in , , ,

Arsenal nje Kombe la Ligi

*Chelsea, Man U wasonga mbele

Arsenal wametolewa katika Kombe la Ligi na Chelsea, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani kwao Emirates.
Arsenal walianza kulizwa dakika ya 25 kwa kosa la beki wao wa kulia, Carl Jenkinson aliyemrudishia mpira kwa kichwa kipa wake, Lukasz Fabiansk.

Jenkinson ambaye ni namba mbili wa Bacary Sagna, alirudisha mpira katika umbali ambao haukuwa sahihi, lakini pia wapinzani wao wakiwa karibu, ndipo Cesar Azpilicueta wa Chelsea alipoupata mpira na kumshinda nguvu kipa Fabianski na kuuweka kimiani.

Timu zote zilichanganya wachezaji wao, ambapo Chelsea walibadilisha wachezaji 10 waliocheza kwenye mechi iliyotangulia dhidi ya Manchester City, wakati Arsenal walibadilisha wachezaji wanane.

Hata hivyo, alikuwa Chelsea walioonekana kuwa wakomavu zaidi na pia wachezaji wake walishazoea mechi ngumu, na washabiki wao muda mwingi walikuwa wakiimba sifa za kocha wao, Jose Mourinho.

Juan Mata aliwapatia Chelsea bao la pili dakika ya 66 baada ya kupatiwa pasi na Willian, ikiwa ni muda mfupi baada ya Arsenal kumwingiza Mesut Ozil kisha wakamwingiza Olivier Giroud kujaribu kuvuka hatua hiyo.

Hii ni mara ya kwanza katika miaka 11 kwa Arsenal kushindwa kuvuka hatua hii ya Kombe la Ligi.

Arsenal wameingia mwaka wa nane bila kombe, na sasa wamebakiwa na matumaini kwenye Kombe la FA, Ligi Kuu na Kombe la Mabingwa Ulaya ambayo ndiyo wanaendelea kushiriki michezo yao.

Katika mechi nyingine, Manchester United wamefanikiwa kusonga mbele kwenye hatua inayofuata, baada ya kuwashinda Norwich 4-0.
United waliokuwa wakikabiliana na Norwich Old Trafford walipata bao kupitia kwa Javier Hernadez ‘Chicharito’ kwa penati mapema katika kipindi cha kwanza na la pili kwa njia ya kawaida dakika ya 54

Mabao mengine yalifungwa na Jones na Fabio dakika za 88 na 90. Mechi hiyo ilichezwa kwa nyongeza ya karibu dakika 10 kutokana na kuumia vibaya kichwani kwa Robert Snograss wa Norwich na kupata tiba uwanjani.

Na habari za sasa hivi ni kuwa timu ya Stoke City imewafunga Birmingham 4-2, kwa mikwaju ya penati, na hivyo kusonga mbele.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Platini ataka timu 40 Kombe la Dunia

Man City, Spurs zasonga mbele