in , , ,

Wachezaji kumiliki timu lina maana gani?

MACHO na masikio kwa sasa yapo kwa wachezaji wanaostaafu kucheza soka sehemu mbalimbali duniani. Wachezaji hawa wamekuwa wakisababisha maswali mengi ikiwemo nini wanachoweza kukifanya baada ya kustafau? Je waingie kwenye uchambuzi kama akina Amri Kiemba, Jemedari Said, Rio Ferdinand, Gary Neville na wengineo? 

Katika maswali hayo ndipo unaibuka mjadala kuhusiana na uamuzi wa wafanyabiashara mbalimbali kuwashirikisha wachezaji wanaostaafu au wastaafu kumiliki timu za soka. Je wachezaji watafanyia nini mabilioni ya fedha wanayovuna wakati  wa uchezaji wao? 

Hayo na mengine ni sehemu ya maswali muhimu katika mchezo wa soka kwa sasa. wachezaji wamekuwa sehemu ya umiliki wa wa timu kama wale Class of 92 wa Manchester United wanaomiliki klabu ya Salford City. 

Wapo wengine pia wameingia umiliki w aubia kati yao na wafanyabiashara mbalimbali. Pia inaonesha kuwa mchezo wa soka ni biashara yenye faida na muhimu sana kwa ulimwengu, na jina la mwisho ambalo limejitokeza katika umiliki wa klabu ya soka ndilo limetanua mjadala zaidi. Jina hilo linahusiana na staa wa zamani wa Wales, Gareth Bale ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka. 

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za kimichezo zimesema kuwa Gareth Bale ni jina jipya ambalo linaingia kwenye mchakato wa kumiliki klabu ya Cardiff City. Inaelezwa kuwa Gareth bale yupo kwenye mazungumzo ya kuchukua sehemu ya umiliki wa klabu hiyo ya Ligi daraja la kwanza baada ya wamiliki wapya kuandaa mpango wa kumshirikisha staa huyo wa zamani wa Real Madrid. 

Kampuni inayotaka kuinunua Cardiff City inakusudia kuhakikisha inaingia dili lingine la Gareth Bale kama sehemu ya kuwavutia mashabiki wa soka Wales. Wamiliki hao wanamwona Bale kama nembo muhimu ya Wales ambayo inafaa kutumika kukuza chapa ya Cardiff City. Bale alianza kufanya akzi ya uchambuzi mara baada ya kustaafu soka mwaka 2024. 

Hata hivyo suala la umiliki wa timu halipo kwa wachezaji wa soka pekee, bali hata wadau wengine wa michezo wamekuwa wakifanya hivyo kwenye michezo mingine. Wachezaji waliostaafu kwenye michezo hiyo nao wanamiliki timu za michezo mingine, mbali ya mchezo wa soka.

TOM BRADY-Brimingham City

Staa huyo wa mchezo wa NFL anamiliki klabu ya Birmingham City. Timu hiyo ilinunuliwa na Tom Wagner wa kampuni ya Knighthead Capital kabla ya kumshawishi Tom Brady kuwa sehemu ya umiliki wake. Knighthead Capital ilikuwa nyuma ya dili la pauni milioni 35 ya kuchukua umiliki wa klabu hiyo mapema mwaka 2023 kabla ya Tom Brady kujiunga kwenye bodi ya timu hiyo. 

Baada ya kuingia wamiliki wapya walimwajiri Wayne Rooney kuwa kocha wao, lakini hawakuwa na mafanikio yoyote hadi pale walipoamua kumtimua. Lakini uamuzi w akumtimu ulikuwa mdogo na ulichelewa mno. Brady na wenzake walimfukuza kazi John Eustace wakati klabu hiyo ilipokuwa kwenye mchuano wa kucheza mechi ya mtoano, lakini lilikuwa kosa kubwa kwnai Rooney aliyeajiriwa badala yake hakufanikiwa kufanya chochote. Hata pale walipoajiriwa Tony Mowbray na Gary Rowett ili kuokoa msimu wa timu hiyo lakini hali ya mambo ilishindikana.

Msimu mpya ulipoanza walimteua Chris Davies kuwa kocha wa Birimingham na walimaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu. 

Kushika nafasi hiyo hakukuja kirahisi kwani walilazimika kusajili mara 30 kuliko timu nyingine kama Wrexham, ambapo Jay Stansfield mmiliki mwenye hisa kubwa alinunua kwa pauni milioni 15.

