in , , ,

UBORA WA COUNTINHO UKO MAENEO GANI ?

Jana Barcelona wamefanikiwa kukamiliza vipimo vya Phillipe Countinho.

Hivo rasmi ni mchezaji wa Barcelona , anachosubiri ni kukabidhiwa
namba ya jezi atakayoivaa.

Yuko kwenye ardhi ambayo alitabiriwa na wengi kama gwiji wa zamani wa
Barcelona, Ronaldinho Gaucho.

Ronaldinho aliwahi kusema mtu pekee anayeweza kuziba pengo la Neymar
ni Phillipe Countinho.

Muda huu tayari Phillipe Countinho yupo sehemu ambayo alikuwa
anaitamani na wengi waliona ni sehemu sahihi ambayo itamfaa kucheza.

Ameshakuwa mchezaji wa Barcelona tayari. Je ataenda kucheza katika
mfumo ambao utamfaa ??

Barcelona msimuu huu wamecheza mifumo kadhaa kama 4-4-2, 4-3-3, 4-2-3-1.

Ndani ya mifumo hii Countinho atafanikiwa kuchezaje ?

4-3-3. Huu ni mfumo ambao unakuwa na mabeki wanne, viungo watatu wa
kati na washambuliaji watatu ambapo wawili watakuwa wanatokea pembeni
na mmoja kusimama kama mshambuliaji wa kati.

Katika mfumo huu Countinho anaweza kusimama kama mtu wa kuziba pengo
la Neymar. Kwa sababu anaweza akawa anacheza kama mshambuliaji
anayetokea pembeni kushoto kama ambavyo alivyokuwa anacheza Neymar.

Katika mfumo huu Phillipe Countinho kule mbele anauwezo wa kucheza
pamoja na Messi ambaye atacheza kama mshambuliaji wa pembeni akitokea
kulia, na Suarez atacheza kama mshambuliaji wa kati.

Kwenye huu mfumo pia, Countinho anaweza kutumika kama mtu wa kuziba
nafasi ya Iniesta.

Iniesta kwa sasa umri unakwenda, Phillipe Countinho anaonekana kama ni
mtu ambaye amekuja kwa ajili ya kumpumzisha Iniesta.

Hivo Phillipe Countinho anaweza akawa anacheza kwa kutokea katikati mwa uwanja.

Hivo kule mbele kuwapa nafasi Dembele, Suarez na Messi kucheza huku
yeye akicheza katikati akicheza na Sergio/Rakitic, Paulinho na yeye
mwenyewe.

Katika mfumo wa 4-4-2, iwe Flat au Diamond anaweza akacheza vizuri
akitokea pembeni kushoto.

4-2-3-1 hapa anaweza akacheza kwa kutokea katikati kushoto , mfumo huu
unaruhusu viungo wawili wa kati ambapo kwenye viungo hao wa kati
anaweza akacheza Sergio Bosquets na Iniesta huku kwa wachezaji watatu
watakaocheza mbele yao wanaweza kucheza Countinho ambaye atatokea
pembeni kushoto, Messi ambaye atatokea katikati na Dembele ambaye
atacheza pembeni kulia huku mshambuliaji wa mwisho akabaki kuwa
Suarez.

Baada ya kuangalia jinsi ambavyo Countinho anaweza kucheza vizuri
katika mfumo wa Barcelona, hebu tuangalie ubora wa Phillipe Countinho
uko wapi?

Uwezo wa kuona na kujitengenezea uwazi ndani ya uwanja.

Moja ya sifa ya Phillipe Countinho ni kukimbia na mpira, anapokuwa
anakimbia na mpira huwa anatoa pasi kwa wenzake na kujiweka sehemu
ambayo ina uwazi ili apokee tena mpira.

Uwezo huu wa kujitengenezea uwazi , huwa unampa nafasi ya kuonesha
madhara akiwa karibu na goli kwa sababu wakati anapotoa pasi na kwenda
sehemu ambayo ni wazi huwa anauwezo mkubwa wa kupiga mashuti ambayo
yana madhara.

Ubora mwingine wa Phillipe Countinho ni uwezo wake wa kutengeneza
muunganiko wa mashambulizi ndani ya timu.

Phillipe Countinho akiwa anacheza katikati ya uwanja, hushuka chini
kuchukua mpira na kuanzisha mashambulizi. Mpaka sasa Phillipe
Countinho ana take ons 39 ambazo ni nyingi kuzidi take ons za Iniesta
na Paulinho. Mchezaji pekee wa Barcelona anayemzidi Take ons ni Messi.

Pia, Phillipe Countinho ni mzuri katika ufungaji na kutoa pasi za
mwisho za magoli.

Barcelona haina tatizo la magoli lakini ujio wake utakuwa umeongeza
uzito katika magoli na upatikanaji wa magoli ( utengenezwaji wa
magoli).

Barcelona ina Messi ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza mipira iliyokufa
( mipira ya adhabu ndogo au free kick).

Phillipe Countinho ni mzuri sana eneo hili pia. Hivo anaingia kwenye
kikosi cha Barcelona kuongeza nguvu kwenye eneo hili.

Hivo, Ujio wa Phillipe Countinho umeonesha namna sahihi ambavyo
Barcelona walivyotakiwa kutumia pesa za Neymar kwa busara.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

WACHEZAJI WANAOFAA KUZIBA NAFASI YA PHILIPPE COUTINHO PALE LIVERPOOL

Tanzania Sports

KUNA HAJA YA LIGI KUU YA ENGLAND KUWA NA MAPUMZIKO