in

LoveLove SurprisedSurprised

SIMBA BINGWA 2019/2020

SIMBA

Tanzania Prisons kidogo iharibu furaha ya Simba

Licha ya kutoa sare ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliofanyika mkoani Mbeya katika uwanja wa Sokoine timu ya Simba imetetea ubingwa wake kwa mara ya tatu mfululizo.


Tanzania Prisons ilionekana kuhitaji kuharibu sherehe ya Simba kwa kucheza kwa kujituma wakiamini kuwa wangepata, ushindi ambao ungewasogeza nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.


Hadi kufikia jana Simba SC  imecheza michezo 32, imeshinda mara 25 ikifungwa Mara 3, timu hiyo imetoa sare michezo 4, imeshinda magoli 69 na kufungwa 16.


Timu pekee ambayo imefunga magoli 69 mengi zaidi kuliko timu yoyote ikizizidi timu ya Yanga na Azam ambazo zikiwa nafasi ya pili na ya tatu.


Simba imetangaza ubingwa huo ikiwa bado michezo mitano mkononi ambapo sasa vita imehamia kutafuta nafasi ya pili, na kushuka daraja huko zinawahusu Azam na Yanga.

Baada ya bingwa kujulikana timu hiyo itageukia michuano ya kombe la Azam maarufu kama ‘Azam Sports Federation Cup’ (ASFC) ambapo itapambana na timu ya Azam uwanja wa taifa Dar as Salaam.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Harmonize

Harmonize kupeleka Bongofleva bungeni?

Matukio ya Simba hadi ubingwa

Matukio ya Simba hadi ubingwa