*Man City wacheka, Liverpool doro
Sasa ni rasmi kwamba Queen Park Rangers (QPR) wameungana na Burnley kushuka daraja.
QPR walipata adhabu kali ya kufungwa mabao 6-0 na Manchester City kwenye uwanja wao , wakiwa wamefanya mchezo wa kushuka, kupanda na kushuka kwa misimu mitatu.
Kwa ushindi huo, Mancester Cit wameendelea kujiimarish katika nafasi ya pili, wakiwa na pointi tatu zaidi ya Arsenal wanaoshika nafasi ya tatu, japo wana mechi mbili mkononi zaidi ya Man City.
Aliyewapulizia sumu zaidi QPR ni mshambuliaji Sergio Aguero aliyefunga mabao matatu kutokana na ulinzi mbovu wa QPR.
Mabao mengine yalifungwa na beki Aleksandar Kolaro, kiungo James Milner naDavid Silva na kujiimarisha katika nafasi ya pili, wakiwazidi Arsenal pia na uwiano wa mabao tisa, japokuwa Arsenal wana michezo miwili mkononi, ambapo Jumanne hii watacheza na Swansea.
Katika mechi nyingine, Liverpool wamekwenda sare ya 1-1 na Chelsea, kwenye mechi iliyopigwa Stamford Bridge na kuwapa Liverpool firsa ngumu ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) na sasa huenda wakaangukia Ligi ya Europa.
Mabao ya John Terry kwa Chelsea na Steven Gerrald, wote manahodha wa klabu zao yalisababisha timu hizo kwenda sare.
Kwa upande mwingine, QPR sasa wanakabiliwa na faini ya pauni milioni 58, kutokana na kukiuka kanuni za uungwana katika matumizi ya fedha, ambapo walimwaga fedha kupanda daraja na kujaribu kubaki juu.
Baada ya Burnley kushushwa daraja na QPR, kinachosubiriwa ni iwapo Hull wataepuka kikombe hicho, kwani ndio wa tatu walio kwenye eneo bobu.
QPR wana pointi 27, Burbley 29 wakati Hull wanazo 34 na wanatakiwa kujitahidi kwenye mechi mbili zilizobaki, lakini wakitakiwa waombe kwamba matokeo ya mechi nyingine yawape faida.
Wengine ambao bado wapo kwenye hatari ya kushuka daraja ni Newcastle, Sunderland, Leicester na Astona Villa, kwani Hull walio kwenye eneo hatari wanaweza kufikisha pointi 40 wakati Villa wanaoshika nafasi ya 14 wanazo pointi 38.
Comments
Loading…