in , , ,

SIMBA WAMEBEBA DHANA YA SIMBA MBUGANI

Mnamo tarehe 25 mwezi wa 7 mwaka wa 2024 klabu ya Simba Sports Club imefanya tukio la kihistoria. Tukio lenyewe ni uzinduzi wa wa jezi mpya za msimu wa mwaka 2024/2025 kwa staili ya aina yake. Wamefanya uzinduzi huo katika mkoa wa Morogoro katika mbuga maarufu barani Afrika ya Mikumi. Tukio hilo ndio ufunguzi wa wiki ya Simba ambayo kilele chake ni siku ya Simba day.  Mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao ni wakazi wa jiji la Dar es salaam walienda mkoa huo jirani kwa kutumia usafiri wa Treni ya kisasa ya SGR.Yatarajiwa matukuio mbalimbali ambayo yatafanywa katika wiki hiyo yatasisismua wakazi wa maeneo husika ambayo matukio hayo yatakapowakuta.

Kwenda kwao kuzindulia jezi katika mbuga ya Mikumi kwanza bila ya shaka kunabeba ila dhana ya klabu yao kuitwa Simba kwani kwenye mbuga hiyo wanyama aina ya Simba ni mojawapo ya wanyama ambao wako kwa wingi sana. Pili wamezindulia hapo kwa ajili ya kukuza utalii wa ndani. Mbuga ya Mikumi ni mojawapo ya vivutio vya ndani ambavyo vipi nchini Tanzania na klabu hiyo kubwa barani yenye washabiki wengi baranu Afrika kuzindulia jezi zao hapo bila ya shaka ni promosheni kubwa sana ambayo mbuga hiyo itakuwa imeipata.

Mkoa wa Morogoro nao utanufaika na ugeni huo kwani mashabiki hao wanaoingia mji huo lazima walale na wakilala ni lazima watatumia pesa zao na hivyo kusababisha kuongezeka kwa mzunguko wa pesa katika mkoa huo kwa mda ambao mashabiki hao waliokuwepo hapo. Jezi zao za mwaka huu kama zilivyokuwa za mwaka jana zimechapishwa na kampuni ya Sandaland. Zitasambazwa na kampuni hiyo halikadhalika. Katika muundo wa jezi hizo kuna mahala ambapo zimeandikwa maneno “SANDA”. Maneno hayo yamekuwa ni gumzo na mjadala mkubwa mitandaoni nchini Tanzania huku makundi katika mijadala juu ya jezi hizo yamegawanyika kuna baadhi wanasifia na wengine wanakosoa. Kama wasemavyo baadhi ya wataalamu wa mahusiano ya umma kwamba “there is no negative publicity” na hapo Simba wamejiongezea jina kwa mwaka huu.

Pili kwa kuamua kutumia usafiri wa treni ya SGR klabu hiyo imeutangaza usafiri huo kwa umma wa Tanzania kwani watu wengi sasa watazidi kufuatilia usafiri huo na wengi wao wataupanda kwani ni usafiri ambao ni wa haraka na watanzania wengi wa kawaida watazidi kuwa wanautumia mara kwa mara. Huku wakiwa Morogoro walisafiri na watu wengi maarufu nchini Tanzania ikiwemo waandishi wahabari ambao walisaidia kufanya safari yao kuweza kuonekana kwa umma mkubwa wa Tanzania. Wamebuni msemo wa msimu ambao ni “ubaya ubwela” msemo huu umebebwa na watu wengi sasa mitandaoni hata na wale ambao sio mashabiki wa Simba kwenye mambo yao nao wamekuwa wanautaja msemo huu. Na yawezekana msemo huu ukaja kuingia kwenye misamiati ya lugha ya Kiswahili kwa kusanifishwa siku za usoni. 

Ilipofika mnamo julai 26 bodi ya klabu hiyoilimteua bwana Francois Resis kuwa afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo. Mtendaji huyo mpya ni raia wa Rwanda ambapo ana uzoefu na uelewa tosha kwenye masuala ya soka la kisasa. Kwanza ni mtaalamu wa uhasibu mwenye cheti cha kimataifa cha IFSAS, Ana leseni ya ukocha ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA license B. tunamsubiri kumuona kiongozi huyo mageuzi ambayo atayaleta katika soka la Tanzania. Na mashabiki wa Simba kwa sasa wanasubiri kuiona klabu yao uwanjani katika msimu mpya wa ligi ya NBC ni mafanikio gani klabu yao wapendwa watayafikia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

MAPATO NA MATUMIZI YA VYAMA VYA MICHEZO..

Tanzania Sports

COASTAL UNION KUNANI PALE?