Kati ya 1994 na 2013, England walifika fainali tano tu katika ngazi ya makundi. Ilikuwa kawaida kutolewa kwenye hatua za awali au hata kukosa kabisa kufuzu kwa mashindano husika…..
Inakaribia miaka 10 tangu wanahabari wa soka na watu wenye ushawishi mkubwa kwenye mchezop huo kukaribishwa kwa kile kilichoitwa ‘kupigania na kuilinda’ soka ya England.
Uchaguzi wa sehemu ulikuwa na hisia na kuhuzunisha, mwaka 1991, Millbank Tower, kwenye kingo za Mto Thames, ndio lilikuwa eneo mikutano muhimu kwenye historia ya soka ya England; eneo la siri la kukutania wenyeviti wa klabu na mtendaji wa televisheni kulidhihirisha kuwa kichocheo cha harakati za kuondokana kulikoashiria zama za Ligi Kuu.
Miaka 20 baadaye, Septemba 2013, mtendaji yule yule wa televisheni, Greg Dyke, alikuwa mwenyekiti wa FA alipochagua eneo lile lile kutoa kilio.
Dyke alizungumzia ‘athari zisizodhamiriwa’ za ukuaji wa Ligi Kuu. Mafanikio yake makubwa, akasema, yamekuja kwa kuwagharimu wachezaji wa ndani na timu ya taifa ya wanaume, iliyokuwa ikiandamwa na hali ngumu na kufanya vibaya kimataifa.
Huku idadi ya wachezaji wa ndani kwenye Ligi Kuu ikipungua kwa kiasi kikubwa mwaka huo, Dyke alionya juu ya hatima isiyo njema kwa England katika ngazi ya kimataifa, na kwa hakika ilishaanza kuonekana hivyo wakati huo.
Licha ya kufika robo fainali mara tatu mfululizo kwenye mashindano chini ya kocha Sven-Goran Eriksson, England walishindwa kufuzu kwa michuano ya Euro 2008, halafu tena wakaja kuzidiwa na kufunikwa kabisa na kikosi cha wachezaji wadogo cha Ujerumani kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2010.
Walijikuta udhaifu wao ukianikwa wazi na Italia kwenye hatua yar obo fainali ya Euro 2012. Walisonga mbele na kumaliza wakiwa wa mwisho kwenye kundi lao katika fainali za Kombe la Dunia 2014 na kutupwa nje ya Euro 2016 na Iceland katika hatua ya 16 bora.
Yalipofika majira ya vuli ya 2013, kile kilichokuwa kikiitwa ‘kizazi cha dhahabu’ kilikuwa kikifikia tamati yake – kwa maelezo Zaidi ni hali za watu kama Ashley Cole, Steven Gerrard na Frank Lampard — na kulikuwa na chipukizi wachache wa kiwango cha juu waliokuwa wakiibuka kubeba mzigo huo.
Wachezaji 11 kati ya 27 walioitwa na kocha Roy Hodgson kwa ajili ya mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia walikuwa na umri wa miaka 24 au pungufu. Lakini, kati ya hao 11 ni Raheem Sterling na Kyle Walker tu walifanikiwa kuchezea timu hiyo walau mechi 50.
Wengi wa hao wengine walipata mechi nyingi kuliko ambavyo waweza kukumbuka – Theo Walcott (47), Jack Wilshere (34), Ross Barkley (33), Chris Smalling (31), Phil Jones (27), Daniel Sturridge (26), Andros Townsend (13) na Tom Cleverley (13) — lakini, iwe ni kutokana na kiwango au masuala ya kuwa fiti, hakuna aliyekuja kuwa mchezaji wa muda mrefu kwenye Timu ya Taifa ya England, wakati ambao mashindano yalikuwa makali zaidi kuliko sasa.
Wakati wa fainali za michuano ya Euro U-21 ya majira ya kiangazi. England walimaliza mkiani kwenye kundi lao, wakifungwa na Italia, Norway na Israel. Ama kwa kikosi alichounda Stuart Pearce Kwenda Israel, ni Jordan Henderson na Danny Rose tu waliopata kucheza mechi 20 kwa Timu ya Taifa ya wakubwa ya England.
Ni wachache tu wengine (Wilfried Zaha, aliyebadili uraia kuwa wa Ivory Coast, Nathaniel Clyne, Craig Dawson, Jonjo Shelvey, Nathan Redmond na hatimaye Jason Steele) waliosonga mbele na kuweza kujijenga katika Ligi Kuu.
