Menu
in

Waamuzi kupewa mafunzo

Chama cha waamuzi wa soka hapa  nchini Tanzania  (FRAT) kwa kushirikiana na shirikisho la soka Tanzania TFF kinatarajia kuandaa kuendesha kozi kwa waamuzi wenye beji ya FIFA na waamuzi wa daraja la kwanza kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa michuano ya ligi kuu Tanzania bara.

Mwenyekiti wa chama cha waamuzi nchini  Tanzania Omary Abdul Kadir amesema mafunzo hayo yamelenga katika kuwapiga msasa waamuzi hao ili kuwa na uwezo wa kutosha kuchezesha michuano hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema waamuzi watakaofanya vibaya katika kozi  hiyo watakosa nafasi ya kuchezesha michuano ya ligi kuu msimu ujao.

Katika kozi hiyo pia yatafanyika mafunzo ya COOPER TEST (mitihani ya majaribio kwa waamuzi hao) ambao kutafanyika mafunzo ya vitendo na nadharia na muamuzi atakaefanya vibaya basi hatochezesha michuano hiyo.

Mwenyekiti huyo wa FRAT hakutaja idadi ya waamuzi wanaowahitaji kuchezesha ligi kuu usimu ujao ila akasema watachagua muamuzi wa kuchezesha ligi hiyo kutokana na uwezo wake na yule mwenye uwezo mdogo haitajiki.

Kila msimu wa ligi kuu hapa Tanzania timu mbalimbali pamoja na washabiki wa soka wamekuwa wakiwalalamikia waamuzi wake wakisema wanauwezo mdogo huku wengine wakienda mbali kwa kusema eti ndio chanzo cha kushuka kwa soka la Tanzania na wengine wakisema wanapokea rushwa ila hadi leo hakuna alisibitisha kama kweli kuna rushwa katika hilo.

Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao wa August  tarehe 23/ 2009  na timu 12 zinashiriki ligi hiyo huku ikiwa na timu tatu zilizopanda daraja msimu uliopita.

Timu zilizopanda daraja ni Maji maji  ( Wanalizombe) ya Songea mkoani Ruvuma, African Lyon  (Wazee wa TMK) na Manyema Ranges (Mkuki wa Sumu) zote za Dar es salaam.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version