in , , ,

Arsenal na Barca mtoano

Baada ya kufuzu kiaina katika hatua ya makundi, sasa Arsenal watacheza
na mabingwa watetezi wa Ulaya, Barcelona kwenye hatua ya mtoano ya
klabu 16.

Arsenal walianza vibaya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kwa kufungwa
mfululizo mechi mbili, wakaja kufufukia kwa Bayern Munich wakiwafunga
lakini wakaenda kuumia Allianz Arena kabla ya kuzishinda timu za
Dinamo Zagreb na Olympiakos na kufuzu.

Kushika kwao nafasi ya pili kulimaanisha kwamba wangepambwa na timu
kubwa Ulaya na walijua hilo, hivyo sasa watajiandaa kuwakabili
mabingwa hao wa Hispania wenye Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar
kati ya majina mengine makubwa.

Droo ya hatua hii ya pili inaonesha kwamba mabingwa watetezi wa
England, Chelsea wanaoonekana kulitema kombe tayari wanakabiliana na
Paris St-Germain (PSG) kwa msimu wa tatu mfululizo.

PSG ndio waliowatoa mwaka jana kwa tofauti ya bao la ugenini na mwaka
huu Chelsea wa Jose Mourinho wasipotwaa ubingwa huo, huenda msimu ujao
wakasikilizia tu hewani michuano husika, maana hata kocha wao anasema
si rahisi kumaliza Ligi Kuu ya England katika nafasi nne za juu.

Manchester City waliofanya vyema kwenye hatua ya makundi msimu huu
watakabiliana na Dynamo Kiev wakati Roma wapo dhidi ya Real Madrid.
Juventus waliofika fainali msimu uliopita wamepangwa na Bayern Munich.

Mechi za mkondo wa kwanza katika ratiba hii zitachezwa kati ya
Februari 16 – 17 na 23-24 mwakani wakati marudiano yatafanyika kati ya
Machi 8-9 na 15-16 mwakani. Chelsea na Man City wataanzia ugenini
wakati Arsenal wataanzia nyumbani Emirates.

Barcelona v Arsenal ni marudio ya fainali ya UCL ya 2006, ambapo
ilikuwa nusura Arsenal watwae ubingwa kama si Barca kupata mabao
mawili ya dakika za mwisho na kushinda kwa 2-1 na kipa wa Arsenal,
Jens Lehman akatolewa kwa kadi nyekundu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Chelsea ni kupigwa tu..

Tanzania Sports

Yanga inataka ubingwa bila usajili makini?