in , , ,

UCHAMBUZI WA BAADHI YA MECHI ZA LIGI KUU YA ENGLAND

LIVERPOOL vs MANCHESTER UNITED.

Kitu pekee ambacho kinaongelewa sana na Jose Mourinho kucheza mchezo
wa kujizuia kwa muda mrefu.

Kitu hiki kiliwapa shida sana Liverpool kwa sababu hawakuweza kupata
nafasi za kupitishia mpira.

Manchester United walihakikisha nafasi za kupitishia zinakuwa haziko
wazi ili kuwanyima nafasi Liverpool kutengeneza nafasi nyingi.

Liverpool walicheza kwa kiasi kikubwa mchezo wa wazi , walionekana
wana nia ya dhati ya kutafuta goli ndiyo maana walifunguka muda mwingi
wa uwanja kutafuta magoli.

Kitu pekee ambacho kiliwagharimu kwa kiasi kikubwa ni kutokuwa na
Mshambuliaji halisi wa kati ambaye anauwezo mzuri wa kufunga.

Salaha amekuwa akipoteza nafasi nyingi za wazi na pia amekuwa hawezi
kutoa pasi za mwisho kwa uharaka zaidi.

Firmino hakuwa na uwezo mkubwa wa kuipita ngome ya Manchester United
kwa sababu alihitaji akili ya ziada ya mshambuliaji halisi wa kati.

Manchester United walishindwa kufanya kitu kimoja kwao, kuzuia ni
sanaa moja wapo kwenye mpira.

Na haikatazwi timu kutumia sanaa ya kuzuia, lakini kitu cha muhimu kwa
kocha ni kujiuliza timu inapataje uwezo wa kupata goli wakati ikiwa
inatumia sanaa ya kuzuia kwa asilimia kubwa?

Kwa kuwa Liverpool muda mwingi walitumia kucheza mpira wa wazi, mpira
ambao ungewapa nafasi Manchester United na wao kushambulia kwa kutumia
mashambulizi ya kushtukiza.

Lakini hawakuweza kufanya hivo na ndiyo maana ilikuwa ngumu kwao
kupata goli ambalo lingewasaidia kupata alama tatu.

WATFORD vs ARSENAL.

Kosa kubwa ambalo Arsene Wenger alianza kulifanya ni kuwaanzisha Xhaka
na Elney pamoja katika kiungo cha kati.

Hapa ndipo Arsenal ilianza kujiwekea wakati mgumu katika mchezo huu
kwa sababu unapokuwa na viungo wa aina ya Xhaka na Elney kwa wakati
mmoja timu yako inakuwa na vitu vifuatavyo.

Moja, timu inakuwa haina kiungo wa kulazimisha pasi za mbele, timu
inakuwa na pasi nyingi ambazo ni square passes ambapo kimsingi
zinakuwa hazina faida yoyote.

Hivo timu inakosa ubunifu kuanzia katika eneo la kati.

Pili, nafasi chache zinakuwa zinatengenezwa na timu husika kwa sababu
ya kiungo kutokuwa na ubunifu.

Unapokuwa unatengeneza nafasi chache unakuwa na asilimia chache za
kupata magoli hasa hasa kwenye timu ambayo ina ulinzi mzuri kama
Watford.

Marco Silva , alifanya jambo la msingi kumwingiza Deeleney kwa sababu
Watford ilianza kucheza mpira wa moja kwa moja ( direct football) ,
aina hii ya mpira imekuwa ikiwasumbua Arsenal kwa muda mrefu sana.

MANCHESTER CITY vs STOKE CITY.

Kitu kikubwa kwa Manchester City ni namna ambavyo Pep Guardiola
ameifanya timu nzima ihusike katika mashambulizi.

Ndiyo maana ni vyepesi kuona watu kama kina Walker wanahusika katika
ufungaji wa magoli kwa Manchester City.

Timu nzima inahusika kushambulia. Na kitu cha muhimu ni kwamba
Manchester City ina viungo wabunifu kama David Silva pamoja na mwenye
timu Kevin De Bryune. Kevin amekuwa akiongoza ubunifu wa mashambulizi
ya Manchester City kwa wakati wote.

CHELSEA vs CRYSTAL PALACE.

Kitu pekee ambacho kilicho waangusha Chelsea ni idadi kubwa ya majeraha
kwa wachezaji muhimu wa kikosi cha Chelsea.

Kukosekana kwa Ng’olo Kante pamoja na mfungaji bora wa kikosi kwa
msimu huu ( Alvaro Morata ) kulikuwa ni pengo kubwa sana kwao.

Ukiachana na kwamba Kante amekuwa muhimu zaidi katika eneo la kuzuia
la kiungo cha Chelsea, pia Ng’olo Kante amekuwa akihusika kwa kiasi
kikubwa kuifanya timu ishambulie kwa kutumia njia zipi ( maeneo
gani).

Katika mchezo huu hakukuwa na mtu ambaye angeifanya Chelsea icheze
katika maeneo yote ya uwanja .

Pia Mshambuliaji wa kuibeba timu hawakuwa naye kwa sababu Morata
alikuwa katika majeraha.

Palace wanapata ushindi wao wa kwanza msimu huu tena katika London
derby dhidi ya bingwa mtetezi.

Hii itawapa wao nguvu katika kupigana kutokushuka daraja.

Zaha alikuwa mchezaji muhimu katika mchezo huu kwani kwa kiasi
kikubwa aliibeba timu yake katika ushindi huu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal: Kichapo stahiki kwa Arsène Wenger

Tanzania Sports

DERBY YA INTERMILAN NA MILAN IMEBAKI KWENYE VITABU