in , ,

Toure, Gervinho waibeba Ivory Coast

Bafana Bafana nje AFCON

*Tunisia waizamisha Algeria ‘jioni’

Washiriki wote 16 wa michezo ya 29 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) wameshuka dimbani.

Jumanne hii ilikuwa zamu ya timu za kundi ‘D’, Ivory Coast wakiumana na Togo, huku Algeria wakipepetana na Tunisia.

Yaya Toure wa Manchester United aliitanguliza Ivory Coast au Tembo kwa bao la kwanza dakika ya nane na Gervinho wa Arsenal akawahakikishia ushindi dakika ya 88.

Licha ya kuingia mchezoni wakipewa nafasi kubwa kushinda, Tembo hao walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia Chiriku wa Togo waliopigana kufa na kupona kurejea mchezoni baada ya kufungwa bao la kwanza.

Mshambuliaji wa Togo, Jonathan Ayite alisawazisha mambo mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Nusura Toure afunge bao la pili, lakini hata hivyo moja alilopata limemwekea historia kubwa, ikimaanisha kwamba amefunga mabao katika fainali nne za AFCON kati ya tano alizocheza.

Nyota ya mshambuliaji Emmanuel Adebayor haikung’ara sana kwenye mechi hiyo, kwani licha ya kuzawadiwa mpira kwa bahati mbaya na Toure, alishindwa kuufanyia maarifa kuupeleka wavuni.

Ivory Coast walionekana kuelewana zaidi na kudhibiti mpira chini ya uratibu wa Toure, huku Gervinho na Max Gradel wakitanua vyema kwenye wingi.

Ilikuwa ni vita kali uwanjani, ambapo Kolo Toure alikuwa na kazi ya kumdhibiti Adebayor wakati Vincent Bossou wa Togo hakufanya ajizi kuzuia madhara kutoka kwa nyota wa kimataifa, Didier Drogba.

Togo wanashiriki fainali hizi baada ya kushinda rufaa yao, wakipinga kufungiwa kutoshiriki fainali mbili kutokana na kujitoa fainali za mwaka 2010. Waligoma baada ya msafara wa timu yao kushambuliwa, watu watatu kuuawa.

Didier Drogba anacheza fainali za sita za AFCON, lakini kwa mechi ya Jumanne, wajina wake wa timu yake pia, Didier Ya Konan aling’ara zaidi.

Ama kwa upande wa mechi ya pili kati ya Tai wa Carthage (Tunisia) na Mbweha wa Jangwani (Algeria), wasiokuwa wavumilivu walitoka uwanjani na kuacha kicheko au kilio.

Hiyo ni kwa sababu timu zilitoshana nguvu kwa kwenda suluhu hadi dakika ya 89.

Alikuwa ni Youssef Msakni aliyewazawadia Tunisa bao dakika ya 90 na kupata pointi tatu muhimu katika kundi lao.

Hata hivyo, Algeria ndio walioanza vyema zaidi mchezo, na Islam Slimani alikosa bao katika dakika ya 29 kwa kiki yake kugonga mtambaa wa panya.

Ilikuwa mechi ya timu mbili zenye historia kubwa kwenye mashindano hayo, ambapo uzuri wake ni kwamba hapakuwa na uadui wa kukamiana sana, bali kuonesha mbinu za soka.

Kwa matokeo hayo, Algeria wameweka rekodi ya kushindwa kufunga walau bao moja katika mechi tano za fainali tofauti za AFCON.

Jumatano hii wenyeji Afrika Kusini wanatoana jasho na Angola wakati Morocco wakipimaba ubavu na Cape Verde.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

AFCON 2013 mwendo wa pole

Vijana wa Madiba wafunika AFCON