in , , ,

Wigan mabingwa FA

*Wawatibulia Manchester City

Gwaride lililokuwa limepangwa kulipamba jiji la Manchester limeota mbawa, baada ya Wigan Athletic kuwaadabisha Manchester City na kutwaa kombe la FA katika fainali dimbani Wembley.
Ilikuwa fainali ya ‘Roberto M’ wawili – Martinez wa Wigan na Mancini wa City, ambapo Mancini alikuwa na shauku ya kombe ili walau kupoza machungu ya kupoteza lile la ubingwa wa England, na kadiri mchezo ukiendelea alihisi kuna bao.
Hata hivyo, kadiri mechi ilivyosonga mbele, Wigan walianza kujijengea ndoto ya kutwaa kombe mara ya kwanza katika miaka 81 ya historia yao, wakiongozwa jukwaa kuu na mmiliki na mwenyekiti, Dave Whelan.
Wachezaji wa City, Kolo Toure, Carlos Tevez, Sergio Aguero, James Milner, David Silva, Jack Rodwell na wengine walicheza vyema kusukuma mipira karibu na goli, lakini hawakufanikiwa kufunga.
Wigan walio katika hatari ya kushuka daraja, waliendelea kucheza kwa kujiamini, na kutolewa kwa kadi nyekundu kwa Pablo Zabaleta wa City kwa rafu dakika za mwisho mwisho, ilikuwa kama chachu kwa Wigan.
Wagumu hao walifanikiwa kulenga shabaha golini mara moja, nalo likawa bao, lililowekwa kimiani na Ben Watson katika dakika ya 90 akiunganisha golini kona akiwa mbele ya wachezaji wa City, huku kipa Joe Hart akishindwa kuchupa kuukamata.
Muuaji wa City aliingia kipindi cha pili, na alikosa mechi nyingi msimu huu baada ya kuvunjika mguu Novemba. Aliwaacha washabiki wa Wigan wakiwa hawaamini, wakashangilia kupita kiasi, na kuona safari yao ya treni ambayo wengine walifunga tangu jana imelipa na hata wakishuka daraja, wameweka historia.
Kichapo hicho kimemwacha Mancini katika fadhaa, kwa sababu Jumamosi ilimwanzia vibaya kwa magazeti kudai kwamba atafukuzwa kazi mwisho wa msimu hata kama angetwaa kombe hilo. Aliwapatia City ubingwa wa England mwaka jana, ikiwa ni mara ya kwanza katika aidi ya miaka 40 ya historia ya klabu hiyo.
Kwa kushindwa kutwaa kombe, ratiba za gwaride na ushangiliaji zilizotarajiwa kuvuruga jiji la Manchester, hasa ikizingatiwa kwamba Manchester United nao watakuwa na sherehe zao za ubingwa wa England wiki ijayo. Halmashauri ya Jiji la Manchester ilikuwa ikijaribu kuepusha mwingiliano huo, lakini sasa wamepunguziwa kazi.
Wigan wanakuwa klabu ya 43 kutwaa Kombe la FA na Martinez Mhispaniola wa pili kulitwaa. Hakuna klabu ya ligi kuu iliyowahi kutwaa kombe hilo kisha ikashuka daraja, labda historia itawekwa msimu huu kama Wigan hawatafanya vyema mechi mbili zilizobaki na kuomba walio chini yao wafanye vibaya.
Matokeo hayo yanakuja wakati Martinez akipigiwa chapuo la kuirithi mikoba ya David Moyes anayeondoka Everton na kujiunga Manchester United kuchukua nafasi ya Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa msimu.

 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea wahitaji pointi moja

Fergie aagwa, Newcastle, Norwich zaokoka