Menu
in , ,

Wasimamizi wa Ligi Kuu wasirudie makosa

Tanzania Sports

LICHA ya kwamba pazia la Ligi Kuu Tanzania limefungwa na shughuli iliyobaki ni usajili na vilabu kujiimarisha kiuongozi, uwekezaji na rasilimali watu lakini bado yapo ambayo yanatakiwa kujadiliwa ili kurekebisha makosa yaliyotokea katika msimu uliomalizika. TANZANIASPORTS inaangazia masuala muhimu ambayo yalisababisha 

Ligi Kuu kuwa na makosa ambayo yalichochea mjadala hasi ambao ulikuwa unatweza majukumu ya wasimamizi na waendeshaji wa Ligi Kuu pamoja na wadhamini wao. Kwa madhumuni ya kujenga jamii bora ya kimichezo, ni muhimu kutambua makosa yaliyopita kama nyenzo ya kuimarisha Ligi Kuu msimu ujao.

Makosa ya waamuzi

Kelele nyingi zilipigwa msimu uliomalizika. Mashabiki wlaikuwa wakilalamikia makosa ya wazi ya waamuzi wa Ligi Kuu na kudai kuwa kulikuwa na upendeleo kwa vilabu fulani. Ukiondoa Ahmed Aragija waamuzi wengi wa Ligi kuu wanatupiwa lawama kusababisha timu zetu kubebwa na kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za soka. Makosa ya waamuzi hao yalikuwa kwenye sheria za adhabu ndogo, adhabu kubwa (pigo kubwa la penati), kuotea na matukio mbalimbali michezoni. 

Waamuzi walitupiwa lawama hizo kwa njia ya kuwakumbusha kubadilika juu ya uamuzi wanaochukua wanapokuwa katikati ya dimba. Ifahamike kuwa ubora wa Ligi Kuu utaongezeka na kutengeneza thamani kubwa ikiwa waamuzi watakuwa wanatoa uamuzi wa haki na kutafsiri vyema sheria 17 za mchezo wa soka. Ushahidi wa makosa ya waamuzi ni ujio wa mnarefa kutoka nchini Misri ambao walikuja kuchezesha mchezo namba 184 kati ya Simba na Yanga. 

Mchezo huo ulikumbwa na mikasa mingi ya kuharishwa, hadi ulipochezwa Juni 25. Si nia yangu kukumbusha yaliyotokea, lakini ifahamike ni somo kubwa kwa waamuzi wa soka nchini walilipata kutoka kwa mwamuzi Amin Omar toka Misri, namna ya kumudu mchezo, kuongoza na kusimamia sheria zote 17 za mchezo pasipo kulalamikiwa. Baada ya mchezo huo mashabiki na viongozi wapande zote pamoja na wadau walikiri kurithishwa na uwezo wa waamuzi waliochezesha mchezo huo. 

Nia yangu ni kuhakikisha kuwa msimu ujao waamuzi hawafanyi makosa kiasi cha kueletewa waamuzi toka nje. Hii si mara ya kwanza, hata serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliwahi kuleta Majaji toka Nigeria kusikilzia kesi ya uhaini kwa kile ilichodai walikuwa na uwezo mkubwa. Hilo lilikuwa na maana kuwa majaji wa Zanzibar walipuuzwa na kukejeliwa uwezo wao wa utendaji wa haki. Ingawa lilikuwa tukio la kisiasa lakini waamuzi wa Ligi kuu wanaweza kujifunza pia kwenye uendeshaji wa kesi ya uhaini uliofanywa na majaji wa Nigeria, pamoja na marefa kutoka Misri.

Mechi kusogezwa mbele

Mara nyingi ratiba ya Ligi Kuu inapopangwa inatakiwa kuendana na ile ya shirikisho la soka duniani, FIFA pamoja na shirikisho la soka Afrika, CAF. Lakini tumeshuhudia mechi kadhaa zikiahirishwa msimu ulioisha huku sababu zikiwa ni mgongano na  mechi za Kimataifa. Mechi kadhaa zililazimika kusogezwa mbele ili kuwezesha zile za mashindano ya kimataifa kama FIFA na CAF zichezwe. Ni wakati sasa kuondokana na mgongano huu ili kuwezesha Ligi Kuu kuwa na thamani yake pamoja na kukuza ushindani. TFF na Bodi ya Ligi  wanapaswa kuketi pamoja na kujadiliana namna nzuri kuhaikisha mgongano huu unakwepwa kwa namna yoyote ile msimu ujao.

