Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, amekuwa katika klabu ya Arsenal tangu mwezi wa Mei mwaka 2004 na anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Cesc Fabregas, aliyehamia klabu ya Barcelona wiki hii.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema: “Van Persie ni kiongozi kutokana na uchezaji wake, kutokana na ushawishi wake na ari aliyonayo ya kushinda.
“Amekuwa aktika klabu hii kwa muda mrefu na kiufundi ni kiongozi.”
Van Persie, ambaye msaidizi wake anakuwa mlinzi Thomas Vermaelen, amesema amefurahia kupata nafasi hiyo.
“Kuwa nahodha, unakuwa ni balozi kwa klabu na nipo tayari kwa hilo,” amesema Van Persie. “Nimekuwa katika soka kwa zaidi ya miaka 10, kwa hiyo naelewa namna ya kutekeleza majukumu yangu.
“Kila mara unalazimika kuonesha heshima mbele za watu.
Van Persie hataiongoza Arsenal katika mechi dhidi ya Udinese usiku wa Jumanne katika kuwania nafasi ya kufuzu mechi za Ubingwa wa Ulaya, kwa sababu anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja na Uefa.
Lakini atachukua hatamu za kuiongoza Arsenal watakapomenyana na Liverpool katika uwanja wa Emirates siku ya Jumamosi kwenye pambano la Ligi Kuu ya Soka ya England.
Tunasubiri mechi ya ligi kuu dhidi ya liverpool kwa hamu