Menu
in , , ,

SPURS ANA NAFASI YA KUSHINDA DHIDI YA ARSENAL

Tanzania Sports

Kwa miaka ya hivi karibuni North London Derby imekuwa na mvuto
kutokana na Tottenham Hotspurs kuwa timu ya ushindani tofauti na miaka
mingi ya nyuma.

North London Derby ya 195 itakayopigwa katika uwanja wa Wembley,
wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23. Mara ya mwisho timu
hizi kukutana katika uwanja wa Wenbley ilikuwa mwaka 1995 katika nusu
fainali ya FA ambayo Arsenal alishinda goli 1 goli la Tony Adams.

Leo hii wanakutana katika mazingira tofauti na ya mwanzo. Mauricio
Pochettino amefanikiwa kuitengeneza timu yenye ushindani hali ambayo
inaonesha mechi hii itakuwa ya ushindani sana.

Kwanini nasema hivo??

Arsenal imekuwa na historia nzuri dhidi ya Tottenham Hotspurs, katika
mashindano yote
Tottenham ameshinda mechi 56 dhidi ya Arsenal na kutoa sare michezo 49 wakati
Arsenal akishinda mechi 76.

Hii ni historia ambayo ilitengenezwa kipindi ambacho Arsenal ikiwa
bora dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Msimu huu Tottenham Hotspurs imekuwa na matokeo ya kupanda na kushuka,
lakini tangu afungwe na Manchester City katika uwanja wa Etihad mpaka
sasa hajafungwa mechi yoyote katika michezo nane zilizopita, akiwa
amefanikiwa kufunga magoli 20 na kupata clean sheets nne (4) katika
michezo hiyo minane.

Inaonekana Tottenham Hotspurs imeshauzoea uwanja wa Wembley?

Mwanzoni mwa ligi Tottenham Hotspurs ilikuwa inahangaika kupata
matokeo chanya katika uwanja wa Wembley na hii ilitokana na sababu
mbili, ya kwanza ulikuwa uwanja mgeni kwao hivo kuna wakati walikuwa
wanajiona ugenini muda mwingi.

Sababu ya pili vipimo vya Wembley ni vikubwa ukilinganisha na vipimo
vya White Hart Lane

Kiufundi uwanja ambao unavipimo vidogo huwa unabana kipindi
unapotengeneza mashambulizi, ukizoea kutumia uwanja wenye vipimo
vidogo itakupa mtihani mgumu kwako wewe pindi unapoanza kutumia uwanja
wenye vipimo vikubwa.

Mwanzoni hiki kitu kiliwapa wakati mgumu sana Tottenham Hotspurs,
lakini kadri siku zinavyozidi kwenda wanaonekana kuuzoea uwanja huu

Mpaka sasa Tottenham Hotspurs wamecheza michezo 12 katika uwanja wa
Wembley bila kufungwa huku wakiwa wamefunga magoli 32 katika uwanja
huo.

Hiki ndicho ƙkitu ambacho kinaonesha utayari wa Tottenham Hotspurs
katika kutumia uwanja huu, na ugumu wa mechi hii unaanzia hapa kwa
sababu Arsenal ameenda katika uwanja wa Wembley kwa miaka minne na
kufanikiwa kubeba makombe matatu ya FA. Mara ya mwisho kwa Arsenal
kufungwa kwenye uwanja wa Wembley ilikuwa mwaka 2011 kwenye fainali ya
Carling cup dhidi ya Birmigham City.

Leo hii Arsenal inaenda Wembley ikiwa na rekodi mbovu msimu huu
inapocheza ugenini, imetoka kufungwa mechi mbili za ugenini dhidi ya
Afc Bournamouth na Swansea City.

Na mara ya mwisho kwao wao kushinda ugenini ilikuwa December 28 mwaka
jana aliposhinda dhidi ya Crystal Palace.

Kipi kimekuwa kikiwagharimu Arsenal katika mechi za ugenini??

Hapana shaka safu yao ya ulinzi imekuwa ikifanya makosa mengi binafsi.
Haina maelewano na hawajipangi vizuri hasa hasa wanapokuwa
wanashambuliwa kwa mashambulizi ya kushitukiza “counter attacks”.

Mara nyingi wanapokuwa wanashambuliwa mabeki hufuata mtu aliye na
mpira hali ambayo hutengeneza uwazi eneo la nyuma, uwazi ambao
hushindwa kuzibwa kutokana na kukoseana kwa mtu wa kuziba ( ku cover),
hivo hujikuta wanafungwa magoli mepesi.

Kwa aina ya wachezaji wa mbele wa Tottenham Hotspurs kwa kasi yao ni
virahisi sana kuwalazimisha Arsenal kutengeneza uwazi katika eneo la
nyuma.

Tottenham Hotspurs mechi kadhaa zilizopita ilikuwa na tatizo hilo
lakini kurejea kwa Toby Alderweireld kutakuwa na msaada kwao kwa
sababu siyo beki ambaye anaweza kutengeneza uwazi eneo la nyuma,
lakini kama Arsenal wakilazimisha kuna uwezekano wa yeye kutengeneza
uwazi katika eneo la nyuma.

Je ni kwa namna gani Arsenal wanatakiwa kumlazimisha Toby Alderweireld
kutengeneza uwazi eneo la nyuma?

Tukumbuke atacheza eneo la beki wa kati upande wa kulia, upande ambao
Trippier aracheza kama beki namba mbili.

Trippier amekuwa na kiwango kizuri hivi karibuni, amekuwa
akitengeneza nafasi nyingi za kufunga kupitia krosi, namna pekee ya
kuepukana na madhara haya kutoka kwa Trippier , Arsenal wanatakiwa
wamfanye awe busy kukaba, kipindi mashambulizi yatakapozidi katika
upande wake, lazima Toby Alderweireld aje upande wa kulia kumsaidia
kukaba, anapokuwa anakuja upande huu basi atakuwa ameacha uwazi eneo
la katikati hivo kutawapa nafasi nzuri kwa Arsenal kutumia uwazi huo.

Pili, Arsenal wanatakiwa wawalazimishe mabeki wa kati wa Tottenham
Hotspurs kukabia eneo la mbele ili eneo la nyuma liwe wazi.

Uwepo wa Harry Kane utakuwa na madhara kwa Arsenal, tangia akutane na
Arsenal kwa mara ya kwanza mwaka 2015 amefanikiwa kuifunga magoli 5.
Na amekuwa na kiwango kizuri katika uwanja wa Wembley akiwa amefunga
magoli 7 katika mechi 5 zilizopita katika uwanja huu.

Eneo lipi Spurs wanajivunia kwa sasa??

Eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na watu wengi wanaoshuka katikati
kuwasaidia Dier na Dembele. Son, Erricksen na Delle Alli wamekuwa
wakishuka katikati kwa nyakati tofauti kuongeza idadi ya wachezaji
katika eneo la katikati mwa uwanja.

Hii inaenda sambamba na kiwango cha Son katika uwanja wa Wembley
ambaye kahusika katika magoli 8 kwenye michezo 6 aliyocheza Wembley,
amekuwa na msaada mkubwa kwa spurs.

Pierre Emirick Aubameyang rekodi yake dhidi ya Tottenham hotspurs ina
nafasi katika mechi ya leo?

Amefanikiwa kuwafunga spurs magoli manne katika mechi nne alizowahi
kukutana nazo.

Hii inampa ujasiri mkubwa kuelekea mechi ya leo , ujasiri ambao
utamwezesha yeye kufanya vizuri

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version