in

Simba wapata mkataba udhamini 20bn/-

KLABU ya Simba imesaini dili na 20bn/- mdhamini Mkuu BetWay baada ya M-Bet kusitisha Mkataba wake.

 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC, Zubeda Sakuru, ametangaza udhamini mpya wa Bilioni 20 kutoka Kampuni ya Betway kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa maana hiyo, Simba SC wameingia rasmi mkataba huu unaomfanya Betway kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Udhamini huo mpya unakuja baada ya Simba kuachana na aliyekuwa mdhamini wake mkuu, kampuni ya M-Bet ambapo mwaka 2023, waliingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya 26.1bn/-.

“Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika.”

“Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,” alisema.

“Kazi yetu ni kuhakikisha brand yetu ya Simba SC inazidi kukua siku hadi siku, mpira una gharama nyingi timu inahitaji fedha, mashabiki wetu tuwaunge mkono Betway ambao ni wadhamini wetu.”

Jimmy Masaoe ambaye ni Meneja Uendeshaji wa BetWay Tanzania, alikuwa na haya ya kusema: “BetWay ni kampuni ya kimataifa na yenye uwezo wa kupokea watu wapya hata wakiwa wengi lakini pia tuna huduma kwa wateja ambayo ipo muda wote kuwahudumia.”

“Mashabiki wategemee huduma bora kutoka kwetu, tumejipanga. Lakini pia kutakuwa na huduma mbalimbali ambazo tumezibuni kwa ajili ya mashabiki wa Simba.”

Jason Shield – Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika naye alikuwa na yake: “Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili.

“Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili.

“Nina furaha kwa ushirikiano huu lakini tutafanya kazi kuangalia namna gani ya kufanikisha ushirikiano na vilabu vingine vikubwa ambavyo tunashirikiana navyo.”

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani aliwapongeza Simba kwa hatua hiyo kubwa, akisema kwamba ni tukio ambalo kila siku TFF wamekuwa waikiliimba, na kwamba ni hatua kubwa.

“Sisi TFF tunasisitiza kila upande uhakikishe unatimiza wajibu wake. Lakini mafanikio haya ya kupata udhamini mkubwa yanatokana na ubora wa ligi yetu sababu inaendelea kuimarika kila siku. Wito wetu sisi ni uwazi kwenye matumizi ya pesa zinazotolewa na wadhamini maana utatusaidia kuaminika na wadhamini,” alisema Nyamlani.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Nilipokuwa nachambua Michezo kupitia BBC

Vyeti sio ‘kila kitu’ kwenye uandishi na utangazaji

Bayern wamnyakua Diaz wa Liverpool

Bayern wamnyakua Diaz wa Liverpool