England wapo nafasi ya nne katika msimamo wat imu bora za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Euro 2024, baada ya kuanza kampeni yao ya kufuzu kwa kushinda mechi zote nne, ikiwa ni pamoja na ushindi wa kiushindani dhidi ya Italia tangu 1977.
Jumamosi jioni England walitwaa ubingwa wa Ulaya kwa U-21 kwa mara ya kwanza tangu 1984, wakiwapiga Hispania 1-0 kwenye fainali, huku golikipa James Trafford akiwa shujaa kwa kuzuia mkwaju wa penati ya Abel Ruiz kwenye dakika ya tisa ya muda wa nyongeza.
Anthony Gordon alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi, na hilo linasema makubwa juu ya ufanisi wa England huko Georgia, na kwamba kumekuwapo na wachezaji wengi wazuri kwenye kikosi cha Lee Carsley; watazame Trafford na mlinzi Levi Colwill.
Kati ya 1994 na 2013, England walifika fainali tano tu katika ngazi ya makundi. Ilikuwa kawaida kutolewa kwenye hatua za awali au hata kukosa kabisa kufuzu kwa mashindano husika.
Tangu 2015 wamekuwa washindi wa pili kwa mashindano ya soka Ulaya kwa U-17 mwaka 2017, washindi kwa U-19 mwaka 2017 na 2022, washindi wa U-17 Kombe la Dunia 2017 na sasa washindi wa U-21 Ulaya, wakiwa na matumaini makub wa tena kwa Kombe la Dunia kwa I-17 nchini Indonesia baadaye mwaka huu.
Huku idadi ya wanasoka wa ndani kwenye Ligi Kuu kuendelea kushuka imedhibitiwa, lakini si kwa kiasi kikubwa. Kutoka asilimia 38 iliyoainishwa na Dyke 2012, ilishuka hadi asilimia 30 msimu wa 2018/19, lakini ikapanda tena hadi asilimia 38 msimu wa 2020/21 kabla ya kushuka tena msimu uliopita hadi asilimia 34.
Muongo mmoja baadaye, ada kubwa zaidi kupata kulipwa kwenye ulimwengu wa soka ililipwa kwa kiungo wa England, Bellingham, akijiunga na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya awali ya £88.5 milioni, kukiwa na uwezekano wa kuongezeka hadi £115 milioni. Kiwango hicho kitaongezeka pale Declan Rice atakapokamilisha uhamisho wake wa £105 milioni kutoka West Ham United kwenda Arsenal. Ada zilizolipwa kwa ajili ya Mason Mount (hata kama alikuwa kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba Chelsea) na James Maddison pia ni kati ya ofa kubwa 10 za msimu wa kiangazi.
Linapokuja suala la ada hizi, jibu rahisi ni kusema kwamba wanasoka wa England wamekuwa wakiwekewa bei kubwa kupita kiasi. Ni kweli kwamba bei zimekuwa kubwa kwa wachezaji walio katika nyakati za kati za misimu yao ya uchezaji hivyo kwamba klabu huamua Kwenda ng’ambo kuchukua wachezaji.
Kabla ya kiangazi cha 2021, Harry Maguire alikuwa mchezaji pekee wa England kupata kufikia bei ya kuvuka £50 milioni. Kwa sasa watatu kati ya wachezaji 12 ghali zaidi duniani ni Bellingham, Rice na Jack Grealish.
Kwa mujibu wa CIES Football Observatory, wachezaji watatu kati ya tisa walio ghali zaidi duniani kwa sasa ni wa England; Saka (wa tatu), Bellingham (wa nne) na Foden (wa tisa). Wa nane kwenye orodha hiyo ni Jamal Musiala, aliyezaliwa Ujerumani kisha akahamia England akiwa na umri wa miaka saba – lakini si Mwingereza japo ni zao la soka ya England. Ndivyo ilivyo kwa yule aliyesajiliwa na Borussia Dortmund kwa €30 milioni, Felix Nmecha, mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani aliyeanza kujengwa akiwa na akademia ya Manchester City.
Wachezaji wengine 12 wa England wapo kwenye 100 wakubwa zaidi kibei, baadhi yao (Marcus Rashford, Trent Alexander-Arnold and Harry Kane) wangeweza kufikiriwa kuwa na bei zaidi kama wangekuwa na muda mwingi zaidi uliobaki kwenye mikataba yao.
Mfumo wa CIES unachukulia kwamba suala ni nguvu za soko lakini pia vipaji – ikimaanisha kwamba wachezaji kwenye Ligi Kuu ya England kwa muundo ulivyo ni ghali zaidi. Miaka 10 iliyopita wachezaji waliokuwa wamewekewa bei kubwa zaidi walikuwa Wayne Rooney, Theo Walcott, Daniel Sturridge, Joe Hart, Jack Wilshere, Danny Welbeck na Phil Jones.
