in , , , ,

Wenger: UCL ni kufa na kupona

* Per Mertesacker aitwa kwa dharura

 
Arsenal lazima wawafunge Besiktas kwenye mechi mbili za mtoano ili wafuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kwa gharama yoyote ile, amesema kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger.

Arsenal wamekwenda Uturuki kupambana na washindi wa pili wa ligi ya nchi hiyo wa msimu uliopita Jumanne hii, ambapoThe Gunners wakitafuta kufuzu kwa msimu wa sita mfululizo na mechi ya marudiano itafanyika Emirates Agosti 27.
“Lazima tuwashinde Besiktas kwa gharama yoyote kwa sababu tunataka kuvuka na kucheza kwenye hatua ya makundi. Tunajua jinsi michuano hii ilivyo mikubwa,” amesema Wenger.

Mfaransa huyoa meamua kumuita kwa dharura Nahodha Msaidizi, Per Mertesacker, ambaye pamoja na Mesut Ozil na Lukas Podolski wapo mapumziko baada ya kuwa na timu yao ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa Kombe la Dunia nchini Brazil.

Hatua hiyo ya Wenger inatokana na beki wa kulia, Kieran Gibbs kuwa na majeraha huku mlinzi wa kati, Laurent Koscielny naye akiwa hana uhakika wa kucheza kutokana na mguu kuwa na matatizo kidogo.

Koscielny ndiye amekuwa akicheza na Mertesacker msimu uliopita kama chaguo la kwanza kwenye beki ya kati, nahodha Thomas Vermaelen aliyeuzwa Barcelona majuzi akiwa kiraka pale mmoja wao anapokosekana.

Mertesacker amecheza jumla ya mechi 62 kwa Arsenal na Ujerumani msimu uliopita, na alitakiwa kupumzika wiki moja zaidi, lakini yupo tayari kuinusuru klabu yake, hivyo anasafiri na wenzake ili kuziba pengo likitokea, au hata kuanza kabisa.

Beki ya kati kwenye mechi chache zilizopita imeundwa na Koscielny na Calum Chambers (19) aliyetoka Southampton kiangazi hiki, lakini pia kuna Nacho Monreal aliyecheza kwenye mechi ya Ngao ya Jamii walipowafunga Manchester City 3-0.

“Mpango wetu ulikuwa kuwarejesha Wajerumani baadaye kwa ajili ya kuwakabili Everton Jumamosi, lakini kwa dharura nitamchukua Mertesacker. Ni mapema kidogo kwake maana walihitaji wiki moja zaidi, lakini kwa vile yupo tayari kucheza, hakuna tatizo,” anasema Wenger.
 
Arsenal walioanza ligi kwa kuwafunga  Crystal Palace 2-1 kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu, wamekwenda Istanbul na watakabiliana na vijana wa kocha Slaven Bilic kwenye Uwanja wa Ataturk Olympic, kwani ule wa Besiktas wa Vodafone Arena unakarabatiwa.

Besiktas wamefika hatua hii ya mtoano baada ya kuwafunga Feyenoord ya Uholanzi kwa mabao 5-2 kwenye mechi mbili walizocheza, ambapo ile ya mkondo wa pili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba alifunga mabao matatu.

Arsenal wanaanza kwenye hatua ya mtoano kwa sababu walimaliza katika nafasi ya nne ligi kuu ya England, nyuma ya Man City, Liverpool na Chelsea waliofuzu moja kwa moja. Msimu uliopita Arsenal waliwapiga klabu nyingine ya Uturuki, Fenerbahce kwenye uwanja huu huu wanaocheza Jumanne hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Mabingwa waanza na ushindi

Chelsea wawashinda Burnley