Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck atakuwa nje ya dimba kwa miezi kadhaa, baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England aliumia mwishoni mwa Aprili na amekuwa akiendelea kupata matibabu lakini hapakuonekana maendeleo mazuri, kiasi cha uamuzi kufanyika kwamba apasuliwe goti hilo.

Arsenal wamesema katika taarifa yao kwamba uamuzi wa kupasuliwa kwake ulifanyika wiki iliyopita, baada ya matabibu kuona kwamba hakuwa akiendelea kwa kasi nzuri ya kupona ili kuanza mazoezi mepesi. Kipindi chote cha kiangazi alikuwa katika programu ya matibabu akitarajia angekuwa fiti kwenye mechi kadhaa za awali za ligi kuu lakini ikashindikana.

Ilishadhaniwa kwamba hapangekuwa na haja ya upasuaji, kutokana na maendeleo mazuri ya awali na jinsi alivyokuwa, siku hadi siku, akiongeza muda na kasi ya maoezi lakini mtaalamu aliyebobea kwenye eneo hilo akashauri kwamba hawezi kuepuka kisu.

Welbeck alitarajiwa angepona ili achangie nguvu zake katika ushambuliaji pamoja na akina Olivier Giroud, Alexis Sanchez, Theo Walcott na wengine, lakini sasa itabidi asikilizie matokeo nje ya uwanja.

Welbeck, 24, ni mshambuliji wa kati anayeweza pia kucheza pembeni na alianzia maisha ya soka katika akademia ya Manchester United 2001 kabla ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa 2008 chini ya Sir Alex Ferguson, akiwa mmoja wa wachezaji kwa klabu hiyo wachache waliozaliwa Manchester.

Kuanzia msimu wa 2011/12, Welbeck alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha United, lakini baada ya kuingia kwa kocha Louis van Gaal, alimuuza kwa Arsenal kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 16 siku ya mwisho wa dirisha la usajili Septemba mwaka jana.

Pamoja na mambo mengine, Van Gaal alidai kwamba Welbeck hakuonesha ubora katika kufunga mabao kwa kuwianisha mechi alizocheza, akilinganishwa na akina Wayne Rooney na Robin Van Persie. Kiangazi hiki Van Persie naye ameuzwa Uturuki kwa sababu kama hizo.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Argentina wababe wa soka

Tanzania Sports

KUFUZU EURO 2016: