in , ,

THAMANI YA KIKOSI CHA 1.3B SIMBA ITAONEKANA HAPA

Kama kuna timu ambayo imewekeza vizuri mno kwenye msimu huu wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara basi ni Simba SC. Na wanastahili kupata matokeo wanayoyapata lakini pia kuwepo hapo walipo kutokana na ubora wa kikosi chao lakini bado hawajathibitisha thamani ya kikosi cha gharama ya takribani Billioni 1.3 kwa kuzifunga timu kama Mbao, Singida wala hata hao Gendamarie wenyewe.

Ndiyo! unaweza kusema Gendamarie walikuwa kwenye michuano ya Afrika lakini kwa ubora walionao hawakuwa na tofauti na hawa kina Njombe Mji wa hapa nchini.

Hawakuwa kipimo tosha kwa simba hii hata kidogo. Kocha anaesema kuwa alitegemea kufungwa goli 9-10 na Simba na kwamba kufungwa 4 tu ni dalili ya kuimarika anakupa picha halisi ya ubora hafifu timu hiyo kutoka Djibouti ilikuwa nao licha ya kuweza kucheza michuano hiyo ya kombe la shirikisho.

Shirikisho huwa ni sawa na Europa ligi tu kwa pale Ulaya ni sawa na timu tu kama Rosenborg au Vitesse zitakavyofuzu michuano hiyo kwa sababu tu zimemaliza wa kwanza kwenye nchi fulani na sana sana zinatimiza idadi na zinaishia kutolewa na hakuna hata anaeshangaa sana sana ni ajabu zenyewe zikifanya maaajabu hata ya kuvuka kundi tu.

Kwa miaka mingi timu zetu za Simba na Yanga zimekuwa zikipata wakati mgumu zinapokutana na timu kutoka kaskazini mwa Afrika lakini binafsi naamini huu ndio wakati sahihi wa Simba kuonesha thamani halisi ya kikosi chao.

Ile dhana ya kwamba waarabu hivi waarabu vile haitakiwi kuwepo. Kama kuna kitu ambacho kiliwagharimu Simba kwa miaka minne nyuma na kuwafanya kukosa ubingwa wa ligi kuu bara basi ni kutofanya uwekezaji wa kutosha lakini kwa sasa wana ubora mkubwa wa kushindana na wapinzani wowote kwenye shirikisho wakiwemo Al Masry na ndipo thamani yao watakapokuwa wameionesha hasa.

Simba wanaweza kuwa na mlima mkubwa zaidi kuliko ndugu zao Yanga licha ya wao kuwa na matokeo chanya zaidi lakini kulingana na rekodi zilivyo dhidi ya timu za Afrika ya kaskazini ni wazi kuwa huu ni mtihani mpevu lakini kuujibu ndio tunachotegemea kwa sasa na kikubwa kinachotushawishi kuamini hivyo ni thamani yao na ubora wa kikosi chao msimu huu.

Ubora wao hapa ndani umechagizwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji walioufanya hasa dhidi ya timu zisizokuwa na uwezo mkubwa wa kushindana na yenyewe sokoni lakini thamani halisi ya uwekezaji wao mkubwa utaonekana dhidi ya timu tishio kwenye hili kombe la shirikisho.

Report

Written by haatimabdul

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Carragher na kashfa ya kutema mate

Tanzania Sports

UNITED WANAPATA WANACHOSTAHILI ILA NI LAZIMA MOURINHO ABADILIKE