Kuanza kwa Alexie Sanchez kama mshambuliaji wa mwisho jana lilikuwa
wazo zuri sana kwa Arsene Wenger.
Kwanini nasema hivo?
Lengo kuu la Arsene Wenger lilikuwa kumtumia Alexie Sanchez kuivunja
safu ya ulinzi ya Manchester City kupitia kasi yake.
Kasi yake pia ilitosha kumwaminisha Arsene Wenger kuwa Sanchez
angeweza kuwafanya Stones na Otamendi kukabia katika eneo lao na
wasiweze kupata nafasi ya wao kusogea mbele kusukuma mashambulizi.
Lakini hili halikufanikiwa hasa hasa kipindi cha kwanza.
Kipi kilichofanya huu mpango wa Arsene Wenger usifanikiwe?
Arsene Wenger alijaribu kuwaanzisha Francis Coquelin na Xhaka kwa
pamoja kwa lengo moja mahususi.
Coquelin alikuwepo pale kushinda mipira yote ya katikati, ili kumpa
nafasi Xhaka kuanzisha mashambulizi kwa mipira mirefu kwa Sanchez ili
iwe rahisi kwake kuipita safu ya ulinzi ya Manchester City.
Lakini Coquelin hakufanikiwa kutimiza lengo la Wenger.
Hali iliyopelekea Xhaka pia awe anarudi chini kwa ajili ya kushinda
mipira , hivo kuacha uwazi mkubwa kati ya Xhaka , Ozil na Sanchez.
Ozil hakufanikiwa kwa kiasi kikubwa yeye kuziba uwazi wake na Sanchez
kwa sababu hakuwa anafanikiwa kukaa na mipira, hata wakati ambao
alikuwa anakaa na mpira hakuwa na maamuzi mazuri ya kutengeneza nafasi
kwa Sanchez.
Ubora wa Manchester City upo kwa Kelvin De Bryune ambao unachagizwa
kwa kiwango kikubwa na ubora wa Fernandinho.
Fernandhinho alikuwa na uwezo mkubwa wa kuisukuma timu na kutengeneza
umbo zuri la timu.
Mabadiriko ya kumtoa Coquelin na kumwingiza Lacazzete yalikuwa na tija?
Hapana shaka Wenger alifanya jambo la busara baada ya kuona mbinu yake
ya awali kuwa imeshindikana.
Kumrudisha Ramsey kucheza kama Box to box Middfielɗer kuliongeza uhai
katika eneo la kati.
Awali alikuwa anacheza kama Orthodox , nafasi ambayo ilikuwa haimpi
nafasi ya yeye kuwa huru zaidi.
Lacazzate aliongeza nguvu ya kushambulia kule mbele, hali ambayo
ilimfanya Arsenal kurudi mchezoni baada ya kufungwa goli 2-1.
Lakini refa alikuwa kuwavunja moyo baada ya kuruhusu goli la kuotea,
goli ambalo liliwavunja nguvu Arsenal.
Kuna uwezekano wa Jose Mourinho kubadirika kwenye mbinu zake ??
Ni swali ambalo jibu lake natamani kuliona katika maisha yangu.
Maisha yote ya kufundisha mpira, Jose Mourinho amekuwa na utamaduni wa
yeye kuamini kwanza ulinzi kisha kushambulia kunafuata.
Hali ambayo imemfanya awe na tabia ya kujilinda sana kuliko
kushambulia hasa hasa kwenye mechi muhimu.
Ipi ilikuwa nguvu ya Chelsea?
Uimara wa Kante na ubora wa Hazard ndivyo vitu ambavyo viliifanya
Chelsea iwe hai kwa muda mrefu kwenye hii mechi.
Kante alifanikiwa zaidi kuilinda safu ya ulinzi pamoja na kusukuma
mashambulizi .
Hali iliyokuwa inafanya viungo wa kati wa Chelsea kuongezeka
wanapokuwa wanashambulia , Chelsea wakati wanashambulia , Kante,
Bakayoko, Fabregas walikuwa wanahusika kushambulia.
Hali hii iliwafanya Matic na Herrera kuwa chini muda mrefu, kitu
ambacho kilipelekea Mickhthryian kushuka chini zaidi kutafuta mpira.
Hiki kilisababisha uwazi kati yake na washambuliaji wa mbele, kitu
ambacho hakikumpa nafasi ya yeye kutengeneza nafasi nyingi za kufunga
kwa sababu hakuwa na kiungo mchezeshaji mzuri katika eneo la kati la
uwanja.
Ni ukweli uliowazi kutokuwepo kwa Paul Pogba kumekuwa na madhara hasi
kwa kikosi cha Manchester United.
Pogba ndiye ambaye alikuwa anawachezesha Mickhtryian pamoja na Lukaku.
Andreas Christensen hakumwangusha Conte?
Ulionekana kama uamuzi wa kushangaza kwa Conte kutonweka David Luiz
kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya timu kubwa na ngumu.
Jambo lililoshangaza zaidi ni kutomweka hata kwenye orodha ya
wachezaji ambao wangehusika na mechi ile.
Jambo la ajabu ni Conte kumwamini , Christensen kijana wa miaka 21
katika mechi ngumu.
Lakini kijana huyu alionesha ukomavu wa hali ya juu katika kuwazuia
kina Lukaku na Rashford.
Kama Chelsea inataka irudi vizuri kwenye mbio za kusaka ubingwa
wanatakiwa wamuombee Hazard awe katika kiwango kizuri kama cha jana.