in , , ,

Van Gaal: Spurs ningefanikiwa zaidi

*Huyu jamaa ana kauli tata sana!

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anasema kwamba ingekwua kazi rahisi zaidi kwake kama angeamua kukubali mkataba wa kuwanoa Tottenham Hotspur badala ya Manchester United aliko sasa.

Kocha huyo aliyeanza vibaya Ligi Kuu ya England na pia kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi na timu ya daraja la tatu, Milton Keyness Dons, maarufu kama MK Dons, anasema kazi ya United ni ngumu.

Baada ya kufungwa mechi moja na kwenda sare mbili na timu ambazo watu waliona ni dhaifu, Mdachi huyo anasema bado sana mambo ya Man U kukaa sawa, akisema kikosi hakikuwa na morali wala kujiamini.

Hata hivyo, Van Gaal amesajili wachezaji wazuri msimu huu na washabiki wanatarajia makubwa, ingawa wamekasirishwa na Danny Welbeck kwenda Arsenal, wakisema kwamba klabu inapoteza utambulisho wake, kwani Welbeck amezaliwa Manchester na amekuwa na klabu tangu akiwa na umri wa miaka minane.

Van Gaal aliitiwa kazi Spurs ambao walimfukuza kazi Andre Villas-Boas lakini pia wakaachana na mrithi wake, Tim Sherwood, lakini Van Gaal aliyekuwa akiwanoa Timu ya Taifa ya Uholanzi akakataa kazi hiyo akatinga Old Trafford.

“Hata hivyo sijutii kuikubali kazi hii. Ni kubwa na nzito. Nafahamu fika na hali ni mbaya kama nilivyokuwa nimefikiria awali. Ningeweza kuchukua kazi rahisi zaidi. Kama ningeenda Spurs kazi haingekuwa ngumu kama ilivyo hapa United,” anasema Van Gaal.

Hadi sasa United wamechukua pointi mbili tu kati ya tisa ambazo wangeweza iwapo wangeshinda mechi zao, na sasa akiwa na kikosi kipya, Van Gaal atatafuta ushindi wake wa kwanza katika mechi ya ushindani tangu ajiunge hapo.

Washabiki wameshaanza kukasirika, lakini wamepozwa na usajili mzuri wa watu kama Angel Di Maria, Radamel Falcao, Marcos Rojo, Luke Shaw, Andre Herera na wana imani kwamba baada ya mapumziko yanayopisha mechi za kimataifa, watafanya vizuri.

Van Gaal amechukua nafasi ya David Moyes ambaye alibatizwa jina la ‘The Chosen One’ kabla ya kukataliwa na washabiki waliotaka aondoke hadi wakakodi ndege iliyochora angani maneno ya kutaka afukuzwe, ikaruka juu ya dimba la Old Trafford.

“Ningeweza kwenda Spurs kirahisi kabisa, lakini nikaamua kukabiliana na changamoto ambayo ni kubwa zaidi kwenye soka. Na kweli nilitaka kujiunga na klabu namba moja nchini, si Tottenham. Kifedha, Tottenham walinivutia sawa na Man United, lakini machoni mwangu Man United bado ni klabu namba moja England, Spurs sio,” anasema Van Gaal.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Welbeck aliota ataingia Arsenal

England wawafunga Norway kwa tabu