in , , ,

Yanga bila Djigui Diara itakuwaje?

GOLIKIPA wa Yanga alipangwa katika mchezo wa ‘Kariakoo Derby’ saa chache baada ya kuwakilisha Timu yake ya Taifa ya Mali. Katika mchezo huo Djigui Diara alikuwa mhimili katika kikosi hicho ambacho kiliibuka na ushindi wa bao moja kwa nunge. Katika mchezo huo Yanga walikuwa na kila sababu ya kushukuru umahiri wa Diarra ambaye aliwanyima bao la wazi Simba. Hata hivyo ipo namna ambayo tunaweza kuchambua juu ya mwenendo wa mlindamlango huo maarufu na mwenye maarifa makubwa kiufundi.

Je uimara wa Djigui Diara upo wapi?

Kila mchezo huwa na uimara wake unaowavutia makocha. Djigui Diarra ni miongoni mwa makipa ambao wanavutia kiuchezaji. Uwezo wake mkubwa ni kupangua mashuti ya ana kwa ana. Pia ni kipa mzuri katika kupangua krosi na kuondosha hatari langoni mwake. Uimara wa kipa huyo unawapa imani na kujiamini mashabiki na makocha wake na hivyo kuwa chanzo cha kutamba kwa Yanga. 

Sifa yake; Uwezo wa kutumia miguu

Sifa kubwa ya golikipa wa kisasa ni uwezo wa kutumia miguu yake katika kushiriki uchezaji wa timu. Kama tulivyosema katika makala zilizopita makipa wanalazimishwa kuendana na mabadiliko kwa kushiriki mchezo kwa muda mwingi wa dakika tisini kuliko kupangua mashuti pekee. 

Kipa huyu amekuwa mhimili wa Yanga kwa misimu kadhaa sasa kutokana na uimara wake. Uwezo wake wa kumiliki mpira ni mkubwa kama ulivyo ule wa ukipa. Ni kati ya silaha ambazo zipo golini mwa Yanga. Uwezo wa kukokota mpira, kumiliki, kugawa au kusambaza mpira ni mojawapo ya mambo muhimu yanayomtofautisha na makipa wengine. Katika eneo hili ushindani pekee aliokuwa akiupata ni kutoka kwa Aishi Manula kabla ya ujio wa Mousa Camara waliopo Simba.

Je udhaifu wa Diarra ni upi?

Kama walivyo makipa wengine, Diarra sio mahiri katika eneo la upanguaji penati. Unaweza kutumia pambano dhidi ya Mamelodi Sundowns kama mfano mojawapo wa udhaifu wake katika eneo la kuokoa penati wakati wa piga nikupige au hatua ya mattua. Ingawaje amefanya hivyo mara kadhaa lakini hajawa mahiri katika kupangua penati. 

Hali kadhalika mashuti ya nje ya 18 ni miongoni mwa mambo yanayoonesha alivyo dhaifu. Kwenye mashindano ya AFCON kulikuwa na kasoro hizo na mara kadhaa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho au Ligi ya Mabingwa amekuwa katika wakati mgumu. Mashuti anayopigiwa nje ya 18 hajamudu bado. Kwamba hajaonesha ule umahiri wa kurukia michomo hiyo ya angani inayopigwa kuelekea langoni mwake kama wasemavyo mashabiki wenyewe ‘nyuzi tisini’ yaani mashuti makali yanayoingia kwneye kona za juu za lango. 

Je ubora wake ni upo eneo gani?

Sifa kubw aya kipa huyu ni uwezo wa kuzungumza na mabeki wake. Anazungumza kuhusu kujipanga, mbinu na uwezo wa kukabiliana na washambuliaji hatari. Ni kipa ambaye anaweza kucheza mabeki wowote kwani umahiri wake unawasaidia kujiamini zaidi. Sifa nyingine ni uwezo wa kuanzisha mashambulizi. Nipa ambaye anaweza kupiga mipira mirefu kuelekea langoni mwa  adui na kuwapa changamoto timu pinzani. Upigaji wa mipira mirefu kutoka kwa makipa imekuwa maarufu sana, Djigui Diarra ni miongoni mwa hazina hizo ambazo zinang’arisha Ligi Kuu Tanzania.

Itakuwaje Yanga bila Diarra siku akiumia?

Mojawapo ya maswali magumu ni hili; siku Djigui Diarra akiumia huku mashindano yakiendelea itakuwaje? Lango la Yanga litakuwa katika umahiri uleule? Kwamba Yanga wamekuwa wakimtegemea mno kipa huyu kiasi kwamba makipa wengine hawapati nafasi ya kunoa umahiri  wao katika mechi. Abdutwalibu Msheri ni kipa mzuri na anajifunza chini ya timu nzuri na mshindani wake ni bora. 

Hata hivyo swali kubwa ni hilo hapo juu siku Diarra akiumia Yanga watakuwa katika umahiri uleule langoni? Ni wakati wa kuangalia sasa namna ya kuwaimarisha makipa wengine waliopo Yanga. Ni muhimu kuwapatia mechi kadhaa kuinua viwango vyao vya ubora vilivyochangia wao kusajiliwa Yanga. Maana tumeozea mwisho w amsimu wachezaji wanatemwa wakati hata mechi hawakuwa wakipewa kuimarisha viwnago vyao. Kila mara wanalaumiwa kushuka viwango au kukosa ari ya kushindana wakati hawakuwa na mechi za kucheza. 

Je Diarra anafundisha nini makipa wa Tanzania?

Zama zimebadilika. Makipa wanatakiwa kubadilika pia. Kwahiyo aina ya makipa kama Metacha Mnata inakwenda kubadilika hivyo lazima wajifunze matumizi ya miguu kwa ufasaha. Nakumbuka golikipa wa Real Madrid Thibaut Courtois alikuwa na changamoto ya matumizi ya miguu, kwahiyo benchi la ufundi likaanza mkakati rasmi wa kumwezesha anakuwa na kiwango kizuri katika matumizi ya miguu. 

Kwahiyo hata makipa wazawa wanaweza kubadilika ikiwa klabu zitatumia muda wao kuwaandaa. Nafasi ya makipa inabadilika sana na ndiyo walinzi namba tano katika mifumo ya kisasa. Yanga wanaposhambulia tazama Diarra anakuwa  eneo gani. Mara nyingi anakuwa katika eneo la namba tano ambalo linasaidia kuongeza idadi ya wachezaji kuelekea kiungo cha ukabaji na kuipa timu uwiano mzuri.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

14 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga wanashuka au Simba wanapanda?

Tanzania Sports

Tunataka Kuwa Wasindikizaji Olympiki Kila Mwaka?