Katika nchi ya England ambayo ndio yenye ligi kubwa na maarufu kuliko zote duniani zaidi ya asilimia 60 ya vilabu vya ligi hiyo kwa sasa vinamilikiwa na raia wa mataifa ya kigeni..
Soka la Tanzania kwa sasa limekuwa kubwa. Timu ya taifa ya Tanzania imeanza kuzoea kushiriki mashindano ya kimataifa. Hivi majuzi ilikuwa imetoka kushiriki mashindano ya AFCON yaliyokuwa yanafanyika nchini Ivory Coast. Licha ya kwamba ilitolewa kwenye hatua za makundi lakini ushiriki wake ilitangaza nchi kwani kwa mujibu wa takwimu ambazo zilizotolewa hivi karibuni na raisi wa shirikisho la soka la barani afrika Dokta Patrice Motsepe zinaonyesha kwamba mashindano hayo yaliangaliwa na watazamaji karibia bilioni 2 kutokana na vituo mbalimbali ambavyo viliomba haki za kurusha matangazo ya mashindano hayo. Tanzania ilinufaika kwa kuonekana katika mashindano hayo kwani ligi yetu nayo imetajwa huko kutokana na wacheaji walioshiriki kutoka vilabu mbalimbali hapa nchini.
Katika nchi ya England ambayo ndio yenye ligi kubwa na maarufu kuliko zote duniani Zaidi ya asilimia 60 ya vilabu vya ligi hiyo kwa sasa vinamilikiwa na raia wa mataifa ya kigeni ambao waliamua kuwekeza katika taifa hilo kwa kununua vilabu hivyo. Uwekezaji mkubwa wa kigeni katika ligi ya England ulianza pale mnamo mwaka 2003 ambapo Tajiri kutoka urusi bwana Roman Abramovich alipoinunua klabu ya Chelsea kutoka kwa Tajiri wa kiingereza bwana Ken Bates ambapo uwekezaji huo uliifanya klabu hiyo kuweza kununua wachezaji wa daraja la dunia na hatimaye kuweza kuchukua makocha wa daraja la dunia na kuweza kubeba ubingwa wa ligi ya uingereza na hata kufikia hatua ya kuweza kubeba ubingwa wa klabu bingwa ulaya na kombe la ligi ya Europa
Uwekezaji wa kigeni umekuwa ni mkubwa sana na vilabu vingine halidhalika navyo vimepata uwekezaji wa kigeni mfano: Arsenal inamilikiwa na bilionea Stan Kroenke ambaye anayokea taifa la Marekani.Aston Villa inamilikuwa na bilionea kutoka ardhi ya misri anayefahamika kama Nasser Sawiris. Bournemouth inamilikiwa na bilionea William Foley ambaye anatokea nchini Marekani. Burnely inamilikiwa na bilionea Alan Pace ambaye anatokea nchini Marekani. Fulham inamilikiwa na Bilionea Shahid Khan ambaye anatokea katika nchi ya Pakistan.Liverpool inamilikiwa na Fenway sports group ambayo inatokea nchi ya Marekani. Manchester city inamilikiwa na kampuni ya Abu Dhabi United group ambayo inatokea katika nchi ya falme za kiarabu.Newcastle inamilikiwa na mamlaka ya uwekezaji ya umma ya kutoka nchini Saudi Arabia.Nottingham Forest inamilikiwa na bilionea kutoka katika ardhi ya nchi ya Ugiriki ajulikanaye kama Evangeles maireny.Wolverhampton wanderers inamilikiwa na kampuni ya Fosun International ya kutoka nchini china. Manchester United inamilikiwa na familia ya kitajiri ya Glazer ambayo inatoka nchini marekani. Chelsea inamilikiwa na bilionea wa kimarekani Todd Boehly ambaye aliinunua kutoka kwa Abramovich.
