in , , ,

Vipaji Vya Umiseta Na Umitashumta Huenda Wapi?

Timu ya Dodoma Girls Volleyball, ilitokana na matunda ya Umitashumta na Umiseta.

Kila mwaka,huandaliwa mashindano ambayo yanahusisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari hapa Tanzania.Mashindano ambayo hufahamika kama Mashindano ya UMISETA (Umoja wa Michezo ya Sekondari Tanzania) na UMITASHUMTA (Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania) ambayo nikiri kuwa ni sehemu muhimu ya mfumo wa elimu ya michezo nchini Tanzania.  

Mara zote kupitia mashindano haya lengo kuu ni kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo na kuimarisha mshikamano, nidhamu, na maadili mema. Ingawa wanafunzi hushiriki michezo kwa malengo ya kuonyesha uwezo wao na kushindana, vipaji vinavyoibuliwa vina nafasi kubwa ya kutumika katika maeneo mengine ya kitaifa na kimataifa lakini swali kubwa la kujiuliza ni kwamba VIPAJI VYA UMISETA NA UMITASHUMTA HUENDA WAPI?

Tumekua mara zote tukilalamika kuhusu kukosa wawakilishi wazuri katika michuano mbalimbali ya kitaifa na ile ya kimataifa katika maeneo mbalimbali ambayo kama nchi tumekua tukipeleka wawakilishi wetu, katika mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA huwa kuna michuano kadhaa kama vile kukimbia mbio ndefu na fupi, kucheza kikapu , mechi za mpira wa miguu na michezo kadha wa kadha ambayo kwa namna moja au nyingine kupitia vipaji ambavyo vinakua vinaonekana ndio ingekua tiba bora katika ichezoambayo tumekua tukiangukia pua kimataifa.

Ni wakati wa kuvitumia vipaji vinavyoibuliwa kupitia UMISETA na UMITASHUMTA katika ngazi zote za vyama vya michezo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa vinatunzwa na kutumika ipasavyo kuiletea nchi manufaa kwani kupitia vipaji hivi itaipa Tanzania nguvu ya kushindana na mataifa mengine katika mashindano ya kimataifa, kama vile Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na Michezo ya Jumuiya ya Madola. Uwekezaji katika vipaji hivi husaidia kuimarisha sifa ya taifa katika nyanja ya michezo na kukuza mshikamano wa kitaifa kupitia mafanikio ya kimataifa.

Tumekua tukiona vijana wengi wenye vipaji wakiishia zao mtaani na wengi wao unakuta ni wale ambao walifanya vizuri sana kutoka katika UMISETA au UMITASHUMTA ni wakati ambao sasa kuandaa mfumo bora wa kuwafuatilia wale ambao walifanya vizuri katika michuano hii na kuwaingiza katika mfumo rasmi wa michezo kwa kuwaendeleza kimichezo huku wakiwa pia wanasaidiwa katika kuendelezwa kimasomo.

Wanafunzi wenye vipaji wanaweza kupewa ufadhili wa masomo ndani na nje ya nchi, jambo linalowasaidia kuendelea na masomo yao bila vikwazo vya kifedha. Katika nchi mbalimbali, wanafunzi wenye vipaji maalum katika michezo hupewa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu na taasisi za elimu za michezo ili kukuza na kuboresha uwezo wao. Hii inawapa nafasi ya kupata elimu ya juu sambamba na kuboresha vipaji vyao jambo ambalo linaweza kusaidia kuunda wataalamu wa michezo na wachezaji bora wenye ufahamu wa kitaaluma wa sekta hiyo.

Hatukatai kuwa michezo ni sehemu ya utamaduni wa Jamii ya watanzania kama zilivyo Jamii nyingine huko duniani, na kupitia mashindano kama UMISETA na UMITASHUMTA, Tanzania inaweza kuendeleza na kuhifadhi tamaduni zake. Mashindano haya mara nyingi huambatana na shughuli za kitamaduni kama vile ngoma za asili, mavazi ya jadi, na nyimbo za kitamaduni, ambazo zinawafundisha vijana kujivunia utamaduni wao na kuuenzi. Kwa namna hii, michezo inachangia kudumisha tamaduni za Tanzania na kuleta mshikamano wa kitaifa kwa kuzitambulisha jamii mbalimbali zinazoshiriki na kupitia njia hii wapo amabo watatamani kuwa wanashiriki katika mambo ambayo yanahusu kuijenga historian a tamaduni ya Tanzania katika vituo vya utamaduni.

Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA yana mchango mkubwa katika kubaini na kukuza vipaji vya vijana wa Tanzania. Vipaji hivi vinaweza kutumika katika maendeleo ya michezo kitaifa na kimataifa, Ni muhimu kwa serikali, mashirika, na wadau wa michezo kuwekeza katika mashindano haya na kutoa fursa zaidi kwa vijana wenye vipaji kujiendeleza. Kwa kufanya hivyo, Tanzania inaweza kuwa na kizazi cha wanamichezo wenye ushindani na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha kuliko kukaa na kila siku kuhoji pesa zinazotumika kuandaa mashindano haya na namna gani hatuoni faida kupitia vipaji ambavyo vinakua vimezalishwa na mashindano haya kwa sekondari na yale ya shule za msingi. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Vita ya Ubingwa Ligi Kuu Tanzania

Tanzania Sports

Liverpool watadumisha tabasamu lao?