in , , ,

Vinara wa ligi wapunguzwa nguvu

*Arsenal, Newcastle, Stoke washinda

Timu zilizo juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) zimevutwa shati kwa baadhi kulazimishwa sare au kufungwa.
Vinara Chelsea walibanwa na Southampton kwa bao 1-1 hivyo kushindwa kuongeza pointi tatu muhimu kuongeza pengo na wanaofuata.

Wanaoshika nafasi ya pili, Manchester City nao walijikuta wakibanwa na Burnley walio eneo la kushuka daraja.
Man City walishaongoza kwa mabao 2-0 hadi muda wa mapumziko, lakini walidorora, wakaruhusu mabao hayo kurudishwa, hivyo kuambulia pointi moja na sasa wana pointi 43, tatu nyuma ya Chelsea.

Vijana wa Louis van Gaal, Manchester United nao hawakufurukuta mbele ya Tottenham Hotspur katika mechi ya mchana, ambapo walikwenda suluhu na kosa kosa nyingi. Wamebaki nafasi ya tatu kwa pointi 36.

Chini yao ni Southampton wenye pointi 33 sawa na Arsenal. Vijana wa Arsene Wenger walipata ushindi wa 2-1 wakiwaengua West Ham katika nafasi ya tano na kuwatupa ya sita.
Kwa sare yao tasa na Man U, Spurs wamebaki nafasi ya saba wakiwa na pointi 31 sawa na West Ham.

Swansea wanakaocheza na Liverpool Jumatatu hii nao wamebaki nafasi ya nane kwa pointi zao 28 wakati Newcastle waliowafunga Everton 3-2 wamepanda hadi nafasi ya tisa wakiwa na pointi 26.
Liverpool wameshushwa hadi nafasi ya 10 wakiwa na pointi 25 sawa na Stoke wanaowafuatia. Stoke waliwapiga West Bromwich Albion 2-0 wikiendi hii.

Everton wamebaki nafasi ya 12 kwa pointi 21 sawa na Aston Villa waliocheza na Sunderland na kwenda suluhu. Sunderland wanafuatia kwa pointi 20.

Queen Park Rangers (QPR) wamezidi kujikomboa, kwani wamepanda hadi nafasi ya 15 baada ya kwenda suluhu na Crystal Palace. West Brom wameangushwa hadi nafasi ya 16 kwa pointi zao 17.
Wanafuatiwa na Hull, Palace na Burnley – wote wakiwa na pointi 16. Hull walikwenda suluhu na Leicester wikiendi hii. Leicester ndio wapo mkiani.

Chelsea wanaongoza kwa uwiano mzuri zaidi wa mabao 27, Spurs wakiwa na sifuri, Burnley wakigonga -15 huku Leicester wakiwa na -14.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ligi Kuu yachanua Krismasi

JE MAKOCHA NA FEDHA NDIYO TEGEMEO KUU LA USHINDI ?