa kwamba anaelekea kupewa unahodha kamili, lakini pia kuna Mathieu Flamini. Wote walipata mapumziko marefu wakati huu wa kiangazi na wanatakiwa wawe fiti.

Kiungo mwingine, Aaron Ramsey atakuwa vyema kuanza akiwa na Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kuonesha mambo adimu kwenye michuano ya Kombe la Emirates. Nyota wao katika usajili msimu huu, Alexis Sanchez kutoka Barcelona anasubiriwa kwa hamu kuendeleza yale aliyoonesha Brazil akiwa na Timu ya Taifa ya Chile.

Huyu anaweza kuendelea kucheza kama winga hadi Theo Walcott akamilishe matibabu yake warudi kuungana na kuonesha kile Walcott alichosema ni mashambulizi makali dhidi ya wapinzani wao.

Upo uwezekano wa chipukizi anayeanaz kuizoea Emirates,  Yaya Sanogo akaongoza mstari wa mashambulizi baada ya kufanikiwa kufunga mabao manne dhidi ya Benfica kwenye mechi za Emirates. Olivier Giroud alikuwa bado anajiandaa, hivyo kuna uwezekano asicheze au akaanzia benchi.
 
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barcelona watangaza manahodha wanne

Arsenal wawafyatua Manchester City