in , ,

Arsenal, Man U nguvu sawa

Arsenal wameshikilia nafasi yao ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya kutoka sare ya 1-1 na Manchester United.
Sare hiyo imewaacha United wakiwa nafasi ya nne, ambapo bao lao lilifungwa na Andre Herrera wakati la Arsenal lilisababishwa na majalo ya Theo Walcott iliyomparaza Blackett.

Ilikuwa mechi ambayo kipa namba moja wa United, David de Gea alilazimika kuondoka uwanjani baada ya kuumia na kwa mara ya kwanza Victor Valdes kuchukua nafasi yake katika EPL.

Arsenal watajihakikishia nafasi ya tatu iwapo watawafunga Sunderland Jumatano hii. Timu zote mbili zimejihakikishia nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) japokuwa kinachogombewa ni nafasi ya pili, tatu na ya nne.

Tayari Chelsea wametwaa ubingwa, hivyo nafasi tatu zinazofuata zinawaniwa na Manchester City, Arsenal na Man United.

Katika mechi nyingine, Man City wamewafunga Swansea 4-2 katika mechi iliyoshuhudia mchezaji wa zamani wa Swansea, Wilfried Bony akifunga bao la mwisho na kuwaadhibu klabu yake ya zamani.

Mabingwa hawa waliovuliwa taji na Chelsea majuzi walicheza vyema, ambapo mabao yao mengine yalifungwa na Yaya Toure mawili na jingine James Milner, wote wakitarajiwa kuondoka klabuni hapo msimu huu.

Swansea walipata mabao yao kupitia kwa Gylfi Sigurdsson na Bafetimbi Gomis, wakiweka rehani matumaini ya kupata kucheza Ligi ya Europa kwani sasa wanashika nafasi ya nane wakiwa na pointi 56.

Chelsea ambao ni mabingwa wanaongoza ligi wakiwa na pointi 84 wakifuatiwa na Man City wenye pointi 76, Arsenal wanazo 71 lakini wana mchezo mmoja mkononi kama walivyo Sunderland.

Nafasi ya nne wanashika United wakiwa na pointi 69, wa tano ni Liverpool wenye pointi 62 wakifuatiwa na Southampton wenye pointi 60.
Mkiani bado wapo QPR wenye pointi 30 sawa na Burnley huku Hull wakiwa nazo 36 na Sunderland waliojikusanyia pointi 37.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Hali tete Ligi Kuu England

Barcelona mabingwa La Liga