Ligi ya italia nayo haiko nyuma kwani nayo imeanza kupata mitaji mikubwa kutoka kwa wawekezaji mbalimbali wan je ya nchi hiyo ambayo wameanza kununua vilabu na kuviendesha. Mpaka sasa vilabu 6 tayari viko chini ya umiliki na usimamizi wa wawekezaji kutoka nje ya nchi ya Italia. Klabu ya Fiorentina inamilikiwa na kampuni ya Rocco Commisso kutoka nchini Marekani. Klabu kongwe ya Ac Milan inamilikiwa na kampuni ya kigeni ya Red Bird capital Panthers. Klabu ya As Roma nayo haijawa nyuma kwani imenunuliwa na bilionea wa kimarekani Dan Friedkin. Klabu pacha ya jiji la Milan nayo halikadhalika imenunuliwa na familia ya kibilionea kutoka nchini China ya Zhang. Uwekezaji wa kigeni umeanza kuzaa matunda kwani vilabu hivyo vya italia navyo vimeanza kusajili wachezaji wakubwa ambao umevifanya vianze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataiga ambapo As Roma imeweza kubeba ubingwa wa kombe la UEFA Conference cup na halikadhalika katika msimu uliofuatia iliweza kufika fainali ya kombe la Europa na kujikuta inafungwa na timu ya kutoka uingereza ya West Ham United. Inter Milan imeweza kubeba taji la ligi ya italia na kufika katika hatua nzuri katika mashindano ya kimataifa ya ulaya. Ac milan nayo imefufuka kwani imeweza kuchukua ubingwa wa ligi ya italia na imeonyesha ushindani katika mashindano ya ulaya baada ya uwekezaji wa kigeni kufanyika.
Ligi ya Ufaransa nayo ilinufaika baada ya kupata uwekezaji wa kigeni kutoka kwa kampuni ya uarabuni ambako ukaifanya klabu hiyo iwe ni moja ya klabu yenye nembo kubwa barani ulaya. PSG ikaweza kufanya usajili wa mastaa mbalimbali kwenda kuchezea katika klabu hiyo ikiwemo Neymar, Mbape, Messi, Verratti na kadhalika. Kalbi hiyo ilifanikiwa hadi kucheza fainali ya klabu bingwa ulaya licha ya kwamba iliukosa lakini uwekezaji umeiongezea thamani klabu hiyo.
Uwekezaji kutoka ne ulifanya ligi ya uingereza kuzidi kuwa ya msisimko na yenye kufanya watazamji kuwa na hamu nayo. Mnamo mwaka 2015 Dunia ya soka ilishangazwa pale ambapo klabu ya Leicester City ilipoibuka bingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuzipiga timu zote kubwa ambazo zilikuwepo kwa nyakati hizo. Hata mwaka huu pale nchini Uhispania nako kuna mashabiki wanashangazwa na namna klabu ndogo ya soka ya Girona inavyowashangaza mashabiki baada ya kufika kuwa kwenye hatua ya tatu za juu katika msimamo wa ligi hiyo na huku dalili zinaonyesha kwamba ina nafasi kubwa kupanda na kwenda kucheza klabu bingwa ya ulaya kwa msimu ujao. Na Girona isingeweza kufanya hivyo ila imeweza baada ya kupata uwekezaji kutoka nje.
Ligi yetu ya Tanzania inajitosheleza kupata uwekezaji kutoka nje kwani ina mashabiki wa kutosha tofauti na ligi zingine barani Afrika. Ifike hatua matajiri wakubwa wan je waje kununua vilabu hata vile vidogo vilivyopo katika ligi kuu ili navyo viweze kuendeshwa kisiasa na kibiashara na hatimaye vilete ushindani barani afrika. Kazi hii isiwe ya vilabu peke yao bali mamlaka za soka zishirikiane na serikali kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa. Inatakiwa ifike hatua kituo cha uwekezaji Tanzania nacho kishughulike na kutafuta wawekezaji kwa ajili ya vilabu na pindi wakija wawekezaji kutafuta miradi ya kuwekeza basi waonyeshwe kwamba wanaweza kuwekeza kwenye vilabu hivyo. Huu mkakati unatakiwa uwe wa miaka mingi na utekelezwaji wake uwe wa ubia baina ya sekta binafsi na serikali.
Comments
Loading…