Kwa mara ya kwanza Mataifa ya Afrika Mashariki yanagonga vichwa vya vyombo vya habari barani Afrika kutokana na ushiriki wao kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani. TANZANIASPORTS inachambuya mbivu na mbichi kwa timu wenyeji wa fainali za CHAN ambazo ni Kenya, Tanzania na Uganda. Mataifa hayo yamepiga hatua kubwa kwenye mashindano hayo kiasi kwamba yanafikiriwa kutamani kulibakiza Kombe nyumbani.
KENYA
Jina la utani la timu ya Taifa ya Kenya ni Harambee Stars. Nchi hii katika ngazi ya klabu timu zake hazijafua dafu kwenye mashindano ya CAF hasa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa miaka ya karibuni. Vilabu vya Kenya havijaweka majina yao kwenye ramani ya kandanda kwa miaka karibia 10 hivi sasa ambapo wanahsuhuydia majirani zao wa Vipers kutoka Uganda pamoja na miamba ya Tanzania Simba na Yangaz ikichachafya vigogo wa soka.
Katika ngazi ya soka la Kimataifa, Kenya inaonekana kuwa miongoni mwa timu nzuri zinazofanya vizuri kwenye mashindano ya CAF. Kenya ni wenyeji wenza wa CHAN, wachezaji wake wameahidiwa kupewa mamilioni ya shilingi kila mchezo wanaoshinda na endapo watanyakua kombe hilo basi watakuwa na zawadi nono zaidi. Rais wa Kenya, William Ruto ni silaha muhimu ya ari na mafanikio ya Kenya kutinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la CHAN.
Kwenye hatua ya robo fainali Kenya watachuana na Madagascar ambayo ilikuwa kundi moja na Tanzania ikitumia uwanja wa Benjamin Mkapa. Kocha Ben McCarthy ameonesha namna alivyokiandaa kikosi chake katika amzingira ya aina yoyote ili kuleta matokeo mazuri. Chini ya kocha huyo Kenya imeimarika na kuwa hatari kwenye mashindano haya na kuibua matumaini ya kulibakiza kombe hilo katika ardhi ya Afrika Mashariki. Je watawezana na hili? Ni jambo la kusubiri na kuona.
TANZANIA
Taifa Stars ndilo jina linalotamba. Tayari wachezaji wake walishanyakua tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kuanzia Feisal Salum na Mudathir Yahya. Taifa Stars ilianza kwa ushindi mnono katika mchezo wa kwanza, kisha ikakumbana na kibarua kigumu mbele ya Mauritania kabla ya kupepetana na Madagascar ambapo kwenye mechi zote walipata ushindi.
Taifa Stars imemaliza kundi ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda michezo mitatu na kutoa suluhu mmoja dhidi ya Afrika ya Kati. Katika mashindano ya CAF ngazi ya klabu, Tanzania inazo sifa nyingi ambazo zinavutia wachezaji mbalimbali kuja kucheza Ligi Kuu Tanzania. Yanga na Simba zimekuwa jukwaa ambalo linatikisa vigogo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Simba na Yanga zote zimewahi kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho na imekuwa na wachezaji wenye viwango na ambao wanalisaidia Taifa kwa sasa. kutokana na kuwa mwenyeji Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa shilingi Bilioni moja kwa Taifa Stars endapo itashinda kombe la CHAN. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa Stars kushinda mechi tatu mfululizo katika mashindano ya CAF na mara ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CHAN.
Hili limeibua ari kwa wachezaji nan a benchi la ufundi kuhakikisha wanalibakiza kombe CHAN nchini. Wakicheza katika dimba la nyumbani la Benjamin Mkapa siku chache zijazo, Taifa Stars watawakaribisha Morocco ambao walimaliza nafasi ya pili katika kituo cha Nairobi nchini Kenya. Je Taifa Stars wataweza kulibakiza kombe la CHAN nyumbani? Ni suala la kusubiri na kuona.
UGANDA
Kw ajina la utani wanaitwa Uganda Cranes, ni nchi ambayo mewtaoa nyota kadhaa waliotikisa Ligi Kuu Tanzania. Vipers ndiyo klabu iliyojitutumia miaka ya karibuni, lakini kwa ngazi ya klabu hakuna mafanikio makubwa kwenye mashindano ya CAF. Katika mashindano ya CHAN, Uganda inakuwa mwenyeji wa tatu baada ya Tanzania na Kenya. Kwa ushirikiano huu Uganda nalo lilikuwa taifa ambalo likifikiriwa kulibakiza kombe la CHAN katika ardhi ya Afrika mashariki. Hii ni nchi ambayo inaoongozwa na kinara wao Allan Okello ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi nzuri za kuipa mafanikio nchi hii. Je nao wataweza kulibakiza kombe hili nyumbani? Ni suala la kusubiri na kuona.

