in , , ,

‘Saudia wasiuziwe Newcastle’

Newcastle United

Bodi ya Ligi Kuu ya England (EPL) imetakiwa kuzuia wawekezaji wa kutoka Saudi Arabia kununua klabu ya Newcastle, kwani malengo yao si kuendeleza michezo bali matakwa ya kisiasa.

Mpango wa mauzo ya klabu hiyo ulielezwa kwamba ulikaribia kukamilika, kwa ntaraka husika kusainiwa kwa ajili ya kuwezesha klabu kutoka mikononi mwa Mike Ashley kwenda kwa Wasaudia, akiwamo Mwana Mfalme Mohammed bin Salman.

Wakati mipango ikiendelea, kumetokea madai kwamba klabu hiyo ya kaskazini mashariki mwa England inayouzwa kwa pauni milioni 300 si vyema kwenda kwa Wasaudia. Bein Sports wameitaka bodi ya ligi kuingilia kati na kuzuia kwa vile wawekezaji hao wanahusishwa na ukiukwaji wa haki za matangazo.

Bein Sports ni moja ya washirika wakubwa wa utangazaji wa EPL, wakiwa na makazi yao Qatar wanadai kwamba Saudia wamekuwa wakijihusisha na kutangaza ligi hiyo kwa magendo, hivyo si vyema kuwauzia watu wa aina hiyo klabu, kwani wameonesha si washirika wema.

Uingiliaji kati wa watangazaji hao unakuja baada ya Shirika la Haki za Binadamu – Amnesty International – kumwandikia Ofisa Mtendaji Mkuu wa EPL, Richard Masters kueleza kwamba kuchukua Newcastle kwa Waarabu hao kunaweza kuwafanya kutumia kama funika funika ya vitendo visivyokuwa vya kimaadili, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Bodi ya Ligi ilikuwa ni moja ya taassi na wasimamiaji wa ligi waliowataka watangazaji wa satelaiti wa Saudia – Arabsat kuacha kutoa jukwaa kwa mtandao wa kiharamia uliokuwa unaidhulumu ligi kwa kuteka na kurusha matangazo ya mechi zake bila kuwa na haki wala kulipa.

Mtandao huo, unaojulikana kama BeoutQ, kwanza ulianza kwa kutiririsha matukio ya michezo kinyume cha sheria mwaka 2017. Licha ya jitihada za taasisi mbalimbali kuutaka usitishe uharamia huo, uliendelea.

Julai mwaka jana EPL walisema kwamba walizungumza na kampuni tisa za sheria za Saudia ambao ama walikataa kuwafanyia kazi au walifanya na kufika mahali wakaacha kuendelea kutoa huduma za msaada ili kuwabana wenye mtandao huo.

Yousef Al-Obaidly, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bein, amewaandikia wenyeviti wa klabu za EPL kuwaeleza kwamba kuchukuliwa kwa Newcastle na Wasaudia hao kutawasababishia hasara kubwa kifedha kwa maana ya mapato ya kibishara na kihadhi kwa klabu hizo.

“Msimu wa EPL utakapoanza tena katika miezi ijayo, matangazo ya ligi hiyo kwa mechi wanazotaka yataendelea kurushwa isivyo halali na BeoutQ. Wanapata kupitia IPTV na haki hizi batili ziliuzwa kwa kiasi kikubwa nchini Saudi Arabia na MENA (eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini),” anasema mtendaji huyo.

Anaongeza kwamba, wakati klabu zikiwa katika hali mbaya kiuchumi kutokana na athari za virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, mechi kuahirishwa na watu kujifungia ndani, athari za kiuchumi kwa klabu zitazidi kuwa kubwa kutokana na maharamia hao wa Mashariki ya Kati.

Katika barua nyingine kwa Masters, Al-Obaidly anaiomba Bodi ya EPL kuchukua hatua dhidi ya Saudi Arabia, kutokana na ukweli kwamba ilishiriki katika kuzindua, kupromoti na kuendeshwa kwa huduma za BeoutQ. Kwamba changamoto ni kubwa kwa EPL katika kulinda haki zake ambazo zimeshaibiwa kwenye utangazaji wa mechi, hivyo si sahihi kuuzia watu hao hao klabu ya Uingereza

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Wachezaji Man U waumia

Tanzania Sports

Bundesliga inarejea