in , , ,

SIMBA YAPAA KILELENI

 

Mabao mawili ya Hamis Kiiza aliyofunga ndani ya dimba la Kambarage jijini Shinyanga dhidi ya Stand United jioni hii yaimeifanya Simba SC kukwea mbaka kwenye nafasi ya kwanza kwenye jedwali la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-1.

Hamis Kiiza ambaye alikosolewa kwa kushindwa kuzitumia nafasi za kufunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar leo alirejea kwenye ubora wake kwa kuifungia timu yake mabao kwenye dakika ya 39 na dakika ya 47 huku David Osman akifunga lile la Stand dakika za mwishoni.

Mchezo huo uliokuwa na msisimko kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa zaidi na Wekundu hao wa Msimbazi hasa kwenye kipindi cha pili ambapo walionyesha makali zaidi kwenye safu ya kiungo iliyoundwa na Justice Majabvi, Said Ndemla, Ibrahim Ajib na wengine.

Simba walifanikiwa kupata bao la kwanza mnamo dakika ya 39 baada ya Hamis Kiiza kumalizia kazi nzuri ya Said Ndemla na kufunga bao maridadi lililoifanya timu yake kujiamini na kucheza mpira mzuri zaidi.

Bao hilo lilidumu mbaka kufikia mapumziko. Kwenye kipindi cha pili Simba walirejea na makali zaidi wakijaribu kutengeneza nafasi za mabao na wakafanikiwa kuongeza bao la pili dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi hicho cha pili.

Stand United waliamka kwa kufanya mashambulizi wakipiga mashuti kadha ya hatari kupitia kwa Elias Maguri na Cholo lakini hawakuweza kuvuna chochote mbaka zilipofika dakika za lala salama ambapo Osman aliwapatia bao la kufutia machozi.

Ushindi huo sio tu unalipa kisasi cha kipigo cha 1-0 walichokipata Wekundu hao mara ya mwisho walipokaribishwa na Stand kwenye dimba la Kambarage, bali pia unawapaisha kutoka nafasi ya tatu mbaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na alama 45.

Yanga ambao jioni hii wameibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Afrika huko Mauritius dhidi ya Cercle de Joachim wanabaki kwenye nafasi ya pili na alama zao 43 wakiwa wamecheza michezo 18 pekee tofauti na vinara Simba ambao leo wamecheza mchezo wao wa 19.

Azam FC ambao kesho wataingia uwanjani kuwavaa Coastal Union jijini Tanga, wapo kwenye nafasi ya 3 wakiwa na alama 42. Hata hivyo mabingwa hao wa Afrika Mashariki wameshacheza michezo 16 pekee.

Ligi imefikia patamu, utabiri juu ya timu gani itanyanyua ubingwa wa msimu huu unazidi kuwa mgumu. Simba ambao hawakutarajiwa kuweza kuleta upinzani wa kiasi hiki sasa wamekuwa moto wa kuotea mbali. Bila shaka mbinu za mwalimu mzalendo Jackson Mayanja ndizo zilizowafikisha hapa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Hapatoshi Man City, United, Chelsea

Tanzania Sports

Man U hoi, Chelsea kicheko