Menu
in , , , ,

Vilabu vifanye usajili makini sasa

Taifa Stars

Taifa Stars

KIPINDI cha usajili kinapofunguliwa tunasikia mipango na kelele nyingi kutoka kwa wanahabari, viongozi wa klabu, mashabiki na wadau wa michezo. Kila timu inasikika kumfuatilia mchezaji wa aina fulani ili asajiliwe kwenye timu zao. Kuna makocha wanaotaka wachezaji  wa kiungo, washambuliaji, mabeki na mawinga. Kila kocha anakuwa amewasilisha mapendekezo yake kwa uongozi ili kuangalia namna ya kupata wachezaji wenye viwnago bora zaidi. 

Kipindi cha usajili kinatawaliwa na tetesi nyingi huku baadhi zikitimia na zingine zinabaki kuwa simulizi za kusadikika. Makocha wanalumbana na viongozi huko ndani na wengine wanataka kuona wachezaji wanaowapenda  wanasajiliwa. Kuna muda mashabiki wanataka mchezaji fulani asajiliwe hata kama klabu yao haina uwezo w akulipia ada ya uhamisho. 

Hili halitokeo katika Ligi Kuu Tanzania peke yake. sehemu nyingi duniani wapo wachezaji wanaouzwa lakini baadhi yua klabu zinashindwa kununua sababu ya dau kubwa. Wapo wachezaji wanaowindwa sana lakini wanakataa kujiunga na timu inawahitaji au wanakosa ari ya kuhamia timu mpya kwa sababu inaonekana haina jambo linalovutia. Kwa mfano mchezaji akitakiwa na Yanga au Simba maana yake anayo fursa ya kulipwa mshahara mnono, kushiriki mashindano ya Kimataifa, uhakika wa kutwaa kombe na marupurupu kadhaa. Kwahiyo inakuwa fursa kwake kuchagua timu hizo. 

Barani Ulaya nako hali inakuwa hiyo hiyo, wachezaji wanawatuma mawakala wao kudai mishahara minono na malipo ya kufuru. Pia klabu zenyewe zinamhitaji mchezaji kiasi kwamba zinakuwa tayari kuvunja rekodi zao za usajili. Hii ina maana klabu husika inatakiwa kujipukuta kwenye akaunti zake za benki kuhakikisha wanafikia dau linalotakiwa na timu zinazomuuza mchezaji husika.

Hapa Ligi Kuu Tanzania msimu uliopita tumesikia malalamiko mengi kutokakwa timu mbalimbali. Ligi Kuu ilitawaliwa na malalmishi kutokana na uamuzi mbovu wa Marefa. Lakini pia malalamiko yalikuwa dhidi ya baadhi ya wachezaji wa klabu husika, kiasi kwamba kocha mmoja amewahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema golikipa wake alifungwa mabao ya kitoto kana kwamba alikuwa amelipwa hongo ili kuruhusu mabao hayo. 

Kocha huyo ni kielelezo cha namna dirisha la usajili linavyokuwa muhimu. kipindi cha usajili ndicho benchi la ufundi linatarajia kupokea wachezaji wapya ambao wametokana na mapendekezo yao. kwahiyo uongozi unaposajili golikipa ambaye anaaminika kuwa na kiwango bora bila shaka anakuwa mchezaji wa kutumainiwa na kumpa kocha kiwango bora. 

Kama golikipa amefungwa mabao ya hovyo, maana yake kocha alikuwa ameruhusu uongozi kusajili mchezaji ambaye hana kiwango cha kuchezea timu yake. kama mchezaji anakuwa na kiwnago duni maana yake kocha anatakiwa kumwimarisha na kuwa bora au azungumze ne na uongozi kuhusiana na uwezo wa mchezaji husika. 

Makocha na viongozi wa vilabu wanapokosa ushirikiana katika kipindi cha usajili matokeo yake ni pale Ligi Kuu inaponguruma na timu ikazabwa mechi kadhaa, ndipo lawama zinapoibuliwa. 

Wengine wanalalamikia maamuzi mabovu ya marefa, wengine wanalalamikia vianja vya kuchezea, wengine wanalalamikia uwezo mdogo wa wachezaji na kadhalika. 

Hapa ndipo TANZANISPOSRTS inawakumnbusha wadau wa soka kipindi cha usajili ni muhimu sana kuimarisha timu. Ni kipindi ambacho benchi la ufundi na uongozi wa klabu wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuepusha migogoro na malumbano wakati Ligi itakapoendelea kitimua vumbi. Soka ni mchezo wa wazi na kila mmoja anaona kinachotokea. Kama timu imesajili mchezaji ambaye hawezi kuwapa ufanisi timu yao, ni jukumu la uongozi kubeba lawama. 

Kipindi cha usajili ni kile kinacholeta matokeo ya uchunguzi wa aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na nafasi ya kuimarisha. 

Kipindi cha usajili sio cha kuanza kutafuta wachezaji bali kutekeleza mipango ya mchezaji wa kusajiliwa ambaye amechunguzwa kwa kipindi kirefu. Benchi la ufundi na viongozi wa klabu wanatakiwa kuwachunguza wachezaji wanaopenda kuwasajili katika klabu zao, kwahiyo suala la kusubiri kipindi cha usajili ndipo waanze kuwachunguza ni chanzo cha matatizo. Ni wakati ambao viongozi wanatakiwa kukubali kuwa benchi la ufundi linapaswa kuwatajia majina ya wachezaji ambao wanatamani wangejiunga na timu yao.

Kama benchi la ufundi linapendekeza nafasi muhimu halafu uongozi ukafanya tofauti kwa sababu za uzembe na usajili wa mapenzi badala ya uwezo, bila shaka tutaendelea kushuhudia malalamiko msimu ujao. Malalamiko hayo yanatokana na udhaifu wetu wa kusimamia mipango ya klabu ili kuwezesha timu kufanya vizuri kwenye Ligi. 

Katika kipindi cha usajili pia kinatakiwa kuleta matokeo ya kuongeza udhamini ambapo viongozi wanawajibika kusaka vyanzo zaidi vya mapato ili kuongeza ufanisi wa idara za timu husika. hatutarajii kuona malalamiko ya makocha eti mchezaji fulani hana kiwnago ilhali wlaimsajili wenyewe.

Mwisho TANZANIASPORTS inawakumbusha wadau kuwa suala la kusajili mchezaji wa kiongozi fulani au kibopa fulani ni chanzo cha kuwa na kundi kubwa la wachezaji ambao hawawajibiki kwa uongozi au benchi la ufundi bali kwa mtu anayemmiliki. 

Mchezaji wa aina hiyo mara nyingi anakuwa hawajibiki ipasavyo kwa sababu anafahamu kuna kinga itakayomlinda endapo mambo yatakwenda kombo. Kwa wachezaji pia, kuwa mchezaji wa kiongozi fulani bila kucheza kw aufanisi ni ishara kuwa hana maadili kwa kazi yake inayompa chakula, mavazi, na nguvu ya uchumi na maendeleo binafsi.

Ni jukumu la benchi la ufundi kuhakikisha wachezaji wanaokuja ni wale wanaoingia kwneye mfiumo yao, sio kuwaambia mashabiki eti hayupo kwenye mfumo huku analipwa mamilioni ya shilingi kama mshahara.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version