in

Yanga, Simba ‘Kusuguana’ Mara Ya Nne

Kikosi cha Simba Sports Club

Wakati vuguvugu la mchezo wa nusu fainali baina ya Yanga na Simba utakaopigwa Julai 12 uwanja wa taifa Dar es Salaam, timu hizo zitakutana mara 4 kwa mwaka huu.

Wakati unaendelea kufikiria itakuwaje ngoja  ‘ nikusanulie’ yaani nitoe ufafanuzi, hayo maneno huwa yanatumika katika kukuza Kiswahili wnaita misimu.

Tayari msimu huu timu hizo zimekutana mara 2 katika mechi za ligi mchezo wa awali ulipigwa mwezi Januari wakati ule wa pili ulipigwa Machi 8 zote zilipigwa uwanja wataifa Dar es Salaam.

Matokeo katika mechi hizo ule uliopigwa Januari ambapo mwenyeji alikuwa Simba matokeo yalikuwa 2-2, Simba ilianza kushinda kwa magoli ya Deo Kanda na Meddie Kagere wakati Yanga ilijibu kipindi cha pili magoli ya Mohamed Banka na Balama Mapinduzi.

Katika mchezo wa pili ambao ulifanyika taifa pia Yanga ilishinda goli 1-0 goli lililofungwa na Benard Morrison.

Mchezo wa tatu utafanyika Julai 12 katika nusu fainali ya kombe la ‘Azam Sports Federation Cup’.

Wakati huo mchezo wa nne hapa tupige mahesabu wote, tena tunaongeza na mchezo wa tano kama ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likipanga mechi moja ya ligi mwaka huu.

Tuanzie hapa, endapo Yanga ikishinda kombe la ASFC mchezo wa kufungua ligi utachezwa kati ya Yanga na Simba.

Endapo Simba ikishinda kombe la ASFC huku Yanga ikishika nafasi ya pili basi mchezo wa kufungua ligi utazikutanisha Yanga na Simba.

Naomba nitoe darasa hapa zamani kidogo tulisoma hesabu zinazoitwa ‘Probability’maana ligi haijaisha hivyo tumepiga mahesabu ya juu na mbali zaidi.

Ieleweke Azam FC inayo nafasi ya kushika nafasi ya pili pia wakati huo Namungo anaweza kufika nafasi ya pili ila ukiangalia kwa mbali unaweza kuona namna mambo yanavyoenda.

Turejee katika ligi kama TFF watapanga ratiba yao  vizuri timu hizo zinaweza kukutana mwaka huu katika ligi kuu ya Tanzania Bara mkondo wa kwanza.

Kama zitakutana hatua hiyo basi zitakamilisha awamu tano kwa mwaka huu wa 2020.

Mchezo wa Simba na Yanga unakuwa na radha yake hapa Tanzania kutokana na ukubwa na ubora wa timu hizo.

Huwa unateka hisia za watu wengi hapa Afrika Mashariki kutokana na ukubwa wa mechi yenyewe.

Simba inatakiwa ije kivingine isidharau Yanga kwa kinachoendelea ndani ya timu hiyo.

Yanga wanatakiwa wasikate tamaa na kujua kuwa wanaweza kurudia kile walichokianya Machi 8 mwaka huu.

Angalizo ubora wa kikosi katika mechi za Yanga na Simba huwa hauna maana yoyote ila tu chakuelewa mchezo wao hautabiriki.

Mifano iko mingi, mchezo ambao Yanga na Simba uliofanyika msimu uliopita wengi hawakuamini kama zitatoa sare pia hata huu wa mwaka huu wengi hawakuamini kama Yanga ingeshinda.

Mtanange wa Simba na Yanga

Kuna msimu Simba ilikuwa mbovu sana Yanga ilitangulia mabao matatu lakini kipindi cha pili Mnyama alibadili matokeo na kuwa 3-3.

Hao ndio mafahari wawili wa Tanzania Simba na Yanga ambazo zina utamaduni wake tofuati na mechi nyingine.

Ukitaka kujua kuwa hawa watu wanafanana, mgogoro ukianza Yanga ukiisha tu wanaupokea Simba na unaendelea ukisha huko unarejea Yanga.

Hizi ndio pacha mbili zilizokuwa na uadui wa ndani ya uwanja uadui usiokuwa wa kupigana bali kuoneshana mpira maarufu kama  ‘mbungi’ baadae wanataniana ila katika shughuli mbalimbali wanakutana na wanashirikiana.

Yanga imeanzishwa mwaka 1935 wakati Simba imeibuka mwaka 1936 zote zinatoka Kariakoo.

Moja iko katikati ya Kariakoo nyingine ipo pembezoni mwa Kariakoo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga na Simba Uwanjani

Waamuzi wetu hawatamani kuchezesha Afcon?

Morrison ni mkubwa kuzidi Yanga

Morrison ni mkubwa kuzidi Yanga !