in , , , ,

Rio Ferdinand aitwa Kamisheni ya FA

 
Nahodha wa zamani wa England ambaye hivi karibuni alijitoa kwenye timu hiyo, Rio Ferdinand ameitwa kwenye Kamisheni ya Chama cha Soka (FA).

Ferdinand ambaye amepata kukumbwa na utata mara kadhaa, ameitwa kwenye kamisheni hiyo pamoja na Kocha Mkuu wa England, Roy Hodgson.

Wahusika hao wameitwa kwa ajili ya kuboresha soka na kuona ni kwa jinsi gani wachezaji wengi zaidi wa England wataweza kucheza katika soka klabu za juu nchini.

Uteuzi huo umekuja siku moja tu baada ya mjumbe pekee mwanamke kwenye bodi hiyo,
Heather Rabbatts kulalamikia muundo wa kamisheni ambayo ilikuwa na weupe na wanaume tupu.

Hodgson (66) na ambaye ni Mwingereza, amefanikiwa kuivusha timu ya taifa kwenda kucheza Kombe la Dunia Brazil mwakani.

Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke, hata hivyo, anasema walishamfikiria Ferdinand muda kadhaa uliopita lakini walikuwa wakijadiliana naye na klabu yake ya Manchester United ili kupata uhakika iwapo ataweza jukumu lake hilo jipya, hasa ikizingatiwa kwamba bado ni mchezaji.

Dyke ameweka malengo kwa England kufika nusu fainali ya Euro 2020 na kutwaa Kombe la Dunia 2022, ambapo anasema alichelewesha kumtangaza Hodgson akisubiri hatima ya England kufuzu kwenda Brazil au la.

Ferdinand aliyezaliwa 1978 alianza kulichezea taifa la England 1997 ambapo kabla ya kujiunga Man United akitokea Leeds United kwa pauni milioni 30 mwaka 2002 alikuwa akichezea West Ham.

Ferdinand amechezea England mechi 81 na kufunga mabao matatu ambapo mechi ya mwisho ilikuwa Juni 2011 dhidi ya Uswisi.

Aliitwa kwenye kikosi cha mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya San Marino na Montenegro Machi mwaka huu lakini alijitoa kwanza akidai alikuwa anaumwa mgongo kisha Mei akatangaza kujiuzulu soka ya kimataifa.

Alipingwa vikali na wadau kwa kupanda ndege kwenda Mashariki ya Kati kuchambua mechi za England badala ya kuonesha uzalendo kwa kucheza mechi alizokuwa ameitwa, na wataalamu walisema kama alikuwa na matatizo ya mgongo haingekuwa rahisi kupanda ndege kwenda Mashariki ya Kati kwa kazi hizo na baadaye kuchezea klabu yake, Man United.

Hata hivyo, kocha wake wakati huo, Alex Ferguson alimtetea, akisema walikuwa na programu maalumu ya mazoezi na kujipanga mechi za kutumikia klabu hiyo.

Ferdinand ni beki wa kati na anasubiriwa kwa hamu atakachochangia kwenye kamisheni hiyo. Wengine walio kwenye jopo hilo ni Makamu Mwenyekiti wa FA, Roger Burden, kocha wa zamani wa England, Glenn Hoddle na mlinzi wa zamani wa England, Danny Mills.

Wengine ni Mwenyekiti Chama cha Mameneja wa Ligi, Howard Wilkinson, Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa, Ritchie Humphreys, Mwenyekiti wa Ligi ya Soka, Greg Clarke na Mkurugenzi wa Soka wa Crewe, Dario Gradi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Simba, Yanga hakuna mbabe….

Machava FC, yaanza kujitetea Ligi Daraja La Tatu, Kilimanjaro