in , , , ,

Vijana wa Mourinho ndani ya robo fainali CHAN

IPO picha moja inayowaonesha vijana wawili wa Harambee Stars wakicheka kwa furaha huku wameshikana mikono. Wote wamevalia mavazi meusi na shingoni wamening’niza kamba za vitambulisho. Kwenye picha hiyo kuna vijana ambao walicheza chini ya Jose Mourinho kwa umahiri na kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ni vijana ambao sasa wameungana kuipendezesha Harambee Stars.

Wakati fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani, zimetamatika katika hatua ya makundi, vijana hawa wawili wanazidi kuwa gumzo kwenye tasnia ya habari na uchambuzi wa michezo. 

Mashindano ya CHAN sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali, ambapo wenyeji wa mashindano hayo Kenya, Uganda na Tanzania zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kuandika rekodi ya aina yake. nchi hizo hazijawahi kufika hatua kama hiyo kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF katika ngazi ya timu za Taifa za wakubwa. Tanzania ilimaliza kundi lake ikiwa kinara, sambamba na Kenya na Uganda ambazo zimewatoa jasho wapinzani wao. 

Miongoni mwa kivutio kikubwa cha mashindano haya ni vijana wa kocha Jose Mourinho. Sifa za kocha Jose Mourinho ni kubwa na amekuwa kipenzi cha wachezaji kutoka Bara la Afrika. Mourinho alianza kazi akiwa timu ya Barcelona ngazi za chini, kabla ya kwenda kwao nchini Ureno kuchukua jukumu la kuwa kocha mkuu. 

Tanzania Sports
Ben McCarthy, Kocha Mkuu Wa Harambee Stars

Miaka michache baadaye alikabidhiwa kazi ya ukocha katika klabu ya FC Porto. Akiwa kwenye kikosi cha Porto, Mourinho alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo katika mchezo wa nusu fainali alimtupa nje ya mashindano kocha mahiri kabisa duniani na Manchester United, Sir Alexc Ferguson. 

Porto walikuwa timu yenye makali makubwa chini ya viungo kama Deco, Alberto Carlos na mwingine alikuwa Ben McCarthy aliyeongoza safu ya ushambuliaji. Nyota huyo wa Afrika Kusini alikuwa chipukizi aliyetamba kwenye mashindano ya AFCON yaliyofanyika nchini Burkina Faso. 

Ben McCarthy alikuwa nyota aliyevutia timu nyingi kwa upachikaji wake wa mabao, kasi, chenga na uwezo wa kucheza kama mshambuliaji pekee (lone striker). Hakuwa mchezaji mwenye mambo mengi katika timu, lakini kazi yake ilimtambulisha kwa makocha wengi. FC Porto ilikuwa miongoni mwa timu zilizovutiwa na kiwango cha Ben McCarthy na hawakusubiri sana walilipa ada na kumhamishia nchini Ureno. 

Ben akiwa chini ya kocha Josep Mourinho aliandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kusini kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ndani ya kikosi cha Porto, Ben McCarthy alikuwa panga pangua. Mourinho alipotaka kucheza mbinu za kujihami, basi nambari 9 alipewa Ben. 

Mourinho alipotaka kubadili mfumo mafno kucheza 4-4-2 bado alimfanya Ben kuwa mshambuliaji wake wa kutumainiwa. Upachikaji wa mabao, kujitolea zaidi ya kile anachokihitaji kocha ni miongoni mwa sifa zilizomfanya awe mshambuliaji wa kuogopeka katika soka wakati wa uchezaji wake. lakini sasa Ben McCarthy ndiye kocha wa timu ya Taifa ya Kenya, maarufu kama Harambee Stars. Akiwa katika kikosi hicho amekutana na kijana mwingine wa Jose Mourinho. 

Huyu si mwingine ni McDonald Mariga staa maarufu wa Harambee Stars na miongoni mwa wachezaji wa Kikenya waliofanikiwa kupenya katika soka la Ulaya. McDonald Mariga alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Kenya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010 akiwa klabu ya Inter Milan chini ya kocha Jose Mourinho. Nyota huyu alikuwa anamudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji. Hii ni nafasi ya wachezaji ambao wanafanya kazi chafu kama ya Yusuf Kagoma wa Taifa Stars ama lile jitu la kutisha la Italia, Genaro Gattuso. 

Nafasi aliyocheza McDonald Mariga ni ile ambayo huitwa ‘injini’ yaani yeye ndiye anakuwa roho ya timu kwa kuhakikisha walinzi wanalindwa na viungo washambuliaji wanafanya kazi zao bila usumbufu wa kutafuta mpira kwa tochi. Kazi ya Mariga ilikuwa kuhakikisha anawadhibiti wapinzani wao wanaotaka kuliandama lango lao, na kwamba alikuwa ndiye mlinzi wa walinzi. 

Kimo chake, misuli, uwezo wa kutumikia nafasi ya kiungo na kipaji chake vilimfanya awe nyota wa Harambee Stars mwenye ujuzi wa kufanya kazi chafu ndani ya dimba. Katika kikosi cha Inter Milan alikuwa nyota anayeingia kwenda kukamilisha kazi ya kuwadhibiti wapinzani. Kazi yake ilikuwa kusafisha uchafu wote kwenye eneo la namba 6. Alikuwa na mapafu ya mbwa. Mchezaji ambaye hachoki, na huwezi kumshinda kwa matumizi ya nguvu za mwili. 

McDoland Mariga na Ben McCarthy ndiyo wanaliongoza benchi la ufundi la Kenya katika mashindano ya CHAN. Nyota hawa wanatoa ufundi na uzoefu wao wa kucheza soka kwa kiwango cha juu ya ushindani mkali barani Ulaya na hivyo wanahamishia kwa Harambee Stars.

Jinsi Harembee Stars wanavyocheza, ni dhahiri unagundua kuwa makocha hawa McDonald Mariga na Ben McCarthy wlaililewa vyema somo la kocha wao Jose Mourinho. Linapofika suala la kujilinda Harambee Stars wamekuwa kama ukuta wa Berlin. Wanajua kukaba, kuziba nafasi, kucheza nguvu-kazi na zaidi kuhakikisha jambo lao linatimia. Harambee Stars wamecheza mechi mbili mfululizo wakiwa pungufu uwanjani kwa dakika kama 70 lakini walifanikiwa kuondoka na alama tatu. Licha ya kuwa pungufu hawakuonesha kuathiriwa na hali hiyo. Harambee Stars wanacheza kwa ari na kujituma kwa sababu wapo chini ya makocha ambao wanajua namna ya kutumia mbinu za mwalimu wao wa zamani Jose Mourinho. Hawa ndiyo vijana wa Jose Mourinho kwenye mashindano ya CHAN yanayoendelea hapa Afrika Mashariki.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Jinsi Simba wanayotaka magoli ya CAF

Taifa Stars

Vilio Tanzania, Kenya zikitolewa CHAN