in , , ,

Yanga walivyoendeleza ubabe kwa Simba

HABARI kwenye mitaa mingi nchini Tanzania kwa sasa ni juu ya matokeo ya Dabi ya Dar es Salaam, ambapo Yanga waliwafunga Simba kwa mara ya sita mfululizo.

Ilikuwa ni mechi ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania, ambapo Yanga wametwaa Ngao ya Jamii na kuweka rekodi nyingine iliyowaacha wanachama na washabiki wake wakiwa furahani.

Washabiki wa Simba walikuwa wameikamia mechi, wengi wao wakisema mitaani na kwenye ofisi mbalimbali kwamba sasa unyonge basi.

Na kweli mechi ilianza kwa wachezaji wa Simba wakionesha ukuu zaidi, wakipeana pasi uzuri na kulishambulia vilivyo lango la Yanga, laiti kama si jitihada za golikipa wao namba moja, Djigui Diarra, Simba wangeweza kuibuka na ushindi.

Tanzania Sports
Kikosi cha SIMBA SC

Kocha Fadlu Davis ambaye amefanya vyema tangu ajiunge na Wekundu wa Msimbazi, alikuwa akisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya mahasimu hao wa Jangwani, lakini haikuwa Bahati yake.

Bao pekee lililowazamisha Simba lilikuwa la Pacome Zouzoua, alilofunga katika dakika ya 54, ikionekana kama vile sababu kubwa ilikuwa kwa golikipa wa Simba, Moussa Camara, kutokufanya jitiuhada za awali za kuokoa mpira uliokuwa ukiambaa ambaa, akiwa awali ameutema.

Washabiki wa Simba wamekuwa wakisema vijiweni na kwenye mitandao kwamba hawakutendewa haki na mwamuazi

Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam lilifurika mashabiki kushuhudia mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ikiwa na mvuto wa kipekee kutokana na historia, ushindani na rekodi za timu hizo kubwa mbili.

Ngao ya Jamii imekuwa ni sehemu ya ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001. Awali, mfumo wa mashindano ulihusisha bingwa wa ligi dhidi ya mshindi wa Kombe la FA.

Miaka ya karibuni, mashindano haya yalihusisha timu nne, lakini msimu huu TFF imepunguza idadi ya washiriki kutokana na ratiba ngumu ya kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa takwimu, Simba wamechukua Ngao ya Jamii mara 10, ikiwemo ushindi wa kwanza mwaka 2002 dhidi ya Yanga kwa mabao 4-1. Ushindi wao wa karibuni ulikuwa mwaka 2023 walipowafunga Yanga kwa penalti 3-1 baada ya sare tasa.

Kwa upande mwingine, Yanga wameshinda Ngao ya Jamii mara 8, wakianzia na ushindi wao wa kwanza mwaka 2001 walipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba. Ushindi wao wa karibuni ulikuwa mwaka 2024 walipoifunga Azam mabao 4-1.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Nani kucheka, nani kununa Simba au Yanga

Tanzania Sports

Sababu za Man United kuwa dhaifu