in

Vikwazo kurejea EPL

Wakati Ligi Kuu ya England (EPL) ikitarajiwa kurejea tena Juni 17, inaonekana kwamba kuna vikwazo kadhaa.

Inaanza kwa ajili ya kumalizia mechi 92 zilizobaki, ambapo watu 300 tu wataruhusiwa kuingia kwenye kila uwanja katika mechi, huku watazamaji wakiwa hawatakiwi bali watatazama mechi kutoka majumbani mwao.

Kutokana na kupigika na virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, klabu zimeathirika na wachezaji kadhalika, hivyo mechi zinapoanza klabu hasa zilizo kwenye uzio wa kushuka daraja zinataka kusiwe na kushuka daraja msimu huu kwa sababu mazingira si mazuri na haki haitakuwa imetendeka.

Hata hivyo, Chama cha Soka (FA) cha England kimeweka wazi kwamba hakikubaliani na ombi la timu kutoshuka, kwa sababu kwenye Ligi Daraja la Kwanza (Championship) kuna timu tatu zinatakiwa kupanda kama ambavyo tatu zinatakiwa kushuka kutoka huko juu.

Jambo jingine linalowachanganya klabu ni kule kuambiwa kwamba watapoteza kati ya £300m na £350m katika mapato ya matangazo ya televisheni, hata kama wataweza kumaliza msimu. Hii ni kwa sababu hawataweza kutekeleza Baadhi ya matakwa ya kwenye mikataba waliyosaini.

Pamekuwapo mapendekezo kwamba kima hicho kijadiliwe na kisiwe ndio uamuzi wa mwisho, lakini watangazaji wanasema kwamba ikiwa msimu hautamalizika mapema kutakuwapo na penati zaidi, hata kama zitalipwa kwa malimbikizo.

Klabu zitatakiwa kutia saini mapendekezo husika ili kuhakikisha kwamba watangazaji wanaweza kuingia uwanjani kwa ajili ya kupiga picha na kurusha, lakini inaonekana kwamba itakuwa ngumu kuruhusiwa kuingia kwenye vyumba vya kubadili nguo kwa sababu ya haja ya watu kutakiwa kujitenga kwa kadiri inavyowezekana.

Kadhalika kuna tatizo kwenye usajili wa vikosi na mikataba ya wachezaji. Klabu zinajadili na huenda wakapiga kura juu ya iwapo wataruhusiwa kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi na kuondolewa kwenye vikosi vya wachezaji 25 kwa kila timu ili kuongeza idadi ya wachezaji kwa kila kikosi kwa vile mechi zitachezwa karibu karibu.

Mfano mmojawapo ni Paul Dummett wa Newcastle aliyepata tatizo la misuli ya paja Januari na kuwekwa nje ya kikosi cha kwanza lakini sasa yu timamu. Dummett anasema kwamba matarajio ni kwamba baadhi ya kanuni zitasitishwa walau kwa muda ili kuhakikisha kila timu inakuwa na kikosi kipana. Klabu zimepewa muda hadi Juni 23 kwa ajili ya kukubaliana na nyongeza ya mikataba ya wachezaji ambao muda wao ungemalizika Juni 30 mwaka huu.

Mechi nyingi zitachezwa katika muda mfupi ligi itakaporejea ili kuhakikisha msimu unamalizika mapema, wachezaji wapate muda wa kupumzika, klabu zijiandae kwa usajili na kuanza kwa msimu mpya.

Mechi zitakuwa zinachezwa kila wikiendi na katikati ya wiki lakini katika mjadala mezani ni ama klabu kuendelea na mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini au zichezwe kwenye viwanja huru ili kuwezesha kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, hasa kwa klabu zilizo karibu zaidi na makazi ya watu.

Suala hili limekuwa mezani kwa wiki kadhaa sasa, klabu zikitaka mfumo wa nyumbani na ugenini uendelee lakini polisi wameendelea kuonya dhidi ya hali hiyo, wakisema kwamba wana hofu kwamba washabiki watakusanyika nje ya viwanja husika.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Hassan Mwakinyo

Plaza kwa Tyson, PTA kwa Matumla, Mwakinyo je?

mchezo wa soka, mahasimu wakiwa uwanjani

Utata wa sheria namba 11 ya soka Duniani