Menu
in , , ,

Vipi Watanzania Kuwa Na Jezi Za Timu Ya Taifa?

Tupo katika kipindi ambacho dunia ya Sasa katika mpira wa miguu wapo Watanzania ambaokumiliki jezi ya klabu ni fahari kubwa zaidi kuliko kumiliki jezi ya timu ya Taifa.Mimi nimekua miongoni mwa wale ambao nimekua nikihudhuria katika Mechi mbalimbali

Tunashindwa Vipi Watanzania Kuwa Na Jezi Za Timu Ya Taifa?

ambazo zinahusisha timu ya Taifa haswa ya wanaume katika uwanja wa Benjamin Mkapa lakinikinachonitatiza zaidi ni kwanini watu wanakua hawavai jezi inayotuwakilisha watanzania wotezaidi sana utakuta watu wanavaa jezi za klabu wanazoshabikia hapa nyumbani Tanzania lakinipia na zile ambazo unakuta ni za klabu pendwa za Ligi kubwa barani Ulaya.

Niliwahi kushuhudia mchezo wa kufuzu AFCON kati ya Ethiopia dhidi ya Jamhuri yaKidemokrasia ya Congo ambao ulichezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kumbuka hawatuko nao kundi Moja kufuzu AFCON ya pale nchini Morocco , kwenye mchezo huu Ethiopiawalikua nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwani baada ya suluhu dhidi ya Tanzaniahawakuondoka walibakia kuutumia uwanja wa MKAPA kwa mchezo dhidi ya Jamhuri yaKidemokrasia ya Congo.

Tanzania Sports
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars

Kitu pekee ambacho kilinifurahisha ni namna ambavyo mashabiki Wa timu ya Taifa ya Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo walivyokua wamevaa jezi ya timu yao ya Taifa Kwa wingi kabisakatika mchezo ule ndipo kikawa kinaniwazisha na mimi kama Mtanzania ambaye mzalishaji wajezi hii yuko hapahapa Tanzania ni kipi kinatufanya tusiwe na hamu ya kuvaa jezi ya timu yaTaifa?

Wengine watakuambia zimekua na bei sana kuzinunua lakini hapohapo utakuta mtu kavaa jezi ya klabu anayoshabikia Ligi Kuu ya Tanzania Bara ndipo unapokuja kujiuliza mbona bei ya jezi ya klabu ni kubwa zaidi ya Ile ya Timu ya Taifa?

Kuna shabiki mmoja aliwahi kuniambia jambo ambalo naweza kusema kwa namna moja aunyingine lina mashiko kwamba Watanzania wengi wana uhusiano wa karibu na timu zao zaklabu kwa sababu klabu hizo zinawakilisha sehemu za karibu na maisha yao ya kila siku kamaule utani wa Simba na Yanga, lakini pia ukitazama ni kwamba Mashabiki hushirikiana na klabuzao kwa kiwango cha juu kupitia michezo mingi ya msimu, jambo linalowafanya kujihisi kuwana umoja zaidi na klabu zao kuliko Timu ya Taifa, ambayo hucheza mara chache zaidi.

Baadhi ya Mashibiki wa Taifa Stars, wakiwa na sare ya vilabu

Nikiri kwamba sikatai kabisa kuwa klabu kubwa kama Simba na Yanga zina historia ndefu bilakusahau kuwa utamaduni wa soka wa Tanzania umejengwa kwa kiasi kikubwa kuzunguka hiziklabu ukitazama pia ushawishi wa mashabiki wa klabu hizi ni mkubwa bila kusahau kuwa najezi za klabu hizo zinaonekana kuwa alama ya utambulisho wa kijamii jambo ambalo linapelekeawatu wengi kuona kuvaa jezi za klabu zao kama njia ya kujitambulisha na jamii fulani, badala yakuhusika na timu ya taifa.

Nadhani pia kupitia maelezo kama haya ya wadau ambao ndio wanavaa na kwenda uwanjani ndipo ambapo kunakuja mawazo mengi zaidi ya kipi kifanyike ili kuhakikisha kuwa mamboyanaenda sawa kwa Watanzania kuwa na jezi za timu ya Taifa na kuzivaa kwa wingi kwanitunaelekea katika michuano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania itakua Moja kati ya mwenyejiwa michuano hii.

Ni wakati ambao ubunifu wa jezi unapaswa kuboreshwa ili kuvutia mashabiki kwani wapoambao utakuta hapendi kuivaa jezi hiyo kutokana na jinsi ubunifu wake ulivyo hivyo jezi mpyaza Taifa Stars zinapaswa kuwa na ubora wa juu, zinazovutia kimtindo na zinazojenga hisia yaumoja.

Pia ni muhimu kuwa na jezi maalum ambazo zinatambulisha tamaduni na alama za Taifa la Tanzania ili kuongeza mvuto wa uzalendo.Nadhani kwa upande wa mzalishaji mkuu wa jezi hizi afahamu kwamba jezi za Taifa Starszinapaswa kupatikana kwa urahisi katika maeneo mengi ya nchi na ziwe na bei nafuu tofauti nazile za klabu ili kila mtu aweze kumudu. Kufanya jezi hizi zipatikane kwa wingi katika madukaya michezo na hata kwenye vituo vya michezo inaweza kusaidia sana kuongeza ununuzi.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version