Bei za wachezaji wa England zimekuwa zikikuzwa tu; tofauti kwa mwaka huu ni kwamba klabu kubwa zaidi na makocha bora kabisa wamekuwa wakichukulia kwamba bei hizo zinastahili – na hiyo inawakilisha mabadiliko katika zama za wenye vipaji wa England kukaribia kuachwa nyuma.
Pep Guardiola alikuwa amekaa Manchester City kwa miezi michache tu alipoanza kuzungumzia viwango vya wachezaji wa England aliokuwa amewaona Ligi Kuu ya England, akiwazungumzia Kyle Walker, Danny Rose, Eric Dier, Dele Alli na Kane, waliokuwa wakicheza chini ya Mauricio Pochettino pale Tottenham Hotspur, pamoja na wachezaji wake wawili; Stones na Sterling.
Aliweka wazi kwamba wachezaji wa England wamekuwa wakiwekewa bei kubwa kuliko uhalisia. “Kusajili wachezaji hawa ni ngumu, ni ghali mno,” akasema.
Hata hivyo, kadiri muda ulivyokwenda amekuwa akiwakumbatia wenye vipaji hao wa England na wamechangia kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo. Kucheza chini ya Guardiola kunahitaji zaidi ya kipaji; inabidi kujielewa sana na kuwa na ufundi mkubwa.
Baadhi ya wachezaji waliofika fainali za Ulaya za U-21 na England 2009 – Joe Hart, Micah Richards, Lee Cattermole, Mark Noble, James Milner, Theo Walcott — walifikia kuwa na wakati mzuri kwenye Ligi Kuu ya England, wa aina ya pekee akiwa ni Milner.
Kwa kunukuu mwandishi wa masuala ya soka, Jonathan Wilson, wachezaji sita kwenye kikosi cha Ujerumani (Manuel Neuer, Jerome Boateng, Mats Hummels, Benedikt Howedes, Sami Khedira, Mesut Ozil) walisonga hadi kutwaa Kombe la Dunia miaka mitano baadaye, wakati saba wa England (Cattermole, Nedum Onuoha, Danny Rose, Adam Johnson, Jack Rodwell, Craig Gardner, Fraizer Campbell) walifikia kuchezea Sunderland.
Kwa muda mrefu, ilichukuliwa kwamba akademia za klabu za England zilikuwa zikiendekeza ngazi Fulani za wachezaji ambao hawakufikia kiwango cha kuwa bora zaidi kwenye Ligi Kuu. Hali hiyo ilizidi pale Guardiola alipoanza kuhubiri aina ya uchezaji, ikiwamo ufundi na umiliki wa mpira, viwango ambavyo wachezaji wengi wa England hawakuwa navyo.
Ikiwa kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa England kilivuma tangu wale waliozaliwa 1974 (Sol Campbell na Paul Scholes) hadi wale wa 1982 (Jermain Defoe), basi si wachache zaidi ya 15 waliochezea timu ya taifa zaidi ya mara 50 England na saba kati ya hao (Gary Neville, David Beckham, Lampard, Rio Ferdinand, Michael Owen, Gerrard na Cole) walau mara 80. Wengi wao walipanda ngazi za juu kwenye soka ya England na Ulaya kwa ujumla kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kwa kizazi kilichokuja baadaye, waliozaliwa kati ya 1983 na 1992, ni saba tu (Rooney, Glen Johnson, Milner, Hart, Gary Cahill, Henderson na Walker) walifikia kucheza mechi 50 timu ya taifa na ni Rooney mwenyewe aliyefikia 80, japo Henderson na Walker walikaribia.
Kwa wale waliozaliwa baada ya hapo, Kane na Sterling wameshavuka mechi 80 wakiwa katika miaka yao ya mwisho ya 20. Stones atafikia hivi karibuni. Rice, 24, kacheza mechi saba tut imu ya taifa, Mount, 24, Foden, 23, Saka, 21, na Bellingham, 20, tayari wana mechi 36, 25, 28 and 24 mtawalia.
Kitu kimoja kinachoweza kusemwa kwa uhakika ni kwamba toka kutokuwa na matumaini muongo mmoja uliopita, England sasa wanaonekana kuwa washindani, kutokana na kizazi cha wachezaji mahiri kilichochipuka na kuchanua kwenye timu ya taifa, wengi wao wakiwa tayari wameonja matunda ya timu ya taifa ya vijana.
Comments
Loading…