in , , ,

Vita ya Ubingwa Ligi Kuu Tanzania

Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi sasa hauna mwenyewe. Kila timu inafanya jitihada kushinda michezo yake pamoja na kuhakikisha wanapata alama ugenini. Baadhi ya timu zimekata tamaa ya kupigania ubingwa ubingwa huo, na zingine zinahaha kujinusuru kwenye mstari wa kushuka daraja. 

Makocha nao wamefurumshwa katika timu mbalimbali na kuifanya Ligi iwe ngumu na ushindani kuwa mkali. Pamoja na yote zipo sifa za timu kubwa bingwa na dalili huwa zinaonekana. Lakini pia upo wakati timu zinazodhaniwa au kuaminiwa zitanyakua ubingwa huwa zinakutana na wakati mgumu. Hapa England kumetokea mashindano ya Carabao ambapo Manchester City imetupwa nje ya mashindano baada ya kuambulia kichapo. Hakuna aliyetegemea, lakini imetokea. Je vipi hali ya Ligi kuu nyumbani Tanzania?

Pointi ngumu nzuri

Singida Black Stars ni miongoni timu zilizokuwa gumzo hivi sasa. Ni timu ambayo inamilikiwa na Mbunge Mwigulu Nchemba imeonesha uwezo mkubwa wa kupambana katika Ligi msimu huu ambapo inaifundishwa na Patrick Asussens raia wa Ubelgiji. Sifa kubwa ya timu yenye kusaka ubingwa ni kupata pointi nzuri kwenye mechi ngumu. 

Mara nyingi mechi ngumu huwa zinatazamiwa kuona yule mshindi anakwenda kuchukua ubingwa, ingawaje upo wakati timu huwa ipoteza mchezo. Angalia Arsenal msimu uliopita ilipoteza pointi muhimu dhidi ya Manchester City, halafu ikawa imefungwa mechi nyingine kadhaa hivyo kupunguza uwezo wa kuchukua ubingwa. Kocha wao Mikel Arteta amegundua mbinu muhimu ya kupambania pointi ngumu. 

Mechi ngumu amekuwa akicheza kwa mbinu chafu na kila aina ya uhuni kuhakikisha timu inaibuka na ushindi. Wachezaji wanaonekana kuelewa maagizo, na kila kitu wanakifanya kuhakikisha hawafungwi mechi ngumu. Kwao alama moja dhidi ya timu ngumu ni muhimu. Singida Black Stars walikuwa wanaongoza Ligi kwa muda mrefu lakini mchezo wao dhidi ya Yanga wamepoteza uongozi kwa kufungwa bao moja kwa nunge. kw amaana hiyo vita ya ubingwa ni lazima upate pointi kwa timu ngumu. Hapo tayari Singida Black Stars wamepoteza alama.

Wachezaji wa kuamua mchezo

Kila timu yenye nia ya kushinda ubingwa lazima iwe na wachezaji wa kuamua mchezo. Hawa ni wachezaji ambao kutokana na juhudi binafsi wanaiwezesha timu kuibuka na ushindi. Katika michezo kadhaa Yanga hawakucheza vizuri lakini walivuna pointi kutokana na juhudi za Max Nzengeli na Pacome Zouzoua. Kocha anapokuwa na wachezaji wenye maarifa binafsi na ubunifu wanamsaidia kurahisisha kazi ya kupata pointi. Hawa ni wabunifu na wana muono wa mbali katika kutafuta ushindi. Ni wachezaji wanaofunga mabao katika mazingira magumu au kutengeneza mabao maeneo yasiyotabiriwa.

Safu ya ushambuliaji na ulinzi

Ili kuibuka na ushindi lazima timu ifunge mabao. Lakini ili ushindi huo udumu lazima safu ya ulinzi ihakikishe inalinda lango lao na kuzuia kufungwa. Washambuliaji makini na wenye kutumia nafasi chache wanazopata ni muhimu kwa timu inayotafuta ubingwa. Mshambuliaji mwenye kuweza kutumia nafasi tatu kati ya tano anazopata kwenye mchezo ni silaha kubw aya kuibuka na ushindi. Kwa maana hiyo safu ya ulinzi nayo inatakiwa kulinda ushindi wao ili kuwazuia wapinzani wao kuleta madhara. Kila upande wa safu ya ulinzi unapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanalinda lango.

Uamuzi wa haraka

Makocha ni sehemu kubwa ya kuamua matokeo ya mchezo. Upo wakati timu inahitaji mabadiliko na upo muda hawahitaji kabisa. Kocha anapofanya uamuzi wa haraka kuinusuru timu isiingie kwenye mtego wa wapinzani na kuruhusu mabao anasifika na kuelekea kwenye ubingwa. 

Kocha anapoona timu yake inazidiwa maarifa na kukosa mbinu za kupenya ngome ya adui ni lazima afanye maamuzi ya haraka; kuwapa maelekezo mapya wachezaji wake ama kusubiri hadi wakati wa mapumziko. Vilevile katika muda wa lala salama pia kocha anawajibika kuchukua uamuzi wa haraka wenye nia ya kuiwezesha timu kulinda ushindi,kusawazisha au kutafuta alama tatu za ushindi. Endapo kocha anakuwa mzito wa kufanya maamuzi ikiwemo kuchelewa maana yake vita vya ubingwa vinamwacha nyuma.

Viongozi wastahimilivu

Kila timu inahitaji viongozi wenye ustahimilivu na kuamini katika mipango yao. Timu inapokuwa na viongozi makini maana yake wanaunda kikosi ambacho kitakuwa na ari ya kupigania ushindi zaidi. Viongozi watahakikisha wachezaji wamelipwa kwa wakati, hamasa za fedha na kadhalika vyote wanatakiwa kuwapa wachezaji wao. Kwahiyo uongozi ni sehemu ya vita ya kuwania ubingwa ikiwemo kumuunga mkono kocha, kuzungumza na wachezaji, kuwa karibu nao na kuhakikisha wanaweza kuibuka na ushindi

Mashabiki nao wamo

Kila timu duniani inaamini mashabiki ni wachezaji wa 12 uwanjani. Hamasa wanayotoa kwa timu yao na kuwatia presha wapinzani ni miongoni mwa mambo yanayopa ari wachezaji. Mashabiki wana mchango mkubwa katika kukamilisha ushindi wa timu. Uhusiano mzuri na mashabiki ndiyo huchangia wao kujazana viwanjani na kuishangilia timu yao. Hiyo ni siri ya ushindi wa timu yoyote.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

61 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ubora wa refa katika vita ya Yanga na Azam

Vipaji Vya Umiseta Na Umitashumta Huenda Wapi?