Zawadi ya bingwa

Msimu ujao litakuwa jambo lenye afya zaidi kuhakikisha kuwa timu inayochukua ubingwa wowote inakabidhiwa hundi na kiasi chake kuwekwa kwenye akaunti zao kuliko kushuhudia malumbano kama yalivyotokea. Yanga na TFF ziliingia kwenye malumbano makali kwa sababu bingwa huyo alilalamika kutopewa zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la soka nchini kw akipindi cha miaka mitatu mtawalia. Ifahamike kuchelewesha zawadi ya bingwa si tatizo ikiwa kunakuwa na uwazi na ukweli kati ya pande zinazohusika. Lakini msimu uliomalizika tumeshuhudia Yanga wakiishutumu hata wadhamini  wa kombe la shirikisho, CRDB kwa madai haikulipa fedha za bingwa wa kombe wanalodhamini. Tukio hili lilisababisha wadhamini kujitokeza hadharani na kufafanua kuwa haikuwahi kuchelewa ama kutolipa fedha za bingwa wa kombe wanalodhamini. Malumbano ni afya lakini yanapofikia hatua ya kutiana aibu kama taasisi na wadau wa soka ni muhimu kuepusha kuharibiana heshima zilizojengwa kwa jasho na damu. Hivyo basi msimu ujao ni muhimu kuepushwa malumbano ya namna hii.

Jambo la pili ni kiwango wanachopewa washindi wa makombe. Ifahamike kiasi wanacholipwa bingwa wa kombe si kwamba ni kibaya lakini inatakiwa kuwa na zawadi ambayo inapandisha thamani ya Ligi Kuu na mashindano ya ndani kwa ujumla. Ligi Kuu ina kila sababu ya kushuhudia bingwa anafikisha zawadi ya shilingi Bilioni moja kwa msimu ikiwa mamlaka zinazohusika zitatilia mkazo katika thamani ya Ligi, maadili na uendeshaji usiotiliwa shaka. Wakati mwingine wadhamini hawajitokezi kwa sababu wanakwepa bali hawajui thamani halisi ya Ligi Kuu kimapato. Kwahiyo inafaa pia hata mshindi wa Kombe la shirikisho apandishiwe kiwango cha zawadi ambacho anakipata pale anapoibuka mshindi.

Tuzo za wachezaji bora

Ni muhimu kutambua kuondokana na makosa ya uteuzi wa wachezaji bora pamoja na kuhuisha na zawadi za wanaoteuliwa. Waendeshaji wa Ligi kuu na mamlaka ya soka nchini wanaweza kupandisha thamani ya tuzo ya kila mwezi ya mchezaji, makocha na watu wanaohusika. Tuzo hii inapaswa kuongezwa thamani kama chachu ya kuwahamasisha wachezaji kushindana zaidi. Pia ni tuzo ambayo inakwenda kuongeza thamani ya Ligi Kuu hasa kwa kuwavutia wachezaji na makocha wa kigeni kwani  wanatambua zipo fursa mbalimbali mbali ya ubingwa amabzo zinawapa heshima na kutengeneza CV zao vizuri. Fursa hizi ndogo ndogo zina nafasi kubwa kwa Ligi kuu na kivutio kwa wageni wanaoleta fedha nchini. Wakati tunasisitiza kutorudia makosa ni muhimu kukumbuka kubuni njia za ziada za kukuza mapato ya Ligi Kuu.

Adhabu za kadi nyekundu

Mara kadhaa tumeshuhudia malalamiko dhidi ya waamuzi namna wanavyotoa adhabu za kadi nyekundu zikiwa kinyume cha tafsiri ya sheria za soka. Wachezaji na makocha wameingia matatani mara kadhaa wakipingana na uamuzi unaotolewa na marefa kuhusiana na adhabu za kadi nyekundu. Kwa msingi huo msimu ujao uwe na mpya na usilete matatizo kama haya ambayo yanaharibu Ligi kuu.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version