Tom Wagner ambaye ni mfanyabiashara na mtaalamu w afedha, aliwahi kueleza malengo yake kwa timu hiyo ni kuhakikisha anakuza chapa yao. “Ukifika jiji la New York, unawaona watu wamevaa jezi za Birmingham City, unaenda Los Angels pia watu wamevaa jezi za Birmingham City wakitembea mitaani. Sina uhakika kama wanaelewa kama wanafahamu kuhusu Birmingham City ni nini. Hatutakuwa na haraka ya kuwafahamisha Birmingham City ni nini, lakini tunataka kuona siku moja wanaifahamu kwa undani klabu hii na wanajivunia nayo,” alisema Tom Wagner alipozungumza na The Atletic.

LUKA MODRIC-Swansea City

Nahodha huyu wa Real Madrid anatarajiwa kuachana na klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia la klabu. Nyota huyo toka nchini Croatia ambaye ameichezea nchi yake michezo 186 amejiunga na Swansea City kama mmiliki mwenza. Wamiliki hao wapya wamesema kuwa wanataka kuona klabu hiyo inaongeza thamani na kuleta faida kwa mashabiki wa Wales. 

Swansea City ina mashabiki wengi ambao wanapenda kuambatana na timu hiyo, na hivyo Luka Modric ameliangalia soko la soka la Wales ambao linawindwa na wamiliki wengi kama walivyotajwa hapo juu ambao wamechukua umiliki wa klabu ya Cardiff City. 

Wamiliki hao wanataka kuona Swansea City inaondokana na hasara kama waliyopata msimu uliopita ambapo ilikuwa kiasi cha pauni milioni 15 mwaka 2024 wakati mwaka 2023 walipata hasara ya pauni milioni 19. Luka Modric amekuwa bega kwa bega na wakala wake Broja Couce ambapo amethibitisha kuwa mteja wake amevutiwa na suala la uwekezaji katika klabu ya Swansea City.

RONALDO DE LIMA-Real Valladolid

Staa wa zamani wa Real Madrid, Barcelona na Inter Milan anamiliki klabu ya Real Valladolid. Nyota huyo anasifiwa kwua mshambuliaji mahiri kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka ni raia wa Brazil alianza kumiliki klabu wakati ambao alikuwa anaelekea kustaafu soka. Akitumia kampuni ya O Femomeno alinunua hisa za kumiliki Valladolid wakati ikiwa ligi daraja la pili nchini Hispania. 

Uweekzaji wake uliongezeka na kuleta tija zaidi baada ya kuinunua klabu hiyo mwaka 2018 na kuhahidi kuleta mapinduzi katika historia yake. Ronaldo De Lima alinunua hisa asilimia 51 zenye thamani ya pauni Milioni 22.3 na kuchukua madaraka ya urais wa klabu hiyo. Ameongoza timu hiyo kwa miaka minne hadi sasa. mafanikio yake ni kuirudisha Ligi kuu Hispania, La Liga. Lakini licha ya kupanda daraja mara mbili, pia ilishuka daraja mara mbili katika kipindi cha Ronaldo de Lima. Baadaye aliamua kuuza hisa zake katika klabu hiyo kwani mashabiki wlaianza kuandamana kwa mabango kutaka nyota huyo aondoke klabuni hapo.

ZLATAN IBRAHIMOVIC

Mshambuliaji matata katika ulimwengu wa soka. Ni miongoni mwa wale wenye uata mwingi wakati akiwa mchezaji, lakini mwaka 2023 aliamua kustaafu soka. Amepata kuzichezea klabu za Barcelona, Juventus, Manchester United, PSG, AC Milan. 

Kwa sasa ana umri wa miaka 43, lakini alishajiandaa na maisha baada ya kustaafu soka. Nyota huyo alinununua hisa katika klabu ya Hammarby IF kwa asilimia 23.5. 

Klabu hiyo inashiriki ligi kuu Sweden na makao makuu yake yapo jijini Stockholm. Hata hivyo uamuzi wao wake wa kununua hisa katika klabu hiyo uliwakera mashabiki wa Malmo ambako alianzia maisha yake ya soka na kuamua kung’oa sanamu yake.

PAOLO MADILINI-

Beki mahiri wa kushoto na kati kutoka Italia na klabu ya AC Milan. Baada ya kustaafu amefanya kazi kama mmoja wa viongozi wa soka katika klabu ya AC Milan, lakini hakukaa mbali na umiliki wa timu. Mwaka 2015 alikuwa mmiliki mwenza wa klabu ya Miami F.C ya Marekani inayoshiriki Major Soccr League ya nchi hiyo. 

Alesandro Nesta alikuwa kocha wa kwanza wa klabu hiyo wakati ikiweka mipango ya kufanya vizuri. Mwaka 2018 Paolo Maldini aliondoka klabuni hapo baada ya kukubali kuwa Mkurugenzi wa michezo wa AC Milan.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

67 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
man city

Man City yaingia anga za Yanga, Simba

Tanzania Sports

Waamuzi Ligi Kuu wachukue somo hili