MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na NHIF.
Makubaliano hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.
Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilizo bora. “ Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa, PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake. Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